...blah, blah, blah...watu tunashindwa kuelewa nini maana ya demokrasia ya kweli au kukuwa kwa demokrasia....hivi leo hii watu wengi huitolea marekan km nchi iliyopiga hatua ktk demokrasia....
Sawa, lakini tuanze kwa kuangalia etiquette ya internet... font na rangi unayotumia, ni dalili ya ulimbukeni. Why are you trying to ram down our throats whatever it is that you believe! Hii ni dalili ya kukosa uvumilivu kitu kinachopingana kabisa na dhana ya msingi ya demokrasia, what are you trying to hide, mapungufu yako ya uelewa?
kwa mfano Obama pindi anagombea urais Hillary Clinton alikua mpinzani wake lakini sasa hivi huyu mama ndie waziri wa mambo ya nje kwan huyu mama kaathiri kitu gani kwa utendaji wa Obama na serikal yake???
Kwanza Obama na Mama Clinton wote ni democrats na walikuwa wanagombea uteuzi ndani ya Chama chao, mfumo ambao huujui na hata ukiujua hutauelewa. Siasa ya Marekani ni zaidi ya uijuavyo kwani mara baada ya uteuzi wa mgombea Uraisi kukamilika ndani ya chama, wagombea huzika tofauti zao na kuwa kitu kimoja katika kampeni. Ndio maana hivi sasa ndani ya chama cha Republican, wapinzani wa Romney wote wanaanza kumuunga mkono moja baada ya mwingine katika kuipeperusha bendera yao.
Nasema hapa nikiwa na maana ya kwamba Kikwete kumteua Mbatia kuwa mbunge sio ajabu wala jambo geni hata kidogo....kwan angemteua wa chadema tungehoji??? au udp,nk..?? hapa anapanua wigo wa siasa na kuondoa siasa za mazoea na za chuki dhidi ya vyama vya siasa ili hata wa cdm akipata na akafanya hivyo watu wasione km ajabu...
Hapana, ni ajabu na ngeni...Kwanza, marekani wabunge hawateuliwi na Raisi, wanachaguliwa na wananchi kama ilivyo kwa Raisi mwenyewe. Mbunge wa Marekani hafungwi mkono kukitetea chama chake, anaweza kabisa kupingana na msimamo wa chama chake na kuwaunga mkono upinzani. Huko ndiko kupanua wigo wa demokrasia na siyo huu usanii unaofanyika Tanzania, eti mtu aliyekataliwa na wananchi anakuja kuteuliwa na Raisi, this is not democracy, it is disingenuousness!
na ieleweke kumpa mbatia hiyo nafas sio kwamba ccm haina watu au wanachama makini sio hivyo hiyo ndio maana halisi ya siasa za kuvumiliana na kuheshimiana na kwa uwazi zaidi...
Acha upuuzi, Mbatia ni mwenyekiti wa chama cha NCCR aliyegombea ubunge na kukataliwa na wananchi...sasa huko kuvumiliana na kuheshimiana kwa uwazi zaidi kunatoka wapi? Huyu huyu Mbatia amewahi kutuhumiwa na wenziwe ndani ya chama chake kwa undumilakuwili na unafiki na najua hizo ni sifa kubwa ndani ya CCM, je hizo ndizo sifa zilizomkuna aliyemteua?
KONGOTO, please think out of the box!
naomba tubadilike SIASA HAINA ADUI WA RAFIKI WA KUDUMU''' naomba kuunga mkono hoja
Toka lini Mbatia amekuwa adui wa Kikwete kisiasa, last I heard ni kuwa amekuwa na tabia ya kumtetea Raisi hasa pale anapotupiwa lawama kiutendaji.
KONGOTO, nakuomba sana usiwe mvivu wa kufikiri na ujaribu kutafakari kwa mfano huko visiwani tunayo serikali ya mseto, je unaweza kudai kuwa kwa kufanya hivyo wigo wa demokrasia umepanuliwa? Haiingii akilini mtu mwenye akili timamu kuunga mkono hoja ya kijinga kama ya kuopoa viongozi kutoka katika dampo walikotupwa na wananchi.