Progressive People's Party of Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Progressive People's Party of Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Nov 15, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Waungwana,

  Maboksi yamenishinda, narudi nyumbani na narudi kuanzisha chama. John Tendwa naomba ajiandae kwa ujio wa Mchungaji.

  Chama changu kinalenga kuleta maendeleo kwa Mtanzania na si kwa kauli tuu bali kwa vitendo.

  Nimejifunza mengi kutoka kwa TANU, CCM, CUF, CHADEMA, TLP na hata katika kubeba maboksi.

  Lengo kuu la kwanza ni kuelimisha Mtanzania ajue haki yake ya kiraia na kikatiba.

  Pili ni kumpa Mtanzania si tegemeo au tarajio tuu kuwa anaweza siku moja kupata ngekewa na kuneemeka, bali ni kumfundisha njia bora za kujineemesha kwa kumpa uimara wa moyo, roho na kisha wa kufanya kazi atambue kuwa hakuna lisilowezekana.

  Tatu, katika kumjenga Mtanzania huyu upya, Chama changu kitalenga kumjenga Mtanzania anayejitegemea kwa kutumia nyenzo na mazingira aliyomo.

  Nne, Chama cha PPPT kitahakikisha kuwa Watanzania wanapewa kipaumbele katika shughuli zote za uzalishaji kwa kutoa elimu ya nadharia na vitendo kuelewa mifumo ya Uchumi iliyoko Tanzania na manufaa yake kwa jamii na maisha yao.

  Tano, PPPT lengo lake la muda mrefu ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa si nchi yenye kuishi katika ndoto za Amani, Utulivu na Mshikamano, bali ni kwa vitendo ambavyo vitadhihirika kwa kumjenga Mtanzania aondokane na Umasikini, Ujinga na Maradhi. Katika lengo hili, PPPT itahakikisha kuwa inashirikiana na Wananchi wa Tanzania kuujenga mfumo mzuri na bora ambao ni adilifu wa uzalishaji mali na uchumi na kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2035, Tanzania itakuwa inazalisha na kulisha nchi zaidi ya 10 inazopakana nazo.

  Sita, Maendeleo ya jamii, yatatokana na mfumo bora wa Elimu na Afya ambao ni chimbuko na msingi mkuu wa Ajira na Uzalishaji mali. Mfumo wa elimu na Afya utapewa kipaumbele ili kujenga Taifa la Watu walioelimika kwa dhati na wenye uwezo wa kufanyia kazi elimu na ujuzi wao kwa kuajiriwa au kujitegemea na Taifa lenye watu walio na afya bora inayoandamana na lishe.

  Saba, PPPT ni chama chenye mrengo wa kati, kitajenga kwa kuchagua mfumo bora wa Uchumi unaowafaa Watanzania, kukiwa na nia ya kujenga nchi ambayo Serikali yake si kubwa na yenye kunenepa kwa utapiamlo, bali ni Serikali iliyo imara na yenye afya bora (lean and healthy) ambayo itapunguzwa ukubwa wake kwa asilimia 50 katika kipindi cha miaka 10 baada ya PPPT kuingia katika mfumo wa kisiasa kuanzia ngazi za Mtaa, Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya na hata Taifa.

  Nane, kwa kuwa Tanzania iko njia panda kuelewa mfumo bora na sahihi kwa wakati (nyakati) na mazingira yetu kiuchumi, PPPT italenga kuelimisha na kutoa msukumo wa Ujasiriamali na kujitegemea kama mfumo mpya wa kiuchumi ambao utakuwa na vibwagizo (element) kutoka kwenye mfumo wa Kibepari, Kikabaila na hata kijamaa katika kuijenga upya Tanzania.

  Tisa, PPPT itahakikisha kuwa inashirikiana na kwa ridhaa ya wananchi na dhamana kutoka kwa Wananchi kuwa shughuli za uzalishaji kutoka kwa wawezekaji wa nje, zinawanufaisha Watanzania kwa zaidi ya Asilimia 3 tunazopata leo hii. Lengo litakuwa ni kuhamasisha Watanzania kushirikiana na Wageni wawekezaji na kuwa washiriki na wabia katika shughuli za Uzalishaji mali na hivyo pato la Taifa kuongezeka kupitia viwango vipya vya kodi na ushuru ambavyo asilimia 50 ya mapato hayo yataelekezwa moja kwa moja kwa wananchi na sehemu husika zilizozalisha mali hizo na kujishughulisha kiuchumi.

  Kumi, PPPT kina dhamira ya kurudisha heshima ya Mtanzania na Utu wa Mtanzania awe wa upande wowote ule wa Muungano, dini, kabila, umri, jinsia, kiwango cha elimu au aina ya Ajira. Kwa Tanzania kuwa nchi yenye uimara wa kiuchumi ambao ndio msingi mkuu wa kuhakikisha kuna Amani, Mshikamano na Utulivu wa kweli, kila Mtanzania atarudishiwa haki yake ya Kikatiba na aliyopewa na muumba kwa kuthaminiwa nafasi yake katika Taifa na zaidi, dhamana yake kupitia sanduku la kura.

  Kumi na Moja, PPPT itahakikisha kuwa Demokrasia inajengwa upya, kwa kuwa na mfumo shirikishi wa Kiutawala, Kikatiba na Kiserikali ambao utatoa nafasi sawa kwa kila Mtanzania bila ubaguzi au kujali maslahi ya kundi fulani. Mfumo huu utatoa nafasi sawa kwa kila mtu kushiriki katika uzalishaji mali, kushiriki katika siasa na uwakilishi bila kuegemea kutoa upendeleo kwa kikundi kimoja au kwa chama kimoja chenye nguvu.

  Mwisho, nawaomba mjiunge nami katika safari hii mpya na wote mnakaribishwa kujiunga mlete mawazo mapya ya kimapinduzi ikiwa tu, mtakuwa tayari kumtumikia Mtanzania na si kutumikiwa na Watanzania!

  Akhsanteni,
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishka,
  Mkuu nakutakia kila la kheri.... Unatisha.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Chama hiki kipya kitafanya nini kushughulikia tatizo la ufisadi:

  a. Benki Kuu
  b. Serikalini (wizarani)
  c. Wahusika wa ufisadi
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh mara imeshakuwa hivyo!
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Katika mfumo bora wa kiutawala, Sheria lazima zifuatwe na Wananchi na wanaotunga Sheria na dhamana ya kutunga Sheria ni lazima wafanye kazi kwa kutimiza wajibu na majukumu yao.

  Kilichotokea Tanzania ni kuvunjwa kwa Sheria na Wananchi wake na kukosekana kwa kuwajibika kwa waliopewa dhamana ya kulinda na kuhakikisha kuwa Sheria na Kanuni zinafuatwa.

  PPPT katika safari yake ya kujenga Taifa, itahakikisha kuwa Sheria, Kanuni na Katiba ndio dira za nchi na si utashi wa mtu mmoja mmoja au vikundi maalum.

  Hivyo, kabla ya kuanza kushughulikia ipaswavyo yaliyopita ya kuhujumu nchi, kazi ya kwanza itakuwa ni kuhakikisha kuwa Sheria, Kanuni na Katiba zinafanya kazi kwa haki na zinavyopaswa, bila kuteterekea kutokana na msukumo wa kisiasa, hujuma au namna yoyote ile ambayo lengo ni kutafuta mianya ya kukiuka Sheria, Kanuni na Katiba.

  Kisha kwa ridhaa na dhamana ambayo PPPT imepewa, PPPT itafuatilia kwa kutumia kitana kila kitu kinachogusa uchumi wa Tanzania kuwa kuangalia mapengo na matatizo yaliyotokea na kuhakikisha hatua madhubuti zinachukuliwa kuziba mianya ya kuhujumu nchi na hatua kali za kisheria na kikatiba zitachukuliwa dhidi ya yeyote yule ambaye amevunja sheria, kanuni na kukiuka Katiba.

  Hivyo kwa mifano hiyo mitatu, naamini kuwepo kwa mfumo bora na uongozi imara, PPPT itaweza kutatua matatizo ya kale na yajayo kwa kuyafanyia kazi na kutoa maamuzi ya haki kwa kutumia Sheria, kanuni na muongozo wa Kikatiba.
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mkandara,

  Nataka ukiamua kwenda Nansio, usitafakari mara tatu tatu kama upande ndege mpaka Kisumu, au basi kwenda Serengeti. Nataka uwe na uwezo wa kuchagua namna fanisi ya kusafiri kwenda Nansio iwe ni kwa anga, Barabara, reli na hata meli.

  Zaidi, nataka kuhakikisha ukifika Nansio, hutakuwa na hofu au mashaka kuwa ukiugua ni Lazima uvuke ziwa na kwenda Bugando au kupandishwa ndege kurudi Muhimbili.

  Aidha, nataka kuhakikisha ukiamua kwenda Nansio, shughuli na huduma zote unazopata Dar Es Salaam iwe ni umeme, maji ya bomba, chakula, bidhaa, huduma na lolote lile, hutaona tofauti sana na Dar Es Salaam zaidi ya tofauti ya majengo na watu, kuwa huko mtaongea zaidi Kikerewe.

  Ama nataka kuhakikisha kuwa Wajukuu wako wakiamukuja kukutembelea au kuishi na wewe, ubora na kiwango cha elimu na malezi watakayoyapata ni sawa na wao kuishi Sinza au Nyakahoja!
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Mchungaji usisahau kupitia Bagamoyo lazima ukatengenezwe kidogo mkuu, usione vyaelea vimeundwa yakhe!

  Respect.


  FMeS!
   
 8. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hili jina si geni masikioni mwangu.........! humu sio mule alipokuwepo somebody ABUBAKAR? na kile cha MWAKITWANGE kilikuwa kinaitwaje?
  naomba kujuzwa...!
   
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Rev., tayari umeshapata mwanachama hapa! Nitajiunga nawe...
  Naomba kuwa mmoja wa ma-strategists wako.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh hii imekaa vizuri kweli maanake nimeshasahau kabisa lugha yangu..muhimu tu mrudishe Chief wangu kuwa mkuu wa wilaya ana uchungu zaidi ya watawala wengine.. Heee heee hee!
   
 11. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Duuh!! Ama kweli siasa kiboko... hata hivo Bagamoyo hawafui dafu kwa Gambushi!!
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  sijui, labda unaichanganya hii na pppt ya mashirika na serikali...
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Ndugu yangu heshima mbele sana, kama Roma hawana macho basi na wewe ni lazima kuyatoa, bongo haijabdilika mkulu bado iko vile vile bila kupitia huko Bagamoyo, au basi hata Kwera kwa Mzindakaya utachekesha mjini hapa!

  - Hujasikia kwamba viongozi wengi wa juu hushinda bila nguo pale Salender-Bridge, lakini huwezi waona unless na wewe uwe mzima kama mimi, Bwa! ha! ha! Unafikiri unaweza kuingia siasa za bongo hivi hivi tu na macho juu!

  - Wewe huoni kina Makamba na Kingunge wanapeta tu unafikiri ni bure, hao ndio ma-co ordinator wenyewe wa ndumba na Ikulu, Bwa! ha! ha!

  Respect.


  FMEs!
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  we got to deal with these au yatarithishwa chama kimoja kwenda kingine; we can not start afresh without dealing with some issues of our past.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lakini tusifanye Utani wakuu zangu hii ya Rev kweli imekaa sawa?
  Kwa nini mkuu wangu usijiunge na chama fulani kisha toka humo ukakua kisiasa kabla hutafikia maamuzi kama haya. Kuanzisha chama kipya inachukua nguvu kubwa sana tena fedha nyingi sana unaweza kufilisika kabisaaa kuwavuta maskini wenye njaa.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  upande mwingine ni hivyo vyama vingine kukumbatia mawazo ya Reverend au vikubali kuvunjika na kuundwa chama hicho kipya cha PPPT..
   
 17. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Usihofu, sometimes inaweza kama kumsukumiza mlevi tu vile... huchelewi kukuta mrundikano wa mivyama isiyo na nyuma wala mbele unafikia kikomo kwa kuwa absorbed na nguvu mpya ya PPPT. Just imagine, akina Mrema, SAS, Slaa, etc etc, wana defect kokote waliko na kujiunga na hili. This is not a dream, the possibility is there! Kwenye tug-of-war wapambe hukimbilia upande wenye nguvu zaidi!
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,
  Nimesoma mahala akisema chama chake kina mrengo wa kati, ndio upi huo (wa kati kulia au kushoto)... Au ndio nawe unaanzisha mapinduzi mapya ya kifikra kuunda mrengo wa KATI yaani usiofungamana na upande wowote ila kwa kuzingatia Mazingira na watu wake!
   
 19. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  May be Liberal?!
   
 20. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  FMES.

  Bagamoyo yetu ni vijijini kwa Watanzania, ni mitaani huko mijini. Uhalali na Uimara wetu hautatokana na kumeza maganda ya mayai ya mjusi au kubandika ****** yetu kwenye kuta za ofisi!

  Sisi tutatengenezwa kwa ridhaa ya wananchi. Tutawahubiria Wananchi na kuwaonyesha kwa vitendo tunachotaka kufanya kifanyike kwa manufaa yao na kuwashirikisha katika mchakato mzima na wao waamue kama wanatuamini na kutupa ridhaa na dhamana ya kuwaongoza au la.

  Kwenda bagamoyo ni sawa na kucheza upatu, mwenzko naye huenda Bagamoyo na kama yeye ataamini kupanda mnazi kinumenyume kichwa chini miguu juu ili wananchi wampende na kumpa kura, hiyo ni shauri yake.

  Katika mfumo wa haki na utu, dhamana hutoka kwa watu na si Milingotini kwa Ajuza fulani au Kibabu fulani kinachokusanya ngozi za Mazeruzeru!
   
Loading...