Qualifications | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Qualifications

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Fredy James, Jun 6, 2012.

 1. F

  Fredy James Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna tofauti gani kati ya Academic qualification na Professional Qualification? Na zinafanyaje kazi kwenye nchi yetu ya Tanzania?
   
 2. M

  Mtanzania makini Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Academic qualification ni ile inayopatikana kutoka shule au chuo (inatokana na performance katika masomo ya fani husika - First class, Upper Second, ..............Pass). Professional qualifications ni ile inayotokana na utendaji wako katika fani husika. Mfano kama wewe ni engineer ni kazi gani umezifanya na kwa muda gani. Kwa upande mwingine professionalism inaangaliwa kwa jinsi chama/taasisi ya wataalamu husika (professional board) imekupa usajili i.e. Registered Engineer, Architect, Nurse, Doctor, Planner, e.t.c.

  Katika nchi yetu (na duniani kwa ujumla) academic qualification inatumika kama entry point ya ajira kutokana na mahitaji husika. mfano mwajiri anataka watu wenye Degree ya kwanza, ya pili, au ya tatu na atawachagua kuwapa kazi wale waliofaulu zaidi ya wenzao. Professional qualification inafuatia baada ya kuridhika na acedemic qualification i.e. muajiri atampa nafasi zaidi yule ambaye academically amefanya vizuri na ameifanya kazi husika kwa muda fulani (anaijua vizuri kazi yake tena kwa vitendo siyo nadharia).

  Mwajiri makini anahitaji mtu mwenye both 'good academic and professional qualifications'.
   
 3. F

  Fredy James Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ebwana kweli ww ni mtanzania makini, ahsante sana kwa jibu zuri na nimelizika nalo kabisa.

  Lakini swali lingine la nyaongeza hapohapo. Kwenye nchi yetu sasa hivi kuna watu wanokwenda kuanza moja kwa moja professional Board baaada ya kumaliza form four alafu wakimaliza hadi kupewa usajili wanaajiriwa na kupewa priority kuliko mtu aliyemaliza form six na degree, wakidai kwamba huyu aliyesajiliwa na board yupo competent zaidi yaani kimatendo kuliko wa degree(Nadharia ya darasani). Hii inakuwaje? Mkuu!
   
 4. M

  Mtanzania makini Member

  #4
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Fredy hapo sijakuelewa, hao wanaoanzia na professional board ni boards zipi hizo ambazo zinawapokea baada ya kumaliza form 4. Kwa sababu ninavyojua mimi professional boards zinatoa usajili kwanza baada ya muhusika kupata academic qualifications zinazokubalika na hiyo board (mfano uwe na Degree, Diploma, ......). Hii ya kuingia board moja kwa moja toka form four naomba nifafanulie zaidi halafu nitachangia tena.
   
 5. F

  Fredy James Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, yaani namaanisha professional board wanakuwa na Levels zao ambazo zinakuwa na link na academic professional kwahivyo watu wenye Degree kuna level ya juu wanaanza lakin wale wa form four wanaanzia level ya chini na baadae kama akifaulu anapanda taratibu ngazi moja hadi nyingine na hatimaye kumaliza mpaka level ya mwisho hadi kusajiriwa.
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mtz makini ameelezea vizuri sana, lakini labda tutumie lugha ya 'formal qualification' kumaanisha hizo academic qualifications. Mfano nimeskia kuna Board of Materials Management wanafanya hiyo kitu, lakini inahusisha formal measurement if competency. Kuna mtihani, unafaulu kwa kiwango/viwango maalum na kupata cheti. Professional qualification sio lazma iambatane na cheti. Inaweza kuwa usajili tu ama short courses ulizohudhuria kujazia kwenye huo ujuzi wako na kukufanya bora zaidi. Inaweza kuwa historia ya kazi ulizowahi kufanya. Mfano kwa ajili ya u-director wa ofisi fulani, hata kama una phd (academic qualification) ama hiyo qualification ya board, hauwi competent unless professional qualification imesimama.
   
 7. F

  Fredy James Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bwana King'ast, swali langu nilikuwa namaanisha Je ni sawa mtu kumaliza form four na kuingia board moja kwa moja na hatimaye kumaliza na kusajiriwa hadi kuajiriwa. Na hata baadaye akipata experiance ya kazi anaweza kujiunga na masters. wapo watu hapa Tanzania wanafanya hivyo MKUU
   
Loading...