Proved: Diamond Platnumz alipia Matangazo Youtube

HELA

JF-Expert Member
May 10, 2015
200
191
Leo kwa mara ya kwanza kupitia mtandao wa video wa Youtube nimeshuhudia tangazo la wimbo wa 'Zilipendwa' ambao umeimbwa na wasanii kutoka 'lebo' ya WCB wakiongozwa na msanii wa kimatatifa, Diamond Platnumz.

Wimbo wa huo unajitokeza mwanzo unapofungua video kwenye mtandao huo kama tangazo ambalo inabidi usubiri wa sekunde 5 ndipo utazame video uliyokuwa unaikusudia kuitazama.
diamond45622.jpg


Hii imenishtua kidogo kwani tangu nianze kumfahamu Diamond sijawahi kuona wimbo wake wowote ambao ametumia aina hii ya matangazo.

Ninachoamini na kukifahamu ni kumba mara zote msanii Diamond amekuwa akipata watazamaji wengi wa video zake pamoja na 'subscribers ' kwanjia ya 'Organic Traffic'.

Japokuwa shutuma za kununua 'Traffic' zipo toka zamani, mimi nilikuwa sijapata uthibitisho wowote hadi kwenye video hii ya Zilipendwa.

Nanachojiuliza na ningependa wadau wake wa karibu mnieleza ni hiki.

Kipi kimepata Diamond pamoja na pamoja na lebo yake ya WCB kufanya hili kwenye wimbo wa 'Zilipendwa'?.

Namuheshimu sana Diamond kwa jitihada zake.
 
Diamond kazi anayo mwaka huu.

Mwaka huu ndio atajua watanzania ni watu wa namna gani. Pamoja na kwamba yeye pia katawaliwa na uswahili mwingi, kazi anayo.

Mshaurini aachane na mambo ya kiswahili, uswahili utamgharimu, kama anataka kuendelea kubakia kileleni, aachane na uswahili, ajionyeshe kua yeye ni international artist.

Mashindano ya kijinga jinga awaachie wajinga, aachane na mameneja waswahili swahili, mameneja wa kizaramo, maneno mengi.

Bado nina imani Diamond ni mwanamziki mkubwa, akiacha uswahili kama miaka 3 au 2 iliyopita, bado utawala wa muziki afrika mashariki na kati ni wake.
 
Nyoka Mwenye Makengeza anajaribu kuifunika "seduce me" kwa views!
Diamomd uswahili ndio unamgharim. Akiachana na mambo ya kiswahili na mameneja wa uswahilini, bado hana mpinzani.

Huo wimbo unaousema ni wimbo wa kawaida sana, sema yeye kaupa headline na jamaa katumia hyo kama kupata public sympathy, baada ya Alkiba kutoa wimbo na kesho yake WCB kutoa wao, Alkiba kapata huruma ya watu kwamba anabaniwa na WCB.

Angetumia akili wala huo wimbo wa Alkiba usingefika popote, ungekua ushajifia kifo cha asili, au usingepata media attention kiasi hicho.

Bado naamini Diamond akiacha uswahili atanedelea vizuri, vinginevyo atapotea.
 
Biashara hiko zaidi ya wewe ujuavyo, Kawaida yetu kumchukia kila mwenye nacho, tunadai Diamond aache uswahili wakati na sisi waswahili wenyewe tunapigana vikumbo kwa waganga kila uchao.

Kulipia Tangazo jambo la kawaida sana jombaaa mpaka hao tunawaowakubali wanafanya hvyo ... Soko linabadilika kila siku

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo wewe unataka Diamond aendeleze uswahili kwakuwa sisi ni waswahili?
Acha hizo wewe na ujiamini maana kila kitu wewe unafanya comparison

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni interesting kidogo. Juzi nilisikiliza wimbo huo wa Zilipendwa pamoja na ule wa Kiba "Seduce Me" nadhani nilizisikiliza mara tatu zote. La ajabu ni kuwa kila ninapoingia Youtube sasa, naonyeshwa "Zilipendwa" kuwa ni Up next hata kama wimbo ninaosikiliza hauna uhusiano kabisa na bongoflava! Nililitewa Zilipendwa kama Up Next wakati nilipokuwa nafuatilia Lecture fulani ya Lie Groups and Lie Algebras. Mwazoni sikuona tatizo ila sasa ninaanza kujiuliza kwa nini. Kila nikiingia Youtube, kwa video yoyote ile, ninawekewa Zilipendwa kama Up next. Hapa ni baadhi ya screenshots ninazopata, I can go on and on!!
upload_2017-9-3_21-58-18.png


upload_2017-9-3_22-13-26.png


upload_2017-9-3_22-15-49.png


upload_2017-9-3_23-20-44.png
 
Mbona hiyo siyo nyimbo ya kwanza kwa yeye kufanya hivyo. Na hata amefanya mini sioni tatizo, ukisikia watu wanafanya promotion ndiyo hivyo kaka!! Hata wasanii wakubwa wanafanya hiyo kitu. Tatizo lako wewe ushamba unakusumbua ndugu. Nyimbo mpya ukitoka kufanyiwa promo ni lazima.

Akili zako unanikumbusha siku moja nilienda kufanya kazi kwa mteja wa kampuni ninayofanyia kazi, nafika pale yule mteja akawa anasema "kampuni yenu siku hizi imeshuka sana kwa namba ya wateja, naona munajitangaza sana na wakati zamani munilikuwa hamufanyi". Mimi nikamuuliza swali dogo tu "mama kwani sisi na kampuni kama tigo, ipo ni kampuni kubwa?", "tigo kampuni kubwa". Nikamuuliza tena "huoni kila ikitembea dakika tano unakuta mabango ya tigo?? Ukifungua radio mara kwa mara unakutangazo za tigo??". Mwisho mama akawa kimya tu.

Na wewe acha majungu ndugu yangu, kama akili yaki haielewi maana ya promotion ilo ni kosa lako na mwalimu wako wa darasani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diamond kazi anayo mwaka huu.

Mwaka huu ndio atajua watanzania ni watu wa namna gani. Pamoja na kwamba yeye pia katawaliwa na uswahili mwingi, kazi anayo.

Mshaurini aachane na mambo ya kiswahili, uswahili utamgharimu, kama anataka kuendelea kubakia kileleni, aachane na uswahili, ajionyeshe kua yeye ni international artist.

Mashindano ya kijinga jinga awaachie wajinga, aachane na mameneja waswahili swahili, mameneja wa kizaramo, maneno mengi.

Bado nina imani Diamond ni mwanamziki mkubwa, akiacha uswahili kama miaka 3 au 2 iliyopita, bado utawala wa muziki afrika mashariki na kati ni wake.
Umenena vyemaaa mkuu
 
Ningefurahi kama mtu angenitafsiria nnini uswahili na nani waswahili nina hhofu hili neno au hawa waswahili wanahukumiwa ndivyo sivyo!
Binafsi kiasili ni mswahili chotara wa Zanzibar,Mafia na Mbwera Rufiji huko ndio asili ya wazee wetu na kuanzia babu na bibi zangu pamoja na ahali yao nimeona ni watu wastaarab wa hali ya juu tena waungwana sana-ni jamii ya waswahili kama wenzao wa Tanga Mombasa Unguja na Pemba na kwingineko .
Tafadhali nopebi tafsiri hasa ya waswahili na uswahili ili tupate kwenda sawa na huyu Diamond ambaye kwa maoni yangu kwa kuwa ni mzaliwa wa Darul salaam .
 
Huyu mtoa post ndio walewale waimba kaswida.Kwa hiyo alitaka na yeye aende kwa Mange Kimambi kupromoti kazi zake???Au anajua maana ya matangazo huyu?Afu asisahahu kuwa diamond ndio msanii wa KWANZA EA ambae viewers zaidi ya 100M+ katika kazi zake za muziki.
Acheni maneno ya wivu mwambieni mwenzenu hii ligi haiwezi
 
Boss tatizo lako unaendeshwa sana na mihemko, diamond au WCB ni brand kama ilivyo tigo na boda, Thamani yao kimauzo inategemeana na jinsi gani wanawafikia watu wengi kwa wakati ndio maana munamuona diamond ana endorsement nyingi za matangazo na ubarozi wa makampuni tofauti tofauti kuliko hao wasanii mnaotaka awaige jinsi ya ku promoted kazi zake, ukiwa kanjanja hauwezi kunielewa nachokiongea but kwa taarifa yako hao hao youtube wamempa tuzo huyo diamond kwa best YouTube chanel kwa east and sahara. Sasa ndio upime upuuzi wako.
 
Back
Top Bottom