Punyeto: Mitazamo ya Uislam na Ukristo

JumaKilumbi

JF-Expert Member
Sep 7, 2022
432
506
Na Jumaa Kilumbi,
31.10.2022

Punyeto ni nini?
ni kitendo cha kujiridhisha kingono kwa kujichua sehemu za siri.
Lakini ieleweke kuwa Punyeto ni kitendo cha kiasili kibailojia na hufanywa na watu wengi sana.

Japokuwa ukiuliza watu wengi hawasemi ukweli ila kila mtu anajua anachokifanya anapokuwa peke yake.

Kuna maneno husemwa kuwa “99% ya watu hupiga punyeto, iliyobaki wanadanganya”

Huo ni utani ila takwimu za kitafiti zinaonesha wazi kuwa zaidi ya asilimia 95% ya Wanaume hupiga punyeto au waliwahi kufanya hivyo kipindi fulani cha maisha yao.
D2E5A36A-71F7-464B-934E-74D58F3D0ECE.jpeg



Na ni 80% ya Wanawake hupiga punyeto au waliwahi fanya hivyo kipindi fulani cha maisha yao.
F9EC0F4E-FD4E-4F3B-B27A-6FBAD87D303F.jpeg


Tatizo kubwa kuhusu punyeto ni kwamba ‘it is addictive’ yani inapelekea mfanyaji kuwa mraibu wa tendo hilo.

Na hufanywa kwa mitindo mbalimbali maana wanaadamu ni wabunifu sana.

Zamani ilikuwa inadhaniwa kuwa punyeto husababisha upofu lakini imegundulika kumbe ni uzushi mtupu na hakuna ukweli wowote wa madai hayo.

Punyeto ikikolea huleta madhara mengi sana kwa mfanyaji ila hilo limeshaandikwa sana hivyo sitalijadili hapa, katika madhara hayo majuto pia huwa ni miongoni mwao.

SABABU ZA WATU KUPIGA PUNYETO
Punyeto hufanywa kwa sababu mbalimbali zikiwemo swala zima la ‘Libido/Sex drive’ au mihemko (naam tunatofautiana viwango, wengine sex drive yao iko juu sana), na sababu nyingine ni muaniko (exposure) tuliyonayo kwenye maudhui ya kingono.

Pigia mfano zile post za Malkia nyuki kule twitter, Post za Kim kardashian huko Instagram, nyimbo za Bongo Fleva huko Youtube, Story za kula tunda kimasikhara za rikiboy na story za Sexual Fantasy za Count Capone hapa JamiiForums vyote hivi vinashambulia akili zetu ku-focus na maudhui haya.

ATHARI YA KUBWA YA PUNYETO
Katika watu niliozungumza nao kuhusu swala hili walisema huwa wanajilaumu na muda mwingine kujichukia baada ya kufanya kitendo hiko.

Sasa haya majuto ndiyo kitu kilichonisukuma kulitazama hili kwa undani kabisa maana ndiyo tatizo kubwa linalowakabili watu.

Majuto haya hupelekea kutojiamini mbele za watu, stress, kujichukia, kutilia mashaka imani zao kwa Mungu n.k

JE, PUNYETO NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU?
Ndiyo, tuangalie kwenye vitabu vitakatifu Quran na Biblia Je, Mungu kakataza Punyeto au tunajishtukia?

Tuanze na kitabu kitakatifu cha Biblia
Katika Biblia nzima hakuna mstari au aya iliyotoa katazo kuhusu punyeto.

Kwenye biblia Kitabu cha mwanzo 38: 3-10 Mungu anatueleza hadithi ya Judah na wanawe Er na Onan.

“1 Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira.

2 Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake.

3 Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri.

4 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani.

5 Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwako huko Kezibu, alipomzaa.

6 Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari.

7 Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana; na Bwana akamwua.

8 Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao.

9 Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao.

10 Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye.”


Kwahiyo Mungu akamuua Onani kwa kosa la kumwaga nje, hii ndiyo maelezo pekee kwenye biblia yanayokaribiana na suala la Punyeto.

Lakini hapa Mungu alimuua Onani kwa kosa la kutokumpatia kaka yake mrithi maana Onani alimwaga nje kusudi ili kaka yake asipate mrithi na sio Nyeto. Case closed!


Tuje kwenye Quran tukufu na hadithi sahih:


Kwenye Uislam tuna vyanzo vikuu vinne vya elimu tuna
1. Quran
2. Hadithi za mtume
3. Fatwa za Wanazuoni
4. Qias

Pia kwenye Quran suala hili halikutajwa moja kwa moja ila aya pekee iliyo karibu na maelezo kuhusu Punyeto ni ile Quran 23:5-7.

“5. Na ambao wanazilinda tupu zao,

6. Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa.

7. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.”


Pia hakuna hadithi sahih ya Mtume (SAW) inayokataza Punyeto.

Dr. Zakir Naik ambaye ni Daktari na mhubiri mashuhuri wa kiislamu anajibu uhalali au uharamu wa nyeto kama ifuatavyo.

Quran na hadithi havijaeleza kuhusu Punyeto, katika vile vyanzo vya elimu tunalazimika kufuata chanzo kinachofuata ambacho ni Fatwa za wanazuoni. Wao wanasemaje?

Hapa Wanazuoni kama ilivyo kwenye mambo mengine wamekhitilafiana (tofautiana). Tuna makundi matatu

  1. Wanaosema Punyeto ni haramu na mbaya
  2. Wanaosema Punyeto ni Muba’a (hiyari, optional)
  3. Wanaosema Punyeto ni Makrooh (yaani si haramu ila haipendezi, kama ilivyo kwa uvutaji wa sigara)

Kwakuwa hili suala ni zito ila japo kwa juu juu tuwatazame hawa wanazuoni wana hoja gani juu ya hili.


1. Wanaosema Punyeto ni haramu na mbaya

Wasomi wengi wa Madhehebu ya Imam shafi na Malik wanasema Punyeto ni haramu na wananukuu aya za Quran 23:5-7 kama nilivyozieleza hapo juu.

Kundi hili la wanazuoni Wanasema kuwa aya ipo wazi na kwamba kujiridhisha kingono (sexual satisfaction) ni halali baina ya mke na mume tu na si vinginevyo.

Kujiridhisha kingono kwa namna nyingine yeyote ni haram.

Hivyo kwao Punyeto ni kinyume na maelekezo ya aya hii.

2. Wanaosema Punyeto ni halali (Muba’a - Halali ila ni hiyari)

Katika aya hizo hizo Quran 23:5-7 kuna kundi la pili la wanazuoni, wao wanaifasiri suala la kujiridhisha kingono kuwa Mungu alimaanisha kufanya mapenzi ambapo ni baina ya watu wawili (ni tofauti na Punyeto ambapo anayehusika ni mmoja na nyeti zake tu) ni halali kwa mume na mke tu ila hakusema kuhusu kujiridhisha mwenyewe (yaani Punyeto) ambapo hauhitaji mtu wa pili.

Kwahiyo wanazuoni hawa wanadai kuwa Punyeto haijakatazwa kilichokatazwa kwenye aya hizo ni kufanya mapenzi na mtu asiye mume au mke wa mhusika tu na haihusiani na kujiridhisha mwenyewe.

Na sababu yao ni kuwa katika Quran na hadith hakuna mahali suala hili limekatazwa na kwakuwa halijakatazwa basi halali na ni muba’a kwa maana ni hiyari kwa mtu mwenyewe.

3. Wanaosema ni makrooh (ni halali la haipendezi)

Kundi hili tunawakuta wanafunzi wa Ibn Abbas ambao wao kwa maoni yao walieleza kuwa Punyeto ni halali ila haipendezi kuwa sifa ya watu wema.

Na kundi hili hutilia uzito suala la punyeto katika mazingira fulani maalum.

Mathalan mtu kapandwa hamu ya kushiriki tendo hapo anakuwa na chaguzi (options) mbili;

  1. Atafute mtu azini nae
  2. Afanye nyeto hamu imuishe
Wanazuoni hawa wanasema kuliko mtu azini ni bora afanye Punyeto.

Katika hali hii wanazuoni hawa wanasema kuwa

Ndoa ni bora kuliko Nyeto,

Nyeto ni bora kuliko zinaa,


Zinaa ni mama wa madhambi.

UHARAMU WA PUNYETO


Dr. Zakir Naik ameeleza kuwa Punyeto inakuwa haramu bila shaka pale inaposindikizwa na kutazama picha au video chafu za utupu.

JINSI YA KUACHA PUNYETO
Njia hutajwa kwa wingi sana ila hapa nitaeleza mbili.

Dr. Zakir Naik amependekeza njia mbili kuepukana na Punyeto.
  1. Ndoa
Mhusika aingie ndoani ili badala ya kupiga Punyeto kujiridhisha ajiridhishe kwa mwenza wake.
2. Kufunga swaum
Swaum inafahamika kwa kupunguza hamu ya kufanya Mapenzi, kama mtu anashikwa sana na hamu ya kufanya tendo basi afunge kupunguza.


MAONI YANGU

Maoni yangu binafsi ni kwamba nakubaliana na Dr. Zakir Naik kuwa Punyeto ni Makrooh, yaani ni halali ila haipendezi.

Kuhusu madhara ukweli usemwe kuwa “an excess of anything is harmful” (Chochote kikizidi huwa na madhara)
Soda ni tamu ila ukinywa sana kisukari kitakushika.
‘Fast food’ tunazipenda lakini tukila sana Presha na kuzidi uzito kutatushika.

Kila unapogusa kuna uzuri na ubaya, na ubaya huwepo pale tu tunapozidisha.

Ukifanya Punyeto kama mara 5-10 kwa siku bila shaka utapata athari mbaya kabisa.

Ushauri wangu kuhusu kila kitu maishani ni “Fanya kistaarabu”
 
Hiyo habari ya kibopa aliyepiga mpira nje ya lango nilikuwa nautafuta kwa kipindi kirefu ipo kwenye kitabu gani cha biblia bila majibu, finally nimejua
Nazihurumia sababu kwa vile huna wa kukuzuia🤣🤣🤣
 
Nashukuru mkuu ila uje na nukuu ya andiko mkuu

Hiyo itasaidia kuleta mjadala unaojenga.
Waache uvivu wakasome Biblia:
Biblia inasema wafiraji na wazinzi hawatauona ufalme wa mbinguni. .

Soma: 1 Wakorinto 6:9
Msidanganyike waasherati hawatourithi ufalme wa Mungu, Wala waabudi sanamu, Wala wazinzi, Wala wafiraji, Wala walawiti, Wala watamanio, Wala wevi, Wala walevi, Wala watukanaji, Wala wanyang'anyi.

1. Waasherati - Hawa ndio wale wapiga nyeto, wawaza sex, wasagaji, wanaoshiriki tendo nje ya ndoa etc
2. Waabudu sanamu - Hawa ndio wale watumiao sex toys na kusema oh my god.
3. Wazinzi - Hawa wanandoa wanaofanya nyeto, mapenzi nje ya ndoa, orgy, threesome. ..
4. Wafiraji - Hawa Wala Tigo, kikunyeo, nyonya puru...
5. Walawiti - Hawa wasagaji, mashoga, wapenda puru.
6. Wevi - wapiga chabo, kuiba wake za watu, kutamani, sex plays ...
7. Watamanio - wapiga chabo, kuota wake waume za watu, sex toys, penda penda
8. Walevi - Hawa wanaongoza kwa ngono zembe
9. Watukanaji- Hawa wanafanya dirt sex like I wanna https://jamii.app/JFUserGuide you infront of your mommy
10. Wanyang'anyi - Hawa wabakaji washenzi wakubwa nao watabakwa motoni, mfano demu kala Hela zako unapanga kumkomoa unahusika. .


Nakunywa juice hapa nikimaliza nitautupia dhambi nyingine wapendwa wa Mungu wazitambue. .
 
Hivi Ni Nani huyo aliyegundua huu mchezo wa punyeto maana jamaa alizua balaa Kweli Kweli,dah!
Cha ajabu mie sikufundishwa nilikuwa naoga nikiwa darasa la Tano. Niliona Raha mpaka nikaka kwenye ndoo chooni, niliendelea na huu mchezo kwa miaka kumi.

Mungu ni Mwema nilikuja kuacha na madhara makubwa nyeto mbaya sana. Penis ilikuwa kama ukuni kwanza niliacha kwa ushauri wa daktari. .

Wapendwa katika Mungu soma : Warumi 1:26-27
 
Na Jumaa Kilumbi,
31.10.2022

Punyeto ni nini?
ni kitendo cha kujiridhisha kingono kwa kujichua sehemu za siri.
Lakini ieleweke kuwa Punyeto ni kitendo cha kiasili kibailojia na hufanywa na watu wengi sana.
Kuna kitu kinaitwa Jamuhuril ghulamaa [msimamonwenye nguvu kulingana na dalili]....

Punyeto ni haramu.... kutokana na dalili ulizozitaja....

Na Mtume amewataka vijana waoe au wafunge....

Jamani mtatufanya our night to be much more longer kwa kuwa na wenza walioathirika na punyeto...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom