PSRS: Ajali zote hizi bado usahili wa madereva mnafanya ujanja ujanja??

Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,503
6,376
Usahili wa awali wa vitendo kwa nafasi ya Dereva ll uliofanyika kuanzia tarehe 6/07/2019 hadi tarehe 26/07/2019 watahiniwa waligawanya katika makundi (Groups)

Katika Group la tarehe 21/07/2019 walifanya watahiniwa (madereva) 21 tu!

Katika majibu yaliyopostiwa kwenye mtandao group hilo hilo lililokuwa na madereva 21 majibu yanaonyesha lilikuwa na watahiniwa madereva 33 na waliochaguliwa ni 22. 😩🤣🤣

Jamani!! Hawa 12 waliozidi wametoka wapi na ndiyo hasa waliopitishwa??

Serikali ina nia ya dhati kweli kupata madereva wazuri katika jitihada za kupunguza ajali kwa watumishi wa umma wawapo safarini??

Mwisho!! Siku hizi kuna mitandao ya kijamii, watu wanafanya usahili na kuunda group la WhatsApp papo hapo! Ukitokea ujanja ni rahisi kujulikana! Au ambaye hakuwepo rahisi kuonekana!!

Mnashindisha watu na njaa mpaka Mkuranga huko halafu ambao hawakufanya usahili ndiyo wanapita maana yake nino??

PSRS mbadilike! Mnaondoa imani kwa wasahiliwa wenu!!
 
Utumishi kujuana mwanzo mwisho na kuna rushwa ya hali ya juu.
Mdogo wangu walifanya oral watu wanne.
Na wote wanajuana ila akaja kuajiriwa mwingine kabisa ambaye hakuwepo ni mwalimu wa st joseph

Sasa kwa nini waliwasumbua watu na je huyo mwalimu si ana ajira tayari?

Nyau kabisa utumishi.
 
Mkuranga Mlienda kufanya nini Boss au Ndo usaili unafanywa huko boss🤔
Mkuu. Interview ya udereva lazima ukatestiwe highway waone kama kweli kazi unaiweza.
Kwa matokeo yaliyotoka inainekana 'utumishi' (VETA) wamepiga chini madereva zaidi ya mia saba kw kutokidhi vigezo
 
Wametisha tena nafasi 400, hivyo mabaharia tujipange kuenda tu maana mgaagaa na upwa hali wali mkavu...japo inauma mtu anapata 65 not selected asee mean mpaka ufike 70 net jambo ambalo lina kigugumizi..
Nb
Ni bora ingekuwa hata 50 maana naamini haya marudiorudio yasingekuwepo
 
Utumishi kujuana mwanzo mwisho na kuna rushwa ya hali ya juu.
Mdogo wangu walifanya oral watu wanne.
Na wote wanajuana ila akaja kuajiriwa mwingine kabisa ambaye hakuwepo ni mwalimu wa st joseph

Sasa kwa nini waliwasumbua watu na je huyo mwalimu si ana ajira tayari?

Nyau kabisa utumishi.

🙆🙆🙆🙆
Hii nchi ni ya hovyo sana!!
 
Ujirani mwema kati ya wakuu wa taasisi zinazo omba vibali vya kuajili na wakuu wanao endesha michakato ya kutafuta wafanya kazi Bora, umeshakuwa na mizizi iliyo komaa kwaiyo Bulldozer litusaidie kukwangua mpka vipele.
 
Ujirani mwema kati ya wakuu wa taasisi zinazo omba vibali vya kuajili na wakuu wanao endesha michakato ya kutafuta wafanya kazi Bora, umeshakuwa na mizizi iliyo komaa kwaiyo Bulldozer litusaidie kukwangua mpka vipele.
Hahahahahahaha
 
Ivi naomba niulize kwa panel ile ya interview unatakiwa umuonge nani au rushwa uwa inatembeaje
Chief tupeane japo uzoefu kidogo wa hii pannel na mfumo mzima wa usaili maana kuna bwana mdogo ameitwa kwenye hii awamu nyingine na yupo huku Mwanza kama ni magumashi apige tu chini mapema
 
Back
Top Bottom