Quality Plaza yaungua?

Ujinga mtupu, insurance nao hawana akili wanalipa tu fweza bila uchunguzi kamili. Haiingii akilini kwa nini majengo mengi yanaungua wakati huu ambao uwezo wa kuzima moto ma technologia za kisasa zipo. Wizi mtupu ngoja waingie wanaoweza kuendesha nchi muone kama upuuzi kama huu utaendelea kutokea.
 
Jamani tuwe na ushirikiano na vitu kama hivi sio jambo la busara kushangilia mambo tusiyoyajua,Nakubali umiliki usio wa halali wa Menji lakini je mmefikiri mali za watanzania wengine waliokodi na kulipa kodi zao ndani ya jengo hilo,Kodi hizo zinazoendelea kusaidia serekali kwa namna moja ama nyingine,Kuna makapuni meng tu yamekodi pale je mmefikiri kuhusu wao juu ya hili..

Tusiwe hivyo watanzania tuache ushabiki usio na maana tuangalie wapi tunahitaji kushirikiana na kujenga taifa hililo na nguvu na sio kushabikia vitu vinavyopoteza umoja wetu.Kuungua kwa jengo hili kunarudisha nyumba nchi yetu na sio busara kushabikia kwa kufanya hivyo hina maana unakubali uwepo wako wa kuwa maskini daima.
 
Jengo si la Manji tena, sehemu kubwa ni la PSPF- Shirika la serikali, na waliomo mle ndani ya jengo ni wafanyabiashara mbalimbali wazalendo wazuri tu watazania. Inasikitisha kushabikia kuungua moto kwa jengo. Ni muhimu kutofautisha umiliki kwa maana ya kuwa na haki na mali fulani na Mali yenyewe.

Mimi niko radhi tuibiwe kama tunavyoibiwa kila kukicha kwenye migodi na makampuni kama ya bia, mabenki nk, ilmradi fedha hio isitoke nje ya mipaka ya tanzania. Wewe iba lakini pesa ibaki Tz kwa maana ya kujenga majengo kama hayo ya Quality Plaza na mengine. Maana hata Manji akifa au akikimbia nchi bado tunakuwa nayo. Ndio maana nafikiri si sahihi hata kidogo kwa mlioshabikia mali kuungua! Ni mali yetu haiondesheki ile ni yetu. Atakapochukuwa nchi jemadari, atasawazisha mapato yote yatokanayo na mali (assets) kama hizi. Lakini kama watakuwa wamekimbiza huko Jersey sio rahisi!

Hivi mnajua ni Bongo tu unaweza ukaingia kwenye Bureau de Change, ukatoa Dola hata 50,000 ukauza na wala usiulizwe tena wewe ni Mtz, na ukienda na vijisenti vyko ni Bongo tu unaweza kununua any amount of dola bila kuulizwa chochote, na bila kupewakaratasi lolote! Ndio hivyo! Ndiyo maana nchi inaliwa. Tujipe pole kwa kuunguliwa mali yetu pale Nyerere Road. Tutumaini jeshi letu la uokozi wa moto limenusuru mali na maisha!

Mkuu maneno mengi ya nini?
Hili jengo ni matunda ya ufisadi uliokubuhu, jengo limenunuliwa na pesa ya wananchi kwa bei ya mara tano ya market price.
Sasa watu wakicheka ni kuwajia juu wale walionunua na kuona kama hiyo pesa itarudi?
Hata kama ililipiwa bima!!!
Ufisadi unaumbuliwa hata kabla hawajastaafu.
 
Jamani tuangalie na wenzetu walio ajiriwa ndani ya mjengo huo,inaweza isiwe likizo bali vibarua kuota nyasi,tuombe Mungu utokee wokovu eneo hilo!!
 
Mkuu maneno mengi ya nini?
Hili jengo ni matunda ya ufisadi uliokubuhu, jengo limenunuliwa na pesa ya wananchi kwa bei ya mara tano ya market price.
Sasa watu wakicheka ni kuwajia juu wale walionunua na kuona kama hiyo pesa itarudi?
Hata kama ililipiwa bima!!!
Ufisadi unaumbuliwa hata kabla hawajastaafu.

Very Low contribution...Hivi kwakuwa Voda wapo Mafisadi wa CCM, basi ikiuungua au kufilisika Tuchekelee...? au watu wakifa Migodoni tuchekelee eti tu kwakuwa viongozi wetu wamekula Rushwa?...Endelea mjenzi wa Taifa
 
inasikitisha kuona watu wanashabikia MOTO!... mambo mengine ondoeni ushabiki wa siasa au personal issues:mad2:
 
Very Low contribution...Hivi kwakuwa Voda wapo Mafisadi wa CCM, basi ikiuungua au kufilisika Tuchekelee...? au watu wakifa Migodoni tuchekelee eti tu kwakuwa viongozi wetu wamekula Rushwa?...Endelea mjenzi wa Taifa
We mwenyewe ukiungua nitachekelea:becky:
 
huyo ndio manji ana akili za ku frame vitu jinsi atakavyo, hatari tupu.
 
kama kawa magazeti yataandika kuwa magari ya fire yalifika bila kuwa na maji
misleading, pump za fire zina uwezo mkubwa sana wa kutupa maji kwa hiyo usishangae dakika tatu tu maji yameisha, then wanalaumiwa fire. katika miji kunatakiwa kuwe na fire hydrants kwa ajili ya fire fighting lakini sijaona kwa sasa hiyo kitu kwenye miji yetu. long time ago mji wa iringa ulikuwa na hii kitu ila sina hakika kama bado mfumo upo.
 
Very Low contribution...Hivi kwakuwa Voda wapo Mafisadi wa CCM, basi ikiuungua au kufilisika Tuchekelee...? au watu wakifa Migodoni tuchekelee eti tu kwakuwa viongozi wetu wamekula Rushwa?...Endelea mjenzi wa Taifa
Mkuu kama wewe ni fisadi uliyekubuhu, siku ukiungua nitakunywa Tusker bariiiiiidi!
Hatukuwa tumekuondoa kwa kupenda lakini fate will have removed you from circulation.
 
Nina wasiwasi km likiteketea kabisa basi lazima atenda tena kuchota mabilioni kwa kikwete basi naomba samahani kwa post ya hapo juu naombea lisiungue sana ili tuokoe kuibiwa pesa zaidi na huyu fisasi papa na nyangumi
 
Kwani Manji akiunguliwa na kajengo hako anaathirika kitu gani?
Kuna habari zimetangazwa na Redio one kuwa Jengo la Quality Plaza (nyerere Road) linaungua, kwa wale waloko eneo la tukio tunaomba mtuhabarishe.

Mod Naomba uihamishe hii baada ya 2 hours
 
Jamani mbona Manji alishauza hili jengo siku nyingi? Lilinunuliwa na PSPF!!! Ila wapangaji ni wazalendo wenzetu hivyo si vema kushabikia sana. Labda kama unataka kuniambia kuwa PSPF walikula njama wakalinunua kwa bei mara tano ya current value na mshiko wa ziada wakatia mifukoni then wanataka sasa walipwe na bima!!! Ha ha ha kama itakuwa kweli basi hapa ni lazima uchunguzi wa kina ufanyike, usikute ni mchezo mchafu kwa pensheni za wazalendo ati. Poleni sana wapangaji mlokumbwa na janga hili.
 
Bandugu, asubuhi hii nimeona jenge la quality plaza, ile sehemu yenye stanbic bank ikiwa imeungua. Kuna mwenye habari zaidi atujulishe?
 
Back
Top Bottom