Taarifa inasema"local people". Haizungumzii watu weusi! Maana yake ni kuwa mmatumbi asiyekuwa local ataruhusiwa. Taarifa imekuzwa pasipo sababu.
Naamini njia nzuri ya kukomesha tabia kama hii ni kuzisusia sehemu hizo wala si kulazimisha kuingia.
Fundi Mchundo, heshima mbele kama jana, na leo, na kesho, na siku zote.
Mtu anapokubagua usiingie sehemu halafu wewe ukamsusia ni kwamba umemnyima kunde. That is the point of segregation, hakutaki uende pale. Ukisusa unampunguzia mashuzi.
Umesema huu sii ubaguzi wa rangi. Ni kweli. Ni ubaguzi wa wazawa. Difference without distinction. Samahani kwa kuchanganya ubaguzi wa wazawa na ubaguzi wa rangi. Ila si vema unapojaribu kusema tuelekeze macho yetu kwenye chanzo cha ubaguzi huu, kwamba tunawaibia wazungu kamera zao. Hiyo ni kutaka kuhalalisha, kusafisha, ubaguzi kwa sababu eti mbaguzi anayo sababu. Na ni kuvunja sheria za nchi. Huwezi kutuambia kwamba tuache kuwaibia wazungu kamera ndio watukubalie kuingia kwenye hoteli zao, wasitubague.
Utapopinga, unapopigania haki na kuheshimiwa kwa Wahindi humu ndani, basi pigania, pinga, linda haki na heshima za wazawa pia kwa nguvu ile ile.
Hata mimi ninaweza kukupa sababu lukuki hapa za kufanya niwachukie wahindi, ambao kiukweli kabisa ndani ya moyo wangu nina wa-maindi ila najitahidi kujizuia, kuwapenda. Nimewajua Wahindi tuko utotoni kama ni watu ambao walikuwa hawakanyagi upande wa pili wa reli ninakoishi mimi, wanajitenga kwenye viota Upanga na Kisutu, akikuajiri kwenye duka lake utakuwa mpagazi tu, huwezi kupanda ukawa meneja, hawana uchungu na utajiri wa nchi wanauhamisha nje, wana pasi za nchi tatu tatu, duka la mhindi akikuuzia the wrong item usithubutu kurudisha dukani. Kijamii, sio rahisi kuoa na kuolewa na mhindi, mpaka watu wanaanzisha thread hapa kutaka msaada wa jinsi ya kuona na mhindi. Udhia mtupu. Lakini pamoja na yooote hayo, unatufundisha, wewe Fundi Mchundo karibia peke yako, unatuasa humu ndani kila kukicha tusibague, tusichukie Wahindi, tusisingizie Wahindi kwa umaskini wetu. Na tunakusikiliza, tunajifunza kwako.
Leo unatamka kwamba yule mteja mzawa angekuwa ni "mmatumbi asiyekuwa local" angekubaliwa kuingia pale hotelini? Wale walinzi getini walijuaje kwamba jamaa sio "mmatumbi asiyekuwa local," waliomba ID inayoonyesha kabila na local address au walimuona tu sio mzungu, wakajua ni "local," mzawa? Wakabagua mzawa. Leo unatamka kwamba habari ya ubaguzi wa wazawa "imekuzwa"? Waziri kasafiri kwenda kupigana na ubaguzi ana kwa ana mpaka wenye hoteli wamekiri wewe Fundi Mchundo unasema hadithi "imekuzwa"?
Ninapinga kwa ukomo wa masikitiko ulivyokataa kulaani ubaguzi wa Wazawa nchi mwetu wenyewe kinyume na sheria za nchi, kinyume na kila aina ya maadili ya jamii zilizostaarabika.