Quran ya wakati wa Mtume SAW

Quran ya wakati wa Mtume SAW

Tokyo40

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
2,065
Reaction score
1,926
View attachment 270372

Chuo cha Birmingham cha Uiingereza, kimetangaza kuwa wana Quran ya iliyoandikwa katika ngozi ya mnyama (parchment) ya wakati wa maisha ya Mtume SAW au miaka michache baada ya kufariki.

Kwa kutumia radiocarbon testing, wamefahamu kuwa Quran Tukufu iliandikwa katika ngozi ya mnyama aliyekuwepo wakati wa uhai wa Mtume SAW na kuandikwa aidha alipokuwa hai au muda mfupi baada ya kifo chake.

David Thomas, Profesa wa dini ya Kiislamu na Kikristo wa Chuo cha Birmingham, alisema kuwa maneno ya Quran waliyoandikwa kwenye ngozi hayana tofauti na Quran ya leo pamoja na Quran iliyo na umri sawa inayohifadhiwa na Bibliotheque Nationale de France huko Paris, Ufaransa.

Profesa huyo akaseka kuwa Quran hii itakuwa imeandikwa baina ya mwaka
AD 568 na AD 645 kwa kutumia utaalam wa "radiocarbon testing" ya Chuo Kikuu cha Oxford na ambao unatoa majibu sahihi ya umri kwa asilimia 95.

Mtume Mohamed SAW alizaliwa mwaka 570, Makka.

source: wsj.com
 
ailiyekwambia imeshushwa kama jiwe nani? imeshushwa kwa maana ya kuletwa kutoka mbinguni kuja duniani kwa njia ya Wahay (hisia/mawasiliano ndania ya mwili wa mtume) na wakati mwingine kuletwa na malaika jibril A.S .
Na pindi inaposhuka aya za Quran maswahaba za mtume ma wake zake hushuhudia na kuwekwa kwenye record mojawapo ndiyo hiyo iliyogunduliwa kuhifashiwa kichwani na kuandikwa kwenye mawe.
mungu ndiye anajua zaidi.
 
View attachment 270372

Chuo cha Birmingham cha Uiingereza, kimetangaza kuwa wana Quran ya iliyoandikwa katika ngozi ya mnyama (parchment) ya wakati wa maisha ya Mtume SAW au miaka michache baada ya kufariki.

Kwa kutumia radiocarbon testing, wamefahamu kuwa Quran Tukufu iliandikwa katika ngozi ya mnyama aliyekuwepo wakati wa uhai wa Mtume SAW na kuandikwa aidha alipokuwa hai au muda mfupi baada ya kifo chake.

David Thomas, Profesa wa dini ya Kiislamu na Kikristo wa Chuo cha Birmingham, alisema kuwa maneno ya Quran waliyoandikwa kwenye ngozi hayana tofauti na Quran ya leo pamoja na Quran iliyo na umri sawa inayohifadhiwa na Bibliotheque Nationale de France huko Paris, Ufaransa.

Profesa huyo akaseka kuwa Quran hii itakuwa imeandikwa baina ya mwaka
AD 568 na AD 645 kwa kutumia utaalam wa "radiocarbon testing" ya Chuo Kikuu cha Oxford na ambao unatoa majibu sahihi ya umri kwa asilimia 95.

Mtume Mohamed SAW alizaliwa 570, Makka.

source: wsj.com

AlhamdulillAh !
 
Ilishushwa Qur an sio Maandishi ya Qur an, hapo yanaongelewa Maandishi. Nyie ndo kizazi kinachoamini ujinga hufutwa kwa kujua kusoma na kuandika tu.

Kwan quran na maandishi ni vitu viwili tofauti?
Ok maandishi hayakushusha kama unavyodai iliyoshushwa ni koran, je hiyo iliyoshushwa iko wapi?

Na ilishushiwa wapi?kwenye nini?
 
Uzi huu si wa kutaka ligi ya udini.

Kila mwenye akili timamu anafahamu historia ya dini yake.

Lengo la uzi huu ni kuelimishana siyo kukashifu dini yoyote.

Kuna watu wanadhani wanajua sana dini.
Ngoja utawaona.
 
Kwan quran na maandishi ni vitu viwili tofauti?
Ok maandishi hayakushusha kama unavyodai iliyoshushwa ni koran, je hiyo iliyoshushwa iko wapi?

Na ilishushiwa wapi?kwenye nini?

Qur an Ilishushwa kwa njia ya Wahyi. Then ikaandikwa, ni sawa na kwny Vikao Ukioneshwa Minutes za vikao kuhusu alichosema au kuagiza kiongozi ubishe kuwa si kweli kwa huo sio Muandiko wake. Qur an Ilishushwa kupitia kwa Mtume Muhammad then akaagiza iandikwe ili iwe rahisi kufikishwa kwa watu. UISLAM unathamini sana Maandishi ndio maana tunalazimishwa kwenye Qur an kuwa Makubaliano yoyote yawe kwenye Maandishi na awepo Shahidi, Fikiria hilo agizo lipo tangu karne ya Saba kabla hata hizo sheria za kilimwengu hazijang'amua hili.
 
Mkuu aya zilishushwa na mwenyezimungu na zilihifadhiwa vichwani kabla ya kuandikwa katika hizo ngozi za wanyama na majabali n.k. hapo awali njia kuu ni kuzikariri orally
 
Qur an Ilishushwa kwa njia ya Wahyi. Then ikaandikwa, ni sawa na kwny Vikao Ukioneshwa Minutes za vikao kuhusu alichosema au kuagiza kiongozi ubishe kuwa si kweli kwa huo sio Muandiko wake. Qur an Ilishushwa kupitia kwa Mtume Muhammad then akaagiza iandikwe ili iwe rahisi kufikishwa kwa watu. UISLAM unathamini sana Maandishi ndio maana tunalazimishwa kwenye Qur an kuwa Makubaliano yoyote yawe kwenye Maandishi na awepo Shahidi, Fikiria hilo agizo lipo tangu karne ya Saba kabla hata hizo sheria za kilimwengu hazijang'amua hili.

Hapo kwenye kuweka kwenye maandishi unadanganya, hayo yalikuwepo kabala hata ya karne ya kwanza utawala wa kirumi ulitumia huo mfumo kwenye mikataba toka enzi za Plato, kwa hiyo sio Quran iliuleta, quran imeukuta upo.

Kwa nini hamsemi ilifunuliwa mnasema ilishushwa?
 
Hujaelewa japo Umesoma nilichoandika. Nimesema Waislam WAMELAZIMISHWA kuwa na Mikataba kweny Makubaliano yao.Hao Warumi hawakuwahi kuwa na Amri ya aina hiyo, hayo mengine ya kushushwa na kufunuliwa ni tofauti ya lugha kwenye kiswahili pengine tungekuwa tunafanya Mjadala kwa kichaga au kinyakyusa pengine isingekuwa hoja
 
Back
Top Bottom