Mashirika ya kijamii yamekuwa yakijitangaza kuwa yana huduma bora sana,mashirika haya ikiwa ni pamoja na PSPF.
Shirika hili lilikuwa linasifiwa kuliko mashirika yote ya huduma za kijamii.
Hata hivyo tumeona katika siku hizi za karibuni huduma za shirika hili zikidorora kwa kiwango kikubwa.
Kwa mfano wastahafu ambao walipaswa kulipa pension zao za kila mwezi angalau ilipofika tarehe moja ya mwezi wa nne mpaka leo hawajalipwa stahili yao.
Mashirika haya yakumbuke kwamba wastahafu hawa wanategemea pension hizi kwa kiwango kikubwa kama vile wafanyakazi wanavyotegemea mishahara yao. Na wakumbuke pia kwamba wastahafu hawa wameneemesha sana mashirika haya.
Ni swala la kiutu tu na uungwana kwamba inabidi watambue mchango wao na shirika hili liwe na mpango thabiti wa kuwalipa wazee hawa mapema. Ni watu waliolitumikia shirika hili kwa siku nyingi kwa hiyo ni vema wakaheshimiwa.
Tukiandika andika hivi mwishoni watapoteza wateja.
Wajirekebishe na watekeleze wajibu wao ipasavyo.