Punguza hasira Temu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Punguza hasira Temu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Annina, Jan 24, 2010.

 1. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Temu, najua umeudhika na unanilaumu, una haki ya kufanya hivyo. Ndio maana nasisitiza niangaliwe kwa jicho la huruma na unipe upendeleo maalum katika kulimaliza hili. Temu, wewe wajua, mimi najua na wengi wanajua kwamba Annina bila ya wewe maisha hayana thamani. Temu, sijasahau hata kidogo uliponiomba niwe mwenzi wako katika maisha kwa kuwa unaamini bila Annina maisha yako hayajakamilika -sijasahau! Temu siku zote nimekuwa msikivu kwako, tumekuwa tukiishi kwa amani na upendo mkubwa huku tukiwa wavumilivu na wenye subira hasa penye majaribu tukitaraji maisha mema baadae - bado naamini hivyo!

  Temu, najua una hasira za mlipuko - waswahili wanasema ndio maumbile yako, nakuhurumia sababu najua unavyoteseka unapokuwa kwenye hali hiyo. Nakuhurumia zaidi sababu nakupenda sana na nisingependa kuona moyo wako ukiwa umetawaliwa na hasira, simanzi na huzuni. Naumia zaidi pale ninapokuwa chanzo cha wewe kuwa kwenye hali hiyo - uniwie radhi.

  Temu wangu, ni nini kimekufanya ufikiri mimi Annina ninatumia muda wangu mwingi na JF kuliko ninavyotumia na wewe? Kwamba ninawathamini wachangiaji mbalimbali wa JF nisiowafahamu hata kwa sura kuliko ninavyokuthamini wewe? Temu mpenzi, angalia basi hata idadi ya posti nilizonazo JF labda utagundua kitu tofauti na unachoamini sasa.

  Temu mpenzi, tafadhali punguza hasira tujadili hili na tulimalize ili tuboreshe zaidi na zaidi mapenzi yetu. Tumeshapoteza muda mwingi sana kukabiliana na vikwazo na changamoto mbalimbali za maisha, naamini tuna kila sababu ya kufurahia maisha yetu sasa - baada ya dhiki faraja...


  Nakupenda kabisa!
  Annina
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  wtf
   
 3. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Amekusoma nadhani
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  ni yule jamaa uliyekuwa una wivu nae wa kupindukia? nashauri pia MODS waiondoe hii mada kwani inashusha hadhi ya mleta mada
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Annina,

  Hii barua inaonyesha jinsi unavyoithamini JF kuliko unavyomthamini Temu, kama kweli hii barua ni ya Temu, kwa nini umeipost JF?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,904
  Trophy Points: 280
  Annina pole sana kwa yanayokusibu kuhusiana na penzi lako, lakini mimi nakushauri haya mambo inabidi yajadiliwe katika faragha badala ya kuyaweka katika kadamnasi kubwa kiasi hiki na kuwapa faida hata wale wasiohusika katika mapenzi yenu wewe na Temu. Kila la heri.

  Have a great Weekend
   
 7. Twande

  Twande JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Imekuaje tena Annina?? Seems na yeye ana wivu hata mate hayapiti!! Hahahaaa sasa mtoto atatoka na wivu mpk pumzi haiendi mfumo wake wa kawaida...anyways u guys must b in deep luv..
   
 8. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Na Temu ni mwana JF?
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huyu naye!
  Ushamba gani huo? Kwani lazima utangaze hadi jina la mpenzio? Au una agenda ya siri zaidi ya kulalama?
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Annina;

  Ninaamini hii ni hekaya na temu ni wa kusadikika... unfortunately wanajamii wameona kama umeenda over the board!!! hebu clarify basi
   
 11. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  JF ina mambo kweli sio mchezo!!
   
 12. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ......Anina kulikoni tena? Mpenzi wako yupo hapa JF?
  Mie naona wala haijakaa sawa hii, mngemalizia wenyewe chumbani kwenu.
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  POLE SANA MAM'II!
  pamoja
   
 14. E

  Edo JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nadhani anajaribu kuonyesha yanayoweza kujiri kwa wana JF. Nakubaliana na waliotangulia kusema kuwa hii ni "story tu"-si jambo la kweli.
   
 15. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  msg sent....mmmmmh
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahaha jamani mapenzi yanachanganya
  mapenzi sio mchezo kusema weka sebene ucheze
  pole Annina
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  FL,
  naomba unipigie....
   
 18. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #18
  Jan 25, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Huyu ni mtunzi mzuri kweli amefanikiwa kufikisha ujumbe wake alotaka kuufikisha- ameathirika na JF lol  Kula buku Annina
   
 19. M

  Msindima JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mmhh jamani hii ni kweli au? Nini lengo la mleta mada?
   
 20. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Annina wewe,
  Ningekuwa mimi ndio huyo Temu, hakyanani, ingekula kwako. Ni kama vile jamaa anakugombeza kakuona na kadume flani kanakutomasa, halafu unaenda kulalamika kwa hako hako katuhumiwa!
   
Loading...