Puerto Rico | Estado Libre Asociado de Puerto Rico

isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
4,125
6,250
| Jumuiya ya Madola ya Puerto Rico, Estado Libre Asociado de Puerto Rico, Commonwealth of Puerto Rico au Free Associated State of Puerto Rico

Puerto Rico
ni kisiwa na mkusanyiko wa visiwa kadhaa katika bahari ya Karibi, Atlantiki na uwanda wa Antilles, ikiwa na mipaka baina ya Jamhuri ya Dominica ' Dominican Republic ' , Virgin ya Marekani, Saint Kitts na Nevis na Visiwa vya Virgin ' Uingereza '.

Puerto Rico.jpg

Bendera ya Puerto Rico

Puerto Rico yenye ukubwa wa eneo zipatazo kilomita za mraba 9,104 sawa na maili za mraba 3,515 nyumbani kwa watu takribani millioni 2,860,853 kufikia Agosti 7, 2020.

Lugha rasmi ni Kihispaniola na Kiingereza, lugha inayozungumzwa na wengi ni Kihispaniola kwa asilimia 85 ikifuatiwa na Kiingereza, Kifaransa na Kiholanzi.

Old San Juan.jpg

La Perla, San Juan ya zamani ©viahero

Pesa rasmi ni Dollar ya KiMarekani, U.S Dollar $1 ni sawa na Cents 100. Kauli kuu ya Kisiwa hiki ni “John ndiye jina lake” | “Joannes est nomen ejus”.

Mji mkuu wa Puerto Rico ni San Juan, mji wenye maendeleo zaidi ukifuatiwa na miji ya Ponce, Bayamón, Carolina, Caguas na Mayaguez.

miramar.jpg

Miramar, pembezoni San Juan ©viahero

Puerto Rico siyo taifa huru wala jimbo la KiMarekani bali ni sehemu iliyokuwa chini ya uangalizi wa Marekani katika jumuiya ya KiMarekani. Kwa tafsiri ya eneo la Puerto Rico ni sawa na zilivyokuwa Guam, Visiwa vya Mariana ya Kaskazini, Virgin ya Marekani na Samoa ya Amerika.

Watu wenye asili ya Puerto Rico ya kuanzia miaka ya 1917 wanatambulika kama raia wa Marekani wakitumia pasi ya kusafiria ya Marekani, lakini raia wa Puerto Rico hawezi kupiga kura ya kitaifa ya kumchagua rais wa Marekani kwa mujibu wa katiba.

Eneo hili kupitia historia ya kale inatambulika vyema kuwa kituo cha ung'amuaji wa watumwa kutoka nchi ya Afrika kabla ya kupitia Cuba na kuelekea Marekani.

Uchumi, Biashara, Kilimo, Uwekezaji, Maendeleo na Utalii

Uchumi katika kisiwa ni wenye kutegemea uzalishaji madawa ' Pharmaceuticals ', kemikali ' Chemicals ', vifaa vya kielektroniki ' Electronics ', masuala ya uchumi na kibenki ' Finance & Banking '.

Uzalishaji mkubwa wa dawa ndani ya Puerto Rico huchagizwa na uwepo wa maji safi yasiyohitaji matibabu kabla ya matumizi.

La-Finca-Maga.jpg

La Finca Maga, bidhaa bora ya Puerto Rico ©See Puerto Rico

Biashara hufanyika pakubwa na mataifa ya Marekani, Ireland na Japan huku uingizwaji wa bidhaa hutegemea Uchina, Hong Kong, Taiwan na Uhispania.

PR Fruits.jpg

San Juan Old Market.jpg

Vyakula na matunda katika soko ©Freshman Puerto Rico

Kilimo ni moja sekta nzuri kwa taifa katika uzalishaji wa mchele, miwa, kahawa, mahindi, ndizi, nanasi na matunda mbalimbali. Nanasi ni tunda lenye heshima na likiwa tunda la Puerto Rico, aina nne za nanasi ulimwa.

Plaza del Mercado Rio Piedras1.jpg

Matunda ndani ya Plaza del Mercado Rio Piedras ©LitePT

Uwekezaji na Maendeleo yanashuhudiwa pakubwa mjini San Juan, mji wenye kiwango cha maisha sawa na Atlanta, Dallas na Seattle huku viwango vya makazi ni sawa na Miami na Los Angeles. Miji ya Ponce, Bayamón, Carolina na Caguas ni sehemu muhimu katika eneo hili.

SJ Old San Juan Fortaleza.jpg

Mtaa wa Fortaleza, San Juan ya zamani ©viahero

Puerto Rico ni nyumbani kwa Plaza Las Américas, sehemu kubwa ya kufanya manunuzi katika uwanda wa Karibi na Casa Bacardi kiwanda kikubwa zaidi uwanda wa Karibi na Antilles.

pinones.jpg

Kivutio cha utalii, Piñones ©viahero

Utalii ni pumzi ya mwisho kwa Puerto Rico, kuanzia Sancturce - C787 Studios, El Mercado Libre na Calle Loiza maeneo yenye kuwakilishwa kwa ukubwa wa kazi za sanaa ya uchoraji, fika hadi Miramar - Cosita Miramar na Teantro Topia utashuhudia uzuri wa dunia huku Condado - 1919, Bayamón na Piñones utaweza kuchangamsha akili na mwili.

bayamon.jpg

Bayamón, Puerto Rico ©Puerto Rico Today

Uwapo Puerto Rico utakuwa karibu na maziwa takribani 46 yaliyoundwa na binadamu, ukipita pembezoni ya fukwe ndefu na yenye kupendeza ya Flamenco, Flamenco Beach ni moja ya fukwe kumi bora duniani kwa miaka 23 mfululizo.

San Juan Beach.jpg

Fukwe ya San Juan ©Jamaal Fareed

condado.jpg

Fukwe ya Condida ©Condvise

Watalii takribani millioni 5.6 kwa mwaka utembelea kisiwa hiki kupitia viwanja vya ndege Luis Muñoz Marin Inter. Airport, Mercedita Airport na Rafael Hernandez Airport.

Conturce Hostel.jpg

Conturce Hostel San Juan ©Conturce Hotels

Elimu

Kiwango cha elimu ni kwa asilimia 92.4, mfumo wa elimu ukiwa na mgawanyo wa msingi, upili na elimu ya juu. Elimu ya juu hutolewa pakubwa na vyuo bora mifano ya Chuo Kikuu cha Puerto Rico, Universidad del Turabo, Metropolitan University, Universidad del Este na Inter American University.

Muziki na Filamu

Unapozungumzia Puerto Rico unachimbua asili ya muziki wa Reggaeton, muziki wenye mjumuiko wa mahadhi ya danza, salsa, afrobeat na dansi ya kielektroniki. Muziki uliyoiteka dunia kwa muda mfupi na kuwa chagizo la uchumi imara baina ya vijana.

Marc Anthony.jpg

Marc Anthony ©LatinMena FM

Muziki ulioasisiwa pakubwa na Dj wa kimataifa raia wa Puerto Rico, DJ Nelson huku ukipiganiwa vilivyo na mfalme Daddy Yankee, Don Omar na waendelezaji kama Ismael Rivera.

Luis Fonsi Ft. Daddy Yankee - Despacito

Puerto Rico ya sasa huwakilishwa vyema na Daddy Yankee ' King Daddy ' aliyetamba na nyimbo mfano wa Gasolina, Rompe, El Mas Duro, Shaky Shaky, Te Sigo Sígueme, Boom Boom akishirikiana na raia wa Afrika Red One, French Montana na Dinah Jane.

Don Omar x Lucenzo - Danzar Kuduro

Don Omar aliyeitikisa dunia na vibao Soledad ' The Last Don ', Te Quiero Pa Mi na wimbo Danza Kuduro uliokaa katika chati za muziki kwa siku 457.

Jennifer Lopez Ft. Wisin - Amor Amor Amor

Huku ujazo na shehena ukiwa baina ya Marc Anthony mwenye I Need You, You Sang To Me, Lie, Between Us na La Gozadera. Jennifer Lopez wa Amor Amor Amor na Se Acabó el Amor, Wisin y Yandel wanaotamba na Callao.

Ozuna - Sigúelo Bailando

Ozuna na Jhay Cortez wenye mirindimo ya Easy, Sigúelo Bailando, Nibiru, Baila Baila na Aura.

Jhay Cortez - Easy

Wengine ni Ricky Martin, Bad Bunny, Lunay, Pyro, Dj Luian, Mambo Kingz, Cauty, Calle Ciega na Anuel AA kwa uchache.

Ricky Martin Ft. Maluma - Vente Pa' Ca

Bad Bunny.jpg

Bad Bunny ©MTV

Wisin y Yandel - Callao

Katika Filamu Benecio del Toro, Rita Moreno na Michel Rodriguez wanapeperusha vyema bendera ya Puerto Rico. Kupitia uchakataji filamu kampuni Isla Films na Lunatic Productions ni chapa ya Kisiwa hiki.

Hii ndio Puerto Rico 🇵🇷
 
| Jumuiya ya Madola ya Puerto Rico, Estado Libre Asociado de Puerto Rico, Commonwealth of Puerto Rico au Free Associated State of Puerto Rico

Puerto Rico
ni kisiwa na mkusanyiko wa visiwa kadhaa katika bahari ya Karibi, Atlantiki na uwanda wa Antilles, ikiwa na mipaka baina ya Jamhuri ya Dominica ' Dominican Republic ' , Virgin ya Marekani, Saint Kitts na Nevis na Visiwa vya Virgin ' Uingereza '.

View attachment 1531149

Bendera ya Puerto Rico

Puerto Rico yenye ukubwa wa eneo zipatazo kilomita za mraba 9,104 sawa na maili za mraba 3,515 nyumbani kwa watu takribani millioni 2,860,853 kufikia Agosti 7, 2020.

Lugha rasmi ni Kihispaniola na Kiingereza, lugha inayozungumzwa na wengi ni Kihispaniola kwa asilimia 85 ikifuatiwa na Kiingereza, Kifaransa na Kiholanzi.

View attachment 1531150
La Perla, San Juan ya zamani viahero

Pesa rasmi ni Dollar ya KiMarekani, U.S Dollar $1 ni sawa na Cents 100. Kauli kuu ya Kisiwa hiki ni “John ndiye jina lake” | “Joannes est nomen ejus”.

Mji mkuu wa Puerto Rico ni San Juan, mji wenye maendeleo zaidi ukifuatiwa na miji ya Ponce, Bayamón, Carolina, Caguas na Mayaguez.

View attachment 1531203
Miramar, pembezoni San Juan viahero

Puerto Rico siyo taifa huru wala jimbo la KiMarekani bali ni sehemu iliyokuwa chini ya uangalizi wa Marekani katika jumuiya ya KiMarekani. Kwa tafsiri ya eneo la Puerto Rico ni sawa na zilivyokuwa Guam, Visiwa vya Mariana ya Kaskazini, Virgin ya Marekani na Samoa ya Amerika.

Watu wenye asili ya Puerto Rico ya kuanzia miaka ya 1917 wanatambulika kama raia wa Marekani wakitumia pasi ya kusafiria ya Marekani, lakini raia wa Puerto Rico hawezi kupiga kura ya kitaifa ya kumchagua rais wa Marekani kwa mujibu wa katiba.

Eneo hili kupitia historia ya kale inatambulika vyema kuwa kituo cha ung'amuaji wa watumwa kutoka nchi ya Afrika kabla ya kupitia Cuba na kuelekea Marekani.

Uchumi, Biashara, Kilimo, Uwekezaji, Maendeleo na Utalii

Uchumi katika kisiwa ni wenye kutegemea uzalishaji madawa ' Pharmaceuticals ', kemikali ' Chemicals ', vifaa vya kielektroniki ' Electronics ', masuala ya uchumi na kibenki ' Finance & Banking '.

Uzalishaji mkubwa wa dawa ndani ya Puerto Rico huchagizwa na uwepo wa maji safi yasiyohitaji matibabu kabla ya matumizi.

View attachment 1531206
La Finca Maga, bidhaa bora ya Puerto Rico See Puerto Rico

Biashara hufanyika pakubwa na mataifa ya Marekani, Ireland na Japan huku uingizwaji wa bidhaa hutegemea Uchina, Hong Kong, Taiwan na Uhispania.

View attachment 1531208

View attachment 1531213
Vyakula na matunda katika soko Freshman Puerto Rico

Kilimo ni moja sekta nzuri kwa taifa katika uzalishaji wa mchele, miwa, kahawa, mahindi, ndizi, nanasi na matunda mbalimbali. Nanasi ni tunda lenye heshima na likiwa tunda la Puerto Rico, aina nne za nanasi ulimwa.

View attachment 1531214
Matunda ndani ya Plaza del Mercado Rio Piedras LitePT

Uwekezaji na Maendeleo yanashuhudiwa pakubwa mjini San Juan, mji wenye kiwango cha maisha sawa na Atlanta, Dallas na Seattle huku viwango vya makazi ni sawa na Miami na Los Angeles. Miji ya Ponce, Bayamón, Carolina na Caguas ni sehemu muhimu katika eneo hili.

View attachment 1531216
Mtaa wa Fortaleza, San Juan ya zamani viahero

Puerto Rico ni nyumbani kwa Plaza Las Américas, sehemu kubwa ya kufanya manunuzi katika uwanda wa Karibi na Casa Bacardi kiwanda kikubwa zaidi uwanda wa Karibi na Antilles.

View attachment 1531218
Kivutio cha utalii, Piñones viahero

Utalii ni pumzi ya mwisho kwa Puerto Rico, kuanzia Sancturce - C787 Studios, El Mercado Libre na Calle Loiza maeneo yenye kuwakilishwa kwa ukubwa wa kazi za sanaa ya uchoraji, fika hadi Miramar - Cosita Miramar na Teantro Topia utashuhudia uzuri wa dunia huku Condado - 1919, Bayamón na Piñones utaweza kuchangamsha akili na mwili.

View attachment 1531221
Bayamón, Puerto Rico Puerto Rico Today

Uwapo Puerto Rico utakuwa karibu na maziwa takribani 46 yaliyoundwa na binadamu, ukipita pembezoni ya fukwe ndefu na yenye kupendeza ya Flamenco, Flamenco Beach ni moja ya fukwe kumi bora duniani kwa miaka 23 mfululizo.

View attachment 1531223
Fukwe ya San Juan Jamaal Fareed

View attachment 1531227
Fukwe ya Condida Condvise

Watalii takribani millioni 5.6 kwa mwaka utembelea kisiwa hiki kupitia viwanja vya ndege Luis Muñoz Marin Inter. Airport, Mercedita Airport na Rafael Hernandez Airport.

View attachment 1531233
Conturce Hostel San Juan Conturce Hotels

Elimu na Afya

Kiwango cha elimu ni kwa asilimia 92.4, mfumo wa elimu ukiwa na mgawanyo wa msingi, upili na elimu ya juu. Elimu ya juu hutolewa pakubwa na vyuo bora mifano ya Chuo Kikuu cha Puerto Rico, Universidad del Turabo, Metropolitan University, Universidad del Este na Inter American University.

Muziki, Filamu na Michezo

Unapozungumzia Puerto Rico unachimbua asili ya muziki wa Reggaeton, muziki wenye mjumuiko wa mahadhi ya danza, salsa, afrobeat na dansi ya kielektroniki. Muziki uliyoiteka dunia kwa muda mfupi na kuwa chagizo la uchumi imara baina ya vijana.

View attachment 1531250
Marc Anthony LatinMena FM

Muziki ulioasisiwa pakubwa na Dj wa kimataifa raia wa Puerto Rico, DJ Nelson huku ukipiganiwa vilivyo na mfalme Daddy Yankee, Don Omar na waendelezaji kama Ismael Rivera.

Luis Fonsi Ft. Daddy Yankee - Despacito

Puerto Rico ya sasa huwakilishwa vyema na Daddy Yankee ' King Daddy ' aliyetamba na nyimbo mfano wa Gasolina, Rompe, El Mas Duro, Shaky Shaky, Te Sigo Sígueme, Boom Boom akishirikiana na raia wa Afrika Red One, French Montana na Dinah Jane.

Don Omar x Lucenzo - Danzar Kuduro

Don Omar aliyeitikisa dunia na vibao Soledad ' The Last Don ', Te Quiero Pa Mi na wimbo Danza Kudo uliokaa katika chati za muziki kwa siku 457.

Jennifer Lopez Ft. Wisin - Amor Amor Amor

Huku ujazo na shehena ukiwa baina ya Marc Anthony mwenye I Need You, You Sang To Me, Lie, Between Us na La Gozadera. Jennifer Lopez wa Amor Amor Amor na Se Acabó el Amor, Wisin y Yandel wanaotamba na Callao.

Ozuna - Sigúelo Bailando

Ozuna na Jhay Cortez wenye mirindimo ya Easy, Sigúelo Bailando, Nibiru, Baila Baila na Aura.

Jhay Cortez - Easy

Wengine ni Ricky Martin, Bad Bunny, Lunay, Pyro, Dj Luian, Mambo Kingz, Cauty, Calle Ciega na Anuel AA kwa uchache.

Ricky Martin Ft. Maluma - Vente Pa' Ca

View attachment 1531274
Bad Bunny MTV

Wisin y Yandel - Callao

Katika Filamu Benecio del Toro, Rita Moreno na Michel Rodriguez wanapeperusha vyema bendera ya Puerto Rico. Kupitia uchakataji filamu kampuni Isla Films na Lunatic Productions ni chapa ya Kisiwa hiki.

Hii ndio Puerto Rico
 
Idadi ya watu 2.8 m; idadi ya watalii 5.6 m exactly twice the population. Inaonekana ni nchi ya maraha sana. Baada ya kuchukua fomu mgombea mmoja alinukuliwa akisema ataifanya Tz iwe kama Ulaya; ha ha ha Ulaya mbali sana; aifanye kama Puerto Rico tu yatosha kama kweli anaweza.
 
Yes, ni eneo la kuvinjari na kitalii ukiangalia idadi ya watalii ni sawa au zaidi ya mataifa kadhaa makubwa.

Rio Piedra's University.jpg

Chuo cha Rio Piedra's

Hotel San Juan.jpg

Hotel San Juan

Hostel H1 Miramar.jpg

Hostel H1 Miramar
 
Kauli kuu ya Kisiwa hiki ni “John ndiye jina lake
Huyu John alikuwa nani?au hii kauli imechagizwa na nini?
 
Back
Top Bottom