Pumzika kwa Amani Desmond Mpilo Tutu Simba wa Afrika

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Mwaka mmoja umepita tangu Disemba 26, 2021 Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa alipotangaza kifo cha Askofu mkuu wa zamani wa kanisa la Anglikana nchini humo Desmond Mpilo Tutu.

Askofu Desmond alifariki akiwa na umri wa miaka 90 kifo chake kinatafsiriwa kuwa pigo kwa watu wengi kutokana na kumbukumbu aliyo iacha katika harakati za kupambania uhuru wa mtu Mweusi nchini Afrika kusini.

Akiwa Askofu wa kwanza mweusi kuaminiwa kushika wadhifa huo wa juu wa kanisa Tutu alitumia nafasi yake kuhubiri umoja na kukemea ubaguzi wa rangi ambao ulikua umetamalaki nchini humo nyakati hizo.
Tutu alizaliwa Oktoba 7 1931 mjini Johnesburg katika familia ya Wazazi masikini yenye asili mchanganyiko wa Wakhosa na Waswana.
Baba yake Zachariah Molilo Tutu alitoka kwenye kabila dogo la Wakhosa.

Mnamo mwaka 1945 Tutu alijiunga na Shule ya Johnesburg Bantu High School ambapo alisoma kwa mafanikio na kupata Ufauru wa daraja la pili baada ya kuhitimu 1950.
Adhma yake ilikua kusomea masuala ya Afya ya binadamu katika kiwango cha elimu ya juu lakini kutokana na umasikini wa wazazi wake alishindwa kutimiza ndoto yake badala yake akajiunga na ualimu Kisha akapata Ufadhiri wa masomo katika chuo cha Pretoria Bantu Normal College.

Akiwa chuoni hapo katika moja ya midahalo akapata kukutana na Mwanasheria mahiri Nelson Mandela ambae baadae alikua Rais wa taifa hilo.
Kipindi hiki kilikua kipindi cha mwanga kwa Tutu kwani alipata kukutana na wanafunzi wengi wenye mawazo tofauti kutoka vyuo mbalimbali kama vile Robert Mugabe ambaye baadae alkawa rais wa Zimbabwe.

1954 Tutu alijiunga shule ya Madibane High School ambapo alifanya kazi Kama mwalimu kabla ya kuhamia shule ya Krugersdorp High School nako alifundisha Kiingereza na historia.
Akiwa shuleni hapo alikutana na Nomalizo Leah Shenxane rafiki ambae alikua rafiki wa karibu wa dada yake Gloria.

1955 mbele ya Mahakama ya Hakimu mkazi ya mji wa Krugersdorp Tutu na Leah waliona na ndoa ikafungwa rasmi kiimani kwenye kanisa Katoliki la Bikra Maria Malkia wa Malaika.
Ingawaje yeye alikua muumini wa kanisa la Anglicana alilazimika kumfuata mkewe ambae alikua ni mkatoliki.

Kutokana na ubaguzi wa rangi uliokua umetawala mifumo ya elimu nchini humo Tutu na mkewe wakaachana na Kazi ya ualimu na 1956 Tutu alijiunga na Uchungaji wa kanisa la Anglikana.

Baadae akajiunga na chuo Cha thiolojia Cha Mtakatifu Peter ambacho kilikua chini ya kanisa la Anglicana ambako alisoma na kutunukiwa Shahada ya elimu ya dini.

Katika miaka 6 ya uwepo wake chuoni hapo Tutu alisifika ka harakati zake za kupinga ubaguzi wa rangi ikiwemo tukio la Vurugu za Mauaji ya 1960 Sharpeville Massecle.
Mwezi disemba 1960 alisimikwa rasmi kuwa mchungaji wa kanisa kuu la Mtakatifu Maria kabla ya kuhamia kanisa la Mtakatifu Philipo mjini Thokoza.
Baadae mwaka 1962 Alipata Ufadhiri wa masomo nchini Uingereza katika chuo Cha King's College London na kutejea Afrika kusini 1966.

Na baadae akateuliwa kuwa Askofu mkuu kanisa la Anglicana Lethoto (1978-1985) Kisha 1986 Johnesburg na baadae Askofu Msaidizi wa Capetown.

Baada ya Mandela kuachiwa kutoka gerezani miaka 1990, Mandela na Tutu waliunda ushirikiano wa kukomesha ubaguzi wa rangi nchini humo na baada ya Nelson Mandela kushinda kiti Cha urais mwaka 1994 Tutu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa tume ya Ukweli na Maridhiano nchini humo ili kuchunguza visa na madhara ya ubaguzi wa rangi nchini humo tangu ilipoanza.

Tutu alikua muwazi Sana aliwahi kumkosoa rais mstaafu wa Afrika kusini Thabo Mbeki juu ya Mgogoro wa Palestina na Israel.
Mnamo 2010 Tutu alitangaza kujihusisha na masuala ya umma.

Miaka ya 1970 Tutu aliwahi kuzua mawazo tofauti miongoni mwa jamii ya watu wa Afrika kusini wazungu wakisema ni mtu mbaya asie badilika huku waafrika wakisema ni mtu mwema anaepigania haki zao.
Mwaka 1984 Tutu alifanikiwa kushinda tuzo ya amani ya Nobel kwa Juhudi zake za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika kusini.

Peter Mwaihola
1672063145454.jpg
 
Askofu Desmond Tutu mtu wa mbali maelfu ya maili kutoka huku nilipokua niliyelazimika kumfahamu kutokana na ushawishi wake juu ya mapigano kuelekea usawa na kuondolewa kabisa kwa ubaguzi wa rangi sio tuAfrica Kusini Bali Tutu Ni picha iliyokuwa na mafunzo mengi kwa wasio waafrika Kusini.Bila shaka Ni kichocheo kipya dhidi ya kuondoa kabisa ukabila na udini miongoni mwetu.
 
Askofu Desmond Tutu mtu wa mbali maelfu ya maili kutoka huku nilipokua niliyelazimika kumfahamu kutokana na ushawishi wake juu ya mapigano kuelekea usawa na kuondolewa kabisa kwa ubaguzi wa rangi sio tuAfrica Kusini Bali Tutu Ni picha iliyokuwa na mafunzo mengi kwa wasio waafrika Kusini.Bila shaka Ni kichocheo kipya dhidi ya kuondoa kabisa ukabila na udini miongoni mwetu.
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom