R.I.P Neema

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
6,565
8,427
Mwaka 2008 nikiwa Taxi driver mzoefu katika jiji la Mwanza nakumbuka ilikua mishale ya saa 4 hivi za asubuhi nikiwa nimepark taxi car yangu aina ya Corolla 100 maeneo ya pamba hostel ambayo leo hii ni chuo cha wasimamizi wa fedha CBE, nikiwa nimekaa kwenye gari aliniijia mdada mmoja akiwa analia sana na kushika tumbo lake huku akinisihi nimkimbize hospital Agakhan maana hutibiwa hapo lakini akaniomba nimsaidie tu maana hana pesa hata kidogo.

Kwa kuwa alikua analia kwa maumivu ya tumbo nikafanya hima kumsaidia akapanda japo kiroho kilitaka kuniuma maana sikuwa nimerusha trip hata moja toka nimefika kijiweni. Lakini baadae roho ya kutoa msaada ilinijia nikajikaza na nikakimbiza gari haraka mpaka pale Agakhan Hospital.

Baada ya kufika hapo niligundua hajiwezi hata kidogo na nikafanya hima nikajitahidi kumbeba na nilipopanda vile vingazi kuna wauguzi wawili waliniona na wakaja mbio kunisaidia,haraka haraka wakampeleka kwenye room moja na kumuita Doctor na akafanya hima kisha wakajifungia humo ndani na mimi nikabaki koridoni kwenye benchi moja nisijue ni nini kimetokea

muuguzi mmoja aliniuliza kilichotokea na nikampa full stor kilichotokea ya kua hata mimi sijui chochote,basi wakamhudumia na kumbe yule dada alikua keshazimia kwa maumivu makali,jasho likimtoka na tumbo likimuuma sana.

Nilikaa pale wakisema wanamhudumia zaidi ya masaa mawili na kisha baadae wakaniruhusu niingie kumuona kidogo,nilimkuta akiwa amelala bado hajitambui,baada ya muda nikasema leo itakuaje nimekuja na mtu nisiyemjua na muda wa kazi unaenda sana,ntapata wapi pesa leo?

ukizingatia wakati huo nilikua bado naendesha gari la mtu ninalopeleka hesabu ya Tsh 80 elfu per week.baadae niliukabidhi mkoba wake mapokezi ukiwa na simu na vitambulisho,kitambulisho kimoja kilikua cha matibabu na kingine nikaona kumbe alikua ni mwanachuo wa SAUT.

Nikamuomba mtu wa mapokezi na yule Doctor kua akizinduka wanijulishe kupitia namba yangu ya simu kisha yule mdada nikamuachia shilingi elfu mbili anunue vocha na anipigie next time kunipa kinachoendelea kisha nikazama town kijiweni kutafuta pesa.

ilikua saa nane ile mpaka saa moja jioni sikuona call yoyote kutoka pale hospital,ilipofika saa mbili nikachapa mwendo nyumbani na kiukweli nilipata hesabu ya boss ya hiyo siku kama kawaida na posho yangu pia, nikalala na kuamka asubuhi tena kama kawaida kuelekea kazini,niliwaza kupita pale Agakhan lakini nikasema wasipopiga simu ntaenda mida ya mchana kujua lolote, saa 5 nikapata call kwa namba nisiyoijua, kwanza nikajua ni mteja lakini nilipopokea ikaongea sauti ya kike na kusema ni yule binti niliyemsaidia.."mimi naitwa Neema yule dada ulinileta hospital jana"nikasema ooh unaendeleaje?

Akadai anaendelea vyema na amepata nduguze wapo hospital ila anaomba niende ili wanione ya kuwa ndiye niliyemsaidia. Basi nikawasha ki Corolla kile nikakimbia pale hospital na kumkuta akiwa mle chumbani kalala na jamaa mmoja nilikuja kugundua ni mpenzi wake na wanachuo wenzie wawili wadada,wakanishukulu kwa msaada wangu na wakataka wanilipe pesa tsh 40 elfu ambayo sijui moyo huo ulitoka wapi niliikataa ile pesa na kusema nilimsaidia tu na wala asijali,baada shuklani hizo nikamtakia maisha mema then nikaondoka zangu.

Miezi minne baadae nilipata kazi shirika moja hapa nchini kama dreva na nikawa nikifanya kazi nje ya mji nikiwa naenda kazini J3 ya wiki na kurudi Ijumaa au Jmosi kama mapumziko ya week end.

Ghafla siku moja nikiwa kwenye kazi za field kule maporini nimejilaza kwenye kimti fulani nikisubili maboss wangu walikua wakipiga training fulani kwa wanachi nikapata simu lakini namba nisiyoijua,na nilipopokea kumbe ni yule mdada,tukasalimiana na nikafurahi sana kumsikia kua ni mzima lakini akasema mala kadhaa hua anaugua na kupona,hapa pana story ndefu kidogo maana mawasiliano yaliendelea kati yangu na yeye huku akinisihi niwe nikimuombea kwa MUNGU juu ya uzima wake maana afya yake hua inayumba kidogo.

Miezi mingine kama 6 hivi alinipigia simu akiomba nikutane nae,nikamueleza nipo vijijini kwa kazi na nikirudi mjini nitamtafuta na ndivyo nilivyofanya,week end moja nilimpigia na nikakutana nae mgahawa mmoja maalufu hapa mjini wa Pizzeria,pamoja na kulalamika kua huugua mala kadhaa lakini alikua na mwili mzuri mwenye uchangamfu mkubwa na tulikula na kunywa kisha akaniomba kwamba akimaliza chuo nijaribu kumtafutia kazi huko nilipo au kama si yeye basi mdogo wake ambaye na yeye atamaliza chuo ktk mwaka huo,nikasema MUNGU anaweza yote usijali,kisha tukaachana na akaenda zake kurudi maeneo ya chuo.

Miezi mingine zaidi ya minne japo hapo sasa tulikua na mawasiliano ya salamu kati yangu na yeye na yule mdogo wake,siku moja moja akanipigia simu akiongea kwa unyonge sana akisema kulingana na afya yake kua inamsumbua ameenda kupima vipimo vingi na vikubwa Muhimbili na amekutwa na kansa ya damu,niliumia sana sana na kumuombea kwa MUNGU ampe wepesi,

siku zikasonga kama mwezi na nusu akanipigia tena simu siku moja akisema ile kansa ilichelewa kugundulika na dawa alizokua anapewa ni kama hazimsaidii isipokua kuna dawa ameandikiwa zinatakiwa kununuliwa India na ni vidonge sita tu lakini gharama yake ni milion 4.7 hivyo anaomba mchango maana wazazi hawana uwezo wa fedha wa haraka na dawa inatakiwa upesi,

bahati nzuri nakumbuka nilikua nimeomba mkopo wa kiofisi wa mfanyakazi maana nilikua na ujenzi enzi hizo,so nilipata pesa kama siku tatu tu mbele kisha nikamchangi shilingi laki 6 tasilimu.alishukulu sana sana na nikamuombea aendelee kupata michango mingine na kweli alifanikiwa na wakamuagizia zile dawa kutoka India na kuanza kuzitumia.

Wiki mbili baadae nikapata simu ya yule mdogo wake ambae kwa sasa ni staff wa idala fulani ya serikali ktk halimashauli moja hapa Mwanza, " G..NASIKITIKA KUKUTAARIFU KUA NEEMA AMEFARIKI DUNIA" kwa kweli niliumia sana sana sana!! na mazishi yake yalifanyika wilaya moja pembeni kidogo ya jiji ambako ndiko nyumbani kwao.

Leo nimejikuta nikimkumbuka yule dada nisijue ni kwa nini imetokea hivyo lakini niliingia imani ya uchungu sana dhidi yake enzi hizo nisijue wapi,lini,anaweza tokea tena.

Mtanisamehe kwa niliowakwaza kwa story ndefu ya kweli ila nimesemea hapa ili kujifunza kwa baadhi ya watu wenye kiburi cha uzima.kuwapenda watu,kuwasaidia wenye shida,kuwashukuru waliojitoa katika maisha yako na pia kukupigania kwa hali na mali.

Good night everybody



JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
binaadamu unazani anaelewa yeye akisha kuwa mzima na pesa au cheo, Wengine wote huwaaona mbwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwengine akiwa anapokea mshahara kama M hivi. Anajiona kama ataishi milele na atataka kukutawala kwa kila kitu. Wengine wamefukuzwa kazi kwasbb ya roho mbaya walizonazo mabos wao.
YOTE KWA YOTE IPO SIKU TUTAKUFA
 
Back
Top Bottom