Chilojnr
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 302
- 1,306
Sijajua kwa serikali ya Tanzania kama wameanza kuwekeza kwenye filamu kuionyesha dunia ni kwa namna gani Watanzania tulivyo, serikali ilivyo kwa wananchi wake, bado sijajua.
Kwa Marekani! Serikali yao inajua kwamba filamu zina nguvu sana na ndiyo maana vitu vingi sana wanafikisha ujumbe kupitia filamu hizo, zinaangalia na mamilioni ya watu, nao wanapitisha propaganda zao humohumo.
Serikali ya Marekani ina nguvu sana, na inaogopwa duniani, asilimia kubwa imechangiwa na filamu hizi tunazoziangalia, wamekuwa wakitumia nguvu sana huko, na kweli wanafanikiwa sana.
Itazame filamu kama Captain Phillips! Wewe utaitazama kwa jicho la kawaida ila kiukweli serikali yao walitaka kukuonyesha kwamba usicheze na mtu anayeitwa Mmarekani, serikali itafanya lolote lile kumuokoa mtu wao bila kujali gharama yoyote ile.
Ile filamu ni ujumbe kwa waharamia wa baharini, kwamba nyie tekeni meli ila msithubutu kuteka meli ya Kimarekani, gharama yake huwa kubwa sana, na mnaweza kupotea muda wowote kwa kuwa sisi tunajali sana wananchi wetu.
Cheki filamu kama Eye In The Sky. Kwenye ile filamu walitaka kutuonyesha kwamba mpaka Marekani wanalipua sehemu, basi jua wamefanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanaokoa maisha ya watu wengine kabla ya kumuua mtu wao.
Angalia jinsi watu walivyohangaika kuyanusuru maisha ya mtoto, walifanya mengi ila mwisho wa siku walipoona wameweza kumuondoa sehemu husika, wakalipua, ila bomu lilikuwa kubwa sana, mtoto akafa. Hapa wanakwambia hakufa kwa kukusudiwa.
Serikali ya Marekani inatumia nguvu kubwa kupitia filamu, wanaendelea kutuonyesha nguvu ya jeshi lao huko, wanasambaza ushoga, usagaji kupitia hukohuko, na sisi tunakubaliana nao kwa kuwa tunapenda filamu.
Filamu zina nguvu sana, tena sana. Mnaweza kuonyesha hata jinsi Watanzania wanavyotumia nguvu kuwalinda watalii, kulinda wanyama wao, maliasili nyingine, zote zikawekwa kwenye mtindo wa filamu, watu wakajulia huko.
Ila bado sijajua kama serikali ishaamua kulifanya hivyo ama wanafikiria kulifanya. Kama bado hawajalifanya, wanatakiwa kulifikiria, hizi filamu zina nguvu sana kusambaza propaganda duniani.
Ni maoni binafsi.
Imeandika kwa Nyemo Chilongani.
View attachment 2144498