Nisaidieni kuziondoa hasira za mdogo wangu/dada yangu...

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
5,767
12,982
INTRODUCTION
Ni mdogo angu (family friend).
Kwao ni wa mwisho kuzaliwa (last born).
Ana miaka 26 na ana mtoto mmoja wa kike.
Yeye na huyo baba mtoto waliachana ila mtoto anatunzwa fresh.

SCENARIO

Huyu binti Wana JF ana hasira sana. Na hapo mwanzo nilishawahi kumuhoji akasema ""Muda mwengine zinapanda mpaka kwa wateja kazini kwake"" Na kibaya zaidi mpaka mimi mshauri wake pia siku hizi ananipandishia hasira..!!

Ni mdogo angu nampenda sana na huwa napenda sana anavyo "faiti" na maisha. Yaani kwenye kutafuta pesa, aisee anajua balaa ila tatizo lake ni HASIRA SANA.

Huwezi amini, hapo mwanzo Mimi ndio nilikua mshauri wake, na kumuonya sana juu ya hasira ila siku hizi "Nikiwa namshauri jambo unakuta hata kwangu hasira zake zinapanda na kunijibu "shit"

Mfano; Kuna siku aligombana na baba mtoto wake na akamtukana huyo mwanaume kuwa ni "Mkund__ na ukoo wake ni ukoo wa mashoga, hivyo anajutaa kuzaa na mashoga..!!". Siku hiyo alimtukana sanaa baba mtoto wake kwenye simu.

Hiyo kesi ikanifikia, Mimi kama kaka ikabidi nimkalishe. Ile kumkalisha nikamwambia ""dada hivi unajua kuwa hasira zinahusishwa na tatizo la akili"" Weee kusema hili neno ""Tatizo la akili ilikuwa nongwa"" aisee kila ukimshauri jambo anajibu shit na kusema ""Mi si nina tatizo la akili""

Kuna siku alipata shida ya ugonjwa akasaidiwa kupelekwa hospitali na mama mmoja ambae siku moja walishachambana kwa hasira zake. Nikaona hapo nichukulie point ya ushauri, niliongea nae ""Ukiwafanyia hasira watu wote, je atakaye kusaidia ni nani kwenye shida zako?""

Unajua alichojibu ""Huyu alinisaidia kwasababu kuna siku alinigongea mlango usiku nikamsaidia, hivyo lazima na Mimi angenisaidie""

Aliongea na mengine mengiii... Ila kifupi ni hasira zake tu. Mi nilijua "scenario" hii ingemfanya abadilike ila hasira zake zikamtawala na kujiona yupo sawa. Ukiwa unaongea nae halafu mada ikamlenga sanaa utaona tu hasira zimepanda na anaanza kujibu shit. Kifupi huyu binti ana hasira balaaa.

THE BIG PROBLEM
Na kengine huyu dada angu amepata mchumba mwengine na kaenda mpaka kujitambulisha kwao.

Jamaa kashapewa mambo yotee ya mahari, kwahiyo familia inasubiri majibu yake kuhusu mahari.
Ila huyo mwanaume naona ka "stack" kuendelea na process za ndoa.

Baada ya kumuhoji huyu Shemeji yangu anasema..... "Amechoshwa na hasira za huyu dada".

Yaani jamaa alikubali kuoa mwanamke mwenye mtoto ila hasira za mwanamke zimemfanya asimamishe kwanza mipango ya ndoa.

Huyu jamaa aliniambiaga...
1. Dada ako ni mwaminifu sanaa, sijawahi hisi lolotee juu ya kuchepuka, na sijawahi fumania lolotee juu ya uchepukagi.
Yaani kwenye uaminifu sina "dauti nae"

2. Dada Ako ni mpambanaji sanaa, ukimpa laki 2 anaizungusha kesho analeta laki 3. Hivyo kwenye mambo ya finance ana kichwa kizuri sanaaa.

3. Kwenye maisha ya pesa kweli nimepata ""Mwanamke faita"" ila tatizo ni hasira zake.
Jamaa anasema hawezi kuoa mwanamke mwenye hasira hivi, na Mimi nikiongea na dada yeye haoni kama hasira zake ni changamoto japo Kuna siku moja tu alishawahi kukiri kuwa ""Ana hasira sanaa na hajui kwanini!""

Na hili la hasira mpaka Kwa mchumba ake nimenyamaza kimya, naogopa siku nikisema kwao huyu dada anaweza nimeza kwa hasira zake.

PROBLEM

Siku hizi anavyonijibu "shit" nikiwa namshauri, basi hata Mimi nafikiria kuachana nae ila sasa Wana JF huyu dada wazazi wake walinilea.

Wazazi wake walichangia pakubwa malezi yangu baada ya Mimi kupoteza wazazi.

Kwahiyo huwa nampenda dada angu kwasababu tumekuwa wote na wazazi wake "in another side" ni kama wazazi wangu pia, ila changamoto inayoniweka mbali ni hasira zake tu, Tena ni hasira hasaa ndugu zangu.

HEBU WAJUZI NIPENI MBINU ZA KUMSAIDIA HUYU DADA ANGU?

Najua humu naweza kupata ushauri wa wataalamu au hata mtu ambaye na yeye alikuwa na hasira akafanikiwa kuzishinda.

Tiba ya huyu dada angu ni nini?

Natanguliza shukrani.

#YNWA
 
Mtaftie mtu kwanza amkaze vizuri tatizo likiendelea ndo tujue
Ushauri sahihi. inawezekana huyu aliyemzalisha alikuwa kama anambaka tu. maskini dada wa watu hajui romance ni nini na hajawahi kufika kileleni. Akiona wanaume anaona wote ni wabakaji tu na anawaonea wivu wanawake wenzake kwa kutamani maisha yao
 
Hii issue imekaa psychological zaidi ni kutafuta wataalamu lakini pia wakati mwingine ongea nae kistaarabu sana (najua unafanya hivyo ila ongeza zaidi ya hapo) pia wajue watu wake w a karibu sana mfano marafiki zake !! Na hii issue kwenye ndoa ni changamoto sana hata kama binti atakua smart kiasi gani kwa mwanaume ni changamoto !!

Ambaye ni mke wangu kwa sasa toka tuko level za Girlfriend na Boyfriend mpaka kwenye uchumba hadi kuoana alikua na shida za design hiyo yaan kitu kidogo tu anabadilika , akiplan kitu kikienda ndivyo sivyo anachukia hatari ! Mpaka nikawa najishtukia aseee anaweza hata kuwa anaandaa chakula lakini kikitoka ambavyo hakutaka hata kama mimi nimekikubali aseee yeye anakua ameshatoka kwenye mstari !! Yan mood yake inaswitch kwa vitu vidogo sana hata ambavyo havina maana !

Labda mnatoka out nguo aliyopanga kuvaa haikumpendeza kama alivyotegemea asee mood inachange hata kama solution itapatikana mambo yakae sawa ila kwake siku ishaharibika !!

Upendo anao heshima anayo ni mpambanaji sana tu tatizo lilikua hilo !
Mimi nilichokua nafanya akitoka kwenye mood namwacha naenjoy kivyangu naendelea na mambo mengine lakini kukaa kuulizana niliacha kwa hiyo akijitoa kwenye mstari na mimi najua kisababishi natulia tu atakaa mwenyewe atajirudi baada ya masaa kadhaa !

Niliongea na rafiki yake pia akaeleza kwamba ana hali hiyo !! Kwa sasa anaendelea vizuri hali inapungua sana !
Hata ikimtokea mimi nakaa pembeni nacheka kwanza akitulia tunaelekezana basi !

Kadri tunavyoenda anakua vizuri zaidi lakini pia alikiri ana hali hiyo hivyo ikawa rahisi kumsaidia !
Kwa hiyo Shemeji yetu kama anamkubali dada ajifunze kwanza kummudu na dada aeleze na akubali udhaifu wake !!

Watu tunaowapenda ni rahisi zaidi kutubadilisha tabia na kutusaidia !

Na Maombi msisahau na waepuke kukerana .
 
ushauri sahihi. inawezekana huyu aliyemzalisha alikuwa kama anambaka tu. maskini dada wa watu hajui romance ni nini na hajawahi kufika kileleni. Akiona wanaume anaona wote ni wabakaji tu na anawaonea wivu wanawake wenzake kwa kutamani maisha yao
Kweli kabisa genye ni mbaya sana
 
Wanasema love can cure all things,mi naamini mwanamke akipendwa vizuri akili yake inakaa vizuri na anapona magonjwa yote,muunyoshe upendo na kumsikiliza na kumheshimu kama ndugu yako utaweza kumsaidia ila mpenzi wake anaweza kumsaidia vizuri maana anaweza ongea nae kupitia sex
 
Kila tatizo huwa lina source yake, kwa hasira mara nyingi huwa ni mtu wa ndani aliyeumizwa tangu akiwa mtoto.Na kama hajawahi kuyaongelea ndiyo haswa inakuwa ni worse.Kama rafiki muulize ni lipi lilimuumiza akiwa kinda,aseme tena na tena kuwa hiyo past experience haitam-winda milele, ajisamehe, asemehe.
 
Umenena jambo. Dada yako ana tatizo kubwa huenda la utotoni halijashughulikiwa. Kitu cha kwanza inabidi akubali na aone ana tatizo. Kitu cha pili, baada ya kukubali ana tatizo, inabidi awe tayari kulishughulikia hili tatizo. Hapo ndipo wanakuja wataalaam kama "social workers, psychologist, psychiatrist, na counselors". Huyu dada yako ana "mental health issue".

Mara nyingi watu wenye tatizo kama hili, yeye ukimwambia ana tatizo la afya ya akili anakimbilia ukichaa, kumbe binadamu wote tunasongwa na mental health issues. Ni pale tu tunapokuwa "overwhelmed" mental health issue inweza ikawa "full blown mental health crisis".

Ukweli ni kuwa huyu anahitaji huduma ya hao niliyowataja hapo juu. Hii itamsadia kuona kuwa kuna wakati mwingine maamuzi yake na mtazamo wake unakuwa "beyond proportion". Mwisho jitahidi kumsaidia na usikate tamaa kuna siku atauona ukweli, na atakushukuru.
 
Huyo ana stress zake za huko nyuma, mkumbushe tuu anayofanya yana madhara makubwa na mabaya kwa wengine especially kwa wanao mpenda, na akiendelea kitu pekee atakachopata ni wote watachoka na watamkimbia, chaguo ni lake
 
Samaki mkunje angali mbichi, hivyo huyo mwanamke hawezi kubadilika angali amekuwa mtu mzima...

Hasira kali ni tabia ambayo ina vyanzo tofauti tofauti, huweza kuwa ni sababu za kiroho au kimwili...

Soma threads hizi kadhaa zilizowahi kuwekwa hapa jamvini...

Thread 'Sababu za hasira na msongo wa mawazo' Sababu za hasira na msongo wa mawazo

Nini chanzo na athari za hasira? | JamiiForums Nini chanzo na athari za hasira?
 
Hii issue imekaa psychological zaidi ni kutafuta wataalamu lakini pia wakati mwingine ongea nae kistaarabu sana (najua unafanya hivyo ila ongeza zaidi ya hapo) pia wajue watu wake w a karibu sana mfano marafiki zake !! Na hii issue kwenye ndoa ni changamoto sana hata kama binti atakua smart kiasi gani kwa mwanaume ni changamoto !!

Ambaye ni mke wangu kwa sasa toka tuko level za Girlfriend na Boyfriend mpaka kwenye uchumba hadi kuoana alikua na shida za design hiyo yaan kitu kidogo tu anabadilika , akiplan kitu kikienda ndivyo sivyo anachukia hatari ! Mpaka nikawa najishtukia aseee anaweza hata kuwa anaandaa chakula lakini kikitoka ambavyo hakutaka hata kama mimi nimekikubali aseee yeye anakua ameshatoka kwenye mstari !! Yan mood yake inaswitch kwa vitu vidogo sana hata ambavyo havina maana !

Labda mnatoka out nguo aliyopanga kuvaa haikumpendeza kama alivyotegemea asee mood inachange hata kama solution itapatikana mambo yakae sawa ila kwake siku ishaharibika !!

Upendo anao heshima anayo ni mpambanaji sana tu tatizo lilikua hilo !
Mimi nilichokua nafanya akitoka kwenye mood namwacha naenjoy kivyangu naendelea na mambo mengine lakini kukaa kuulizana niliacha kwa hiyo akijitoa kwenye mstari na mimi najua kisababishi natulia tu atakaa mwenyewe atajirudi baada ya masaa kadhaa !

Niliongea na rafiki yake pia akaeleza kwamba ana hali hiyo !! Kwa sasa anaendelea vizuri hali inapungua sana !
Hata ikimtokea mimi nakaa pembeni nacheka kwanza akitulia tunaelekezana basi !

Kadri tunavyoenda anakua vizuri zaidi lakini pia alikiri ana hali hiyo hivyo ikawa rahisi kumsaidia !
Kwa hiyo Shemeji yetu kama anamkubali dada ajifunze kwanza kummudu na dada aeleze na akubali udhaifu wake !!

Watu tunaowapenda ni rahisi zaidi kutubadilisha tabia na kutusaidia !

Na Maombi msisahau na waepuke kukerana .
Upande wangu nilishindwa ku'survive
Hata tuliachana mara ya kwanza sababu ilikuwa ya kawaida sana
Baaye tulirudiana
Makasiriko na vitu vidogovidogo tena tukavunja mkataba & sasa nimefanya usajili mpya
Uvumilivu wako ndokitu nilikosa sababu alikuwa akivimba mimi na lazimisha kutafuta amani ikawa na kuta nazidi kukereka sababu muda mwingine unakuta sababu ya ugomvi ni yeye
 
Back
Top Bottom