Radio Free Africa Wajirekebisha

Radio Free Africa Wajirekebisha

Swat

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
4,201
Reaction score
2,002
Ni katika kipindi chao cha magazetini asubuhi.

Kuliwahi wekwa uzi humu kwamba kipindi chao cha kupitia magazeti asubuhi kimejaa matangazo ya biashara na habari za magazeti zinasomwa kiduchu tu.

Kipindi kilikua na matangazo kumi kabla, matangazo kumi katikati na matangazo kumi mwishoni!.Watu wengi wiiponda kwa mpangilio huo.

Kwa karibu wiki sasa nimekua nasikiliza kipindi hicho na kwa sasa wanaweka matangazo mawili mwanzo,mawili kati na mawili mwishoni.

Tena leo ndio ilikua poa zaidi,waliweka tangazo moja tu mwanzoni, mawili katikati na kama matatu mwishoni.

Taasisi nyingine zijifunze kwa hawa katika kushughurikia malalamiko ya wananchi.

Kudos.
 
Halafu ni kama vile msomaji wao leo ameazimwa toka stesheni nyingine maana katulia sana imenivutia tofauti na siku zingine zote huwa nikisikia "makinika nami" mara "swadataa" naboreka naamua kuhama station. Usomaji wa leo ndiyo ungekuwa wa siku zote wengi tungesikiliza
 
'makinika nami' 'swadaktaaaa' mwisho atasema 'nen'geneka nami wakuu markslups na Elungata ha ha ha.
 
Last edited by a moderator:
Hapa nimeona umuhimu wa Jamiiforum. Inazidi hata magazeti,radio na televisioni katika kuibua madudu na kurekebisha jamii.
 
Ni katika kipindi chao cha magazetini asubuhi. Kuliwahi wekwa uzi humu kwamba kipindi chao cha kupitia magazeti asubuhi kimejaa matangazo ya biashara na habari za magazeti zinasomwa kiduchu tu. Kipindi kilikua na matangazo kumi kabla,matangazo kumi katikati na matangazo kumi mwishoni!.Watu wengi wiiponda kwa mpangilio huo.
Kwa karibu wiki sasa nimekua nasikiliza kipindi hicho na kwa sasa wanaweka matangazo mawili mwanzo,mawili kati na mawili mwishoni!. Tena leo ndio ilikua poa zaidi,waliweka tangazo moja tu mwanzoni,mawili katikati na kama matatu mwishoni. Taasisi nyingine zijifunze kwa hawa katika kushughurikia malalamiko ya wananchi. Kudos.

Kwa sasa wako poa sana.
 
Kwa msomaji wa magazeti ya leo ameitendea haki taaluma yake
 
Mzee wa makinika yuko vizuri,inaonekana wewe uliyeleta uzi ni mtumishi wa hicho kituo na mnapigana majungu nyinyi wenyewe, swadakta,makinika ni utambulisho wa huyo gwiji wa habari,TOM CHILALA, toka radio tumaini jamaa anakimbiza kwenda mbele
 
Hii radio inasikilizwa sn mikoani kwa hapa Dar mm sijawahi ona mtu ametega station hii ht mara1, ila ni station kubwa na nzuri ingawa hawaendi na wakati...inawezekana ni kwa vile wapo mbali na Dar mambo mengi yanawapita
 
RFA inafundisha kuliko kupotosha kama redio za hapa Dar, tatizo frequency walizopewa ziko mbali na redio nyingi hazifiki 98.9
 
Kwa msomaji wa magazeti ya leo ameitendea haki taaluma yake


Katiririka bila kigugumizi, bila sauti mkwaruzo mpaka nikahisi wametumia software badala ya mtu maana sikusikia hata utambulisho wake, amenikumbusha mtangazaji mmoja wa RTD alikuwa anaitwa Christine Chakunegela
 
Tom Chilala huwa ananiudhi! Mzee wa "ndugu msikilizaji popote pale ulipo"...
 
Jamani huyo mtangazaji ni nani ili na mimi nianze tena kuisikiliza hii redio! manake radio maarufu za hapa Dar zimezidi mizinguo, yaani wanatuchagulia habari za kutusomea utafikiri wameandika wao manina zao claus.
 
Mzee wa makinika yuko vizuri,inaonekana wewe uliyeleta uzi ni mtumishi wa hicho kituo na mnapigana majungu nyinyi wenyewe, swadakta,makinika ni utambulisho wa huyo gwiji wa habari,TOM CHILALA, toka radio tumaini jamaa anakimbiza kwenda mbele

Kati ya watangazaji makini naye huyu unamuweka? Bora hata mimi naweza kutangaza vizuri lakini sio huyo....
 
Reporters wa mikoani wa RFA wamechika sana. Wanarudiarudia maneno, habari haina mtiririko na wanauhaba wa misamiati ya kiswahili.

Fuateni nyayo za kina Benjamin rwegasira na mbazigwa hasani
 
hao mambo yao ya kizeezee kama redio one,hawatak kubadilika.ndio maana hapa town humkuti mtu akiwasikiliza,hata mikoani sikuiz haisikilizwi sana maana cloudz wameanza kufika mikoa mingi.so wasikilizaji wao hasa ni vijijini na sehem ambazo cloudz haifiki
 
Nikimsikia Tom Chilala na station nabadilisha! Jamaa lazima aanze na gazeti la uhuru
 
Back
Top Bottom