Mwanaume, mwache mwanamke aondoke (Men, Let her go)

The Best Of All Time

JF-Expert Member
Aug 30, 2022
2,968
6,839
Naona nyuzi nyingi sana na pia hata huku mtaani, mwanamke anapomuacha mpenzi wake wa kiume, inamuumiza mwanaume kiasi kwamba wanaume hao wanabadilika kitabia, wanawatukana, na pia wengine wanajichukulia sheria mkononi kiasi cha kutaka kumdhuru mwanamke na ikiwezekana kumuua kabisa.

Mwanamke anapokuacha ni kwamba anakuona wewe si sahihi kwake, na hivyo ataacha kukuheshimu, atatafuta mwanaume au atamkubali mwanaume ambaye kwa hisia zake anaona ni bora kuliko wewe.

Unapoona dalili zozote mwanamke anaacha kabisa kukutafuta au kukuambia wazi kuwa anataka muachane, usimbembeleze, we kubali kumuacha. Najua ugumu wa suala hili ila ni njia sahihi kuliko njia zote kwasababu mpaka hatua hiyo mwanamke anakuwa hakuheshimu tena, kumbuka kwa mwanamke inaanza heshima, mvuto na then upendo ndo kitu cha mwisho. Usitarajie mwanamke wako akutreat kama wanaume ambao ni marafiki zako wakutreat.

Ukilazimisha mahusiano yaendelee anazidi kukuona dhaifu, na kakuweza inachofuata atakufanyia usaliti wa waziwazi ili akuonyeshe kuwa hakutaki. Hapa ndo reactions kama hasira kutoka kwa mwanaume zinapoanza. If a woman pulls a plug off, you have to do it the same, don't turn back.

Cha kufanya, ikitokea jambo kama hili, mwache aende, msamehe kwa kuwa usipomsamehe italeta roho ya uchungu na kisasi ambao hasara yake itakutafuna wewe, then msahau. Kumsahau itakuwa ngumu mara ya kwanza, ila kwa msaada wa marafiki zako wa kiume unaowaamini, kushiriki ibada za kiroho na pia kujishughulisha vitakufanya mdogomdogo umsahau. Hakikisha ili umsahau chagua kusudi na ulifanye la muhimu zaidi, alafu jaribu kulirudia rudia then utafanikiwa kumsahau. Usijihusishe na mada zitakazofanya umkumbuke katika muda huu wa mpito. Jijenge, mtafute sana Mungu, utapata amani. Kwa wanaomwamini Mungu unaweza tubu dhambi ya uasherati then unasali kwa bidii kuondoa hayo maumivu, time to time utahisi ule mzigo kukuondoka.

Usichukue hatua za kijinga kama kumkaripia mwanamke, kumuumiza au kujaribu kumuua eti kisa anataka kukuacha. Hizo ni hatua za wanaume dhaifu na wasio na malengo katika maisha. Mwanaume umeumbwa na Mungu Mtakatifu kwa kusudi, tafuta hilo kusudi na ulifanyie kazi. Tengeneza future yako na ya kizazi chako cha baadaye, usipoteze muda kuwatafuta wanawake kwa moyo wako wote, kwa kuwa at the end of the day, Utakufa.

Achana na huyo mwanamke and MOVE ON.
 
Hatutaki ushauri wako, hatuachi sasa.

Tukikufa tunatoa ajira kwa watu

Askari magereza atapata kazi ya kufanya,

Manesi na madokta watapata kazi za kufanya

Viongozi wa dini watapata kazi za kufanya

Nanyi commentators mtapata mada za kuanzisha 😁😁
 
Back
Top Bottom