Rafiki alieleta zegwee maskani!

zado-blue

Member
Apr 2, 2022
59
34
Habarin, wana JF wezangu niko na ka kipande ka uzi nataka niwapatie.

Ilikuwa April 21. Mwaka 2020 niko zangu mishe mishe kipande fulani cha Moro na pambania 10 zangu.

Wachi wachi simu inaingia ni Maza nikapokea tukabonga pale aka nipangilia kuwa Babu anatoka zake mbeya na Precision Air na kuja jiji la (Daudi) a.k.a nyingi Dar-es-salama kwaajili ya matibabu inabidi uje kumpa support.

Nikasema sio kesi kesho yake nikaingia zangu kwa bus uyo mpaka maskani kweli mzee nikamkuta story za kule tuka peana hakuwa that serious lkn alitakiwa kufanyiwa operation days zika songa check up nyingi niko na mzee tunaenda tunarudi ikafika day ya operation ikawa good tu mzee akaruhusiwa alikuwa poa tu badthing akazidiwa.

Day yenywe ikawa hard mkimbizano huku kule madactari wakaniruhusu nitoke out so nika agree
Nko flow ya chini naona pisii fulani chotara c chotara iko apo tu. Nikawaza nikasema ngoja ni refresh unajuwa kuwa hospital for a long time unaona mambo mengi unaweza uka okoka.

Nikaisogelea na kuipa salamu ikawa Attracted na meme so it's was ma lucky day pia ma baddest day ever mtoto aka nikatia ma code nikajuwa ntalaza shingo siku si mingi tuka agana akasepa. Kidogo naitwa chumba cha "ICU" doc ana sema una kifua jikaze bac mzee akaw ameondoka.

Time imefika 26 November 2020 ndo mzee alifariki so kama unavyo elewa arrangement za mazishi kwetu wa kristo zina chukuwa kidogo time tukutane ndugu tujikusanye tusepe kwa pamoja ikawa ivyo tuka wasili green city kumpumzisha mzee bac ikawa ni majii tu stak semezana na mtu ku memories zile good moments .
Dec 5 baada ya mazish me nikawa mtu wa kwanza kurudi maskani kuweka mjengo fresh cos palikuwa apako good.

Niko home mida mibovu txt inaingia "hey price charming" nika mjibu kumbe upo akanipea pale salamu za pole story za apa na pale nikamuuliza una fanya mishe gani akasema nime maliza degree yangu niko tu home thinkn nn cha kufanya

Ilikwa 22 Dec 2020 kama una vyo jua 23 ni X-ms eve aka nialika niiende anapo ish apakuwa mbali ni mbweni tena kwa miguu tu nikafika.

Tuka enjoy for real nilimkubali mtoto fulani makinj sema siku laza shingo love happens sio u force japo alinitengenezea mazingira ila nili sita tu.

Ikawa night mbovu nikamuaga .. me uyo na zawadi juu ya maziwa wachi wachi mpaka home .

Days zika songa sherehe zika pita tukawa tuna wasiliana vizur tu akanimbia ameanza kufanya production ya pilipili aondokane na utegemezi nika mcongrats pale kuwa ni brave mida ya saa sita mchana aka nicheck kuwa ana pita maeneo ya home nika sema si mbaya kumkarbisha maskani pia apajue na wazee wamuone.

Kama unavyo juwa vi foleni foleni vya apa na pale pengine na story on the way mtoto alifika jion fresh .
Akanielekeza alipo nika mfuta imekuwa saa moja jioni hiyo tuka fika home picha linaanza mtoto ana sema mijengo kama hii mikubwa kuna mambo mengi yana happen nika mwambia kokote tu ata ukiwa mjengo mkubwa au mdogo as long wana ishi binadamu lazima mambo yaweko tu.

Reaction ya wazee ilikuwa noma ilkuwa kubaya ndani nadhani walijuwa nimekuja kumtambulisha mchumba kumbe me nilimleta rafik japo urafiki wetu unge zaa penzI.

Basi bhna mtoto alitamani aridh ifunguke azame ndani lkn haikuwa ilibd nimvushe mtoto side be
Na kuwaeleza wazee Wat happened kuwa ange fika mapema sema kuna mambo zilitokea on the way.

Najaribu tu kuwaza wazee wanatupeleka shule tunajifunza western culture na wanataka tuishi African culture

End
 
Back
Top Bottom