Pumzika kwa amani rafiki yangu A

Pumzika kwa amani rafiki yangu A

Bigdada

Member
Joined
Jun 16, 2015
Posts
35
Reaction score
34
Ingawa ni ngumu kuamini Leo ni mwaka mmoja kamili tangu ulipoondoka na kuniacha mpweke ni upweke ambao siwezi kuuelezea ingawa sikuwahi kukuona ila ulikuwa karibu yangu kama mtu tuliyejuana naye miaka mingi tulikutana hapa Jamii Forum na ukawa kaka, mshauri na msaada mkubwa kwangu.

Nitakukumbuka milele sikuamini siku nilipopiga simu yako na ilipokelewa na mdogo wako na kunijulisha kuwa umefariki sikuamini ila kadri siku zinavyoenda na upo kimya nazidi kuamini kuwa ni kweli haupo duniani niliumia na nitaendelea kuumia mpaka mwisho wa maisha yangu na sitaacha kukuombea Mungu akupe pumziko la Amani.


 
Pole sana inaonekana alikuwa anakujali sana kwa ushauri ikumbukwe kuwa ni wachache sana wa kutoa ushauri wa dhati na hekima. Mungu amuweke pema mahali alipo
 
Bigdada Life goes on..... (kila siku watuhufariki Dunia, Kila siku watu huzaliwa upya) Furahia maisha yako...!!
 
Last edited by a moderator:
Mmmmh masikini au bado yupo hai? Alikuwa anatumia id gani?
 
Bigdada pole sana. A yule alikuaga UK? Kifo chake kilikua cha gafla sana kama ndio yeye.
 
Back
Top Bottom