Uchaguzi 2020 Queen Sendiga aahidi kujenga chumba cha kuhifadhia maiti haraka sana wilaya ya Arumeru patandi

ADC Party

Member
Sep 14, 2020
28
29
Mgombea wa Urais Kupitia chama cha ADC Mh Queen Cuthbert Sendiga leo hii ameahidi kujenga chumba Cha kuhifadhia maiti haraka sana katika hosp ya wilaya ya Arumeru (Patandi) endapo atapatiwa nafasi ya kuwa rais wa nchi hii ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya ADC yenye sera ya maboresho ya mifumo ya Afya.

Sambamba na afya, miundombinu ya barabara na soko la wafanyabiashara wa Tengeru ni changamoto kubwa sana katika wilaya hii ya Arumeru.

Mgombea Queen Sendiga ameahidi kujenga soko jipya ndani ya miezi 3 ya mwanzo atakapoingia serikalini ili wafanyabiashara wapate uhakika wa kufanya kazi vipindi vyote vya mwaka na pia kufanya matengenezo ya barabara ili ziweze kupitika katika vipindi vyote vya mwaka.

Mgombea amefanya mikutano yake ya kampeni na kuweza kunadi sera zake katika maeneo ya Legauga Stand , Magadini , Ngarasero na kumalizia Maji ya Chai.

Mgombea anaendelea na ziara kesho mkoani Arusha wilaya ya Arusha Mjini.

585277068.jpg
235621191.jpg
121616008.jpg
1584757486.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Huyu mama huwa namuelewa sana. ila aione haja ya kuunganisha nguvu ya kumuondoa jiwe. huyu alitakiwa achukue jimbo muhimu hata hapo Dar akawe waziri muhimu wa Tundu Lissu. BTW Tundu Lissu afikirie kumpa ubunge wa viti vi5 ya rais
 
Back
Top Bottom