Radio za Kilugha...

Chief

JF-Expert Member
Jun 5, 2006
2,378
2,000
Ni takriban miaka zaidi ya 60 imepita tangu kupata uhuru. Nyerere, raisi wa kwanza alifanya juhudi kubwa kuuondoa ukabila na kuweka utaifa mbele. Kwa hili alifanikiwa Sana.

Katika kipindi hiki, tumeshuhudia watu wa makabila mbalimbali wakioana bila shida yeyote. Lakini, moja ya athari ya umoja huu wa kitaifa ni kupotea kwa lugha za makabila yetu. Si ajabu kuona walioona wa kabila tofauti, watoto wao hawajui lugha yeyote ya wazazi wao.

Vile vile, kuenea kwa kiswahili kama lugha ya taifa kumesababisha lugha za makabila kupotea kidogo kidogo. Miaka 50 ijayo, waweza kuta ni watu wachache wanaoweza kuongea kigogo, kiha etc.

Kwa hiyo basi, napendekeza kuwa serikali iruhusu Radio/TV mbalimbali kutangaza katika lugha mbalimbali iki kutunza hizo lugha zisiotee. Na katika ngazi ya kitaifa, serikali itengeneze archive (Kama haipo ) ya lugha zote ambazo itajumuisha audio/video records za lugha, tamaduni na maandishi ya lugha mbalimbali.
Idara Itakayofanya kazi hii yaweza kujiunga na DELAMAN

About – DELAMAN

Faida kubwa ni kuwa tutatunza kwa vizazi vijacho mila, lugha, tamaduni na desturi za makabila ya nchi yetu.
 
Mdomo bakuli

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
3,250
2,000
Moja kati ya mawazo ya kijinga na kipumbavu zaidi kuwahi kutolewa hapa JF...
Siwezi kukwambia mengi ila moja kati ya vitu vinavyoleta UKABILA nchini KENYA ni hivi....
Dunia ya sasa ya kuoana makabila MBALIMBALI we bado unaleta habari hizi? Ndo maana wachangiaji wengi wanapita kimya kimya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri hujui faida ya tamaduni mila na desturi. Sijapinga watu kuoana wa lugha mbalimbali bali nina promote preservation ya cultures, language etc za makabila mbalimbali ambazo zinaelekea kutokomea. Sijui kama unaona umuhimu wa hili.
 
1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,745
2,000
Ni nini umuhimu wa lugha ya kikabila.
Ikiwa kila kabila linaweza kuwasiliana na kabila jingine bila kikwazo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom