Pwani: Basi la Kampuni ya Maning Nice limepata ajali ya kupinduka

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Basi la Kampuni ya MANING NICE ambalo lililokuwa linafanya safari zake kutoka Mtwara kwenda Morogoro, limepata ajali ya kupinduka maeneo ya Kisevule karibu na kiwanda cha Cement mchana wa leo, hakuna vifo vilivyoripotiwa kwa sasa. Taarifa zaidi ya ajali hiyo tutawataarifu kadri tutakavyopata kutoka kwa mamlaka husika.
IMG_20180515_182504_584.jpg
 
Hii kampuni IPO Mozambique pia,kuna miaka Fulani nilipita Mozambique nikayaona!nasikia hata kule walichinja sana watu kwa ajali za mabasi yao na kampuni yao kufungiwa kwa muda
 
Hii kampuni IPO Mozambique pia,kuna miaka Fulani nilipita Mozambique nikayaona!nasikia hata kule walichinja sana watu kwa ajali za mabasi yao na kampuni yao kufungiwa kwa muda
Lakini Tanzania hayana rekodi mbaya sana katika ajali..wamejitahidi sana maana Kusini kote wamejaa Nachingwea, Masasi, Mtwara.
 
Ajali ni popote pale unaweza kupata, lakin uende kokote ukiyakuta bus za kampuni ya CITY BOY au MINING NICE kaa Mbali, kumbuka Ajali haikimbiliki lakin mabasi yanayoendeshwa na bangi yanakimbilika
 
Ni Habari/Taarifa ya kusikitisha.

Pole nyingi ziwafikie ABIRIA waliokuwemo kwenye BASI hilo.

MOLA awafanyie wepesi na kuwalinda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom