Propaganda zinatupeleka pabaya; Waandishi waingizwa vyumba vya upasuaji MOI

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Leo tusubiri taarifa za habari kujionea propaganda zinazoenezwa na serikali kuwa mgomo umekwisha.
 
hii sasa ni hatari.lakini kuna video nimeiona sehemu MOI imebaki kama gofu.
 
jana tulimuona aligaisha leo tumeonyeshwa MOI lakini MNH hatuonyeshwi.
Mgomo haumalizwi na vyombo vya habari bali mazungumzo ya dhati.
 
MOI nao wameingizwa kwenye siasa za liwalo na liwe?

ukweli utajulikana ndani ya saa 24 kama ilivyotokea kwa MNH.tukumbuke kuwa huu ni mgomo endelevu,nasubiri tamko la madaktari kama wameridhia kurejea kazini.
 
Kumbe wamewahonga vyombo vya habari. Hata kuna jamaa kasema hapa mbona hawa madaktari bingwa ni wapya hamfahamu hata mmoja naye ni mfanyakazi wa pale.
 
ITV nayo ni TBC!!! jambo la maana hapa ni tamko la madaktari kama walivyoamriwa na mahakama lionekane kwa maandishi katika vyombo vya habari ili wananchi warudishe imani na kufika hospitali. kufuatana na taarifa ya ITV usiku huu wagonjwa walikuwa wachache wakiwa hawana imani kama mgomo umekwisha. madaktari wawe wazi katika hili - sizitaki mbichi kusiwepo
 
madaktari wanaofundisha MUHAS waliombwa kuingia wodini ili kupiga picha.
Wananchi wanadanganywa ili wakaonje athari za mgomo huu ni uhaini jamani.
Kesho tutasikia story nyingine kutoka kwa hawa hawa itv.
 
wagonjwa waliombwa ridhaa ya kuonyeshwa kwenye TV?kama sivyo wana haki ya kudai fidia.mateso kwa mgonjwa yasiwe turufu ya kujitafutia umaarufu.ITV punguzeni kigeugeu msije mkawa kama TBC.
 
Zama hizi za smartphone na Internet ni aibu sana kutumia propaganda za karne ya 18. Shida nyingine viongozi wanasubiri taarifa za kuletewa na kutazama kwenye tv, watendaji wanawadanganya kisha wanapanga vyombo vya Habari.

Chombo cha Habari kinachokubali kutumika kudanganya umma nacho kinashiriki mauaji ya raia. Wanalipwa bei gani? Kufa kufaana
 
Tatizo hawa wakubwa wanafikiri bado tuko kwenye zama za RTD na S.L.P

Umenikumbusha mbali, umesahau Airform- ukitumia hiyo huna haja kubandika stempu, every thing is inclusive.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Unajua mimi sielewi kabisa kama hawa wauaji wanajua ya kuwa dunia ya sasa ni imebadilika na watanzania c hao wa zamani kama wao walivyo. Nitaendele kuwasisitiza katika dunia hii hakuna yasiyo kuwa na mwisho, teseni, ngoeni meno na kucha na hata kuhasi mhasi, Mungu kashaamru mushidwe na hamtashinda.
 
Back
Top Bottom