Profits Are Better Than Wages. Do you agree?

Nxt Millionaire

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
406
Reaction score
89
Profits Are Better Than Wages.

My mentor, when I was 25 years old, dropped a phrase on me that changed my life forever when he said, “Profits are better than wages. Wages will make you a living. Profits can make you a fortune.”

You know it is a bit difficult to get rich on wages, but anybody can get rich on profits. Profits change your whole attitude, even if you start part time—whether it’s part time on your entrepreneurial business, network marketing company or service business.

It can be a landscape business in the summer or hanging Christmas lights in the winter. It can be training, consulting or tutoring. It can be your hobby, such as painting, writing, crafts, woodworking, computers or cooking. But once you start investing even part-time effort into your own business, you will find how much more exciting it is to get up in the morning and go to work on your fortune, even if you’re only spending a few hours a week doing it.


How empowering it is to be able to go to work on your fortune every day rather than going to work to pay the rent. Now it is noble to go to work to pay the rent, but if you could also parcel out part of your time, go to work to make your fortune.
Your whole attitude changes. Your spirit changes. It is in your voice. It is in your face. It is in your gestures. And then you can say, “I am now working full time on my job and part time on my fortune because I found a way to make profits.” Wow!
And I will know what you mean.

By Jim Rohn.

How far do you agree with Jim Rohn? your comments will say it all.
Merry Christmas and Prosperous New Year 2013, See you at the top.
 
kabla ya kupata profit unakuwa umetoa expenses , mara nyingi kodi inalipwa baadae wakati wages unakuwa ushakatwa , mwenye mshahara wa mil 24 kwa mwaka sio sawa na anaye pata faida ya mil 24 kwa mwaka
 
sasa kama mnayajua hayo huko mnafanya nini njooni huku japo mwanzo mgumu lakini ni bora mje haraka kazi waachieni watoto zenu ala!
 
Mkuu Nyenyere, Nimeipenda hii, "IF YOU WANT MORE FREEDOM FACE YOUR FEARS"

Hii ndo changamoto kubwa kwa watu wengi, watu wanajifungia ktk FEARS zao badala ya kuzishinda, na kutafuta kila aina ya visingizio vya kushindwa.

To move forward we need to face our fears, change the way we perceive somethings or opportunities before us.
 

Huu ndo Ugonjwa mkubwa sana, Fear, mkuu kila mtu ukimuuliza atakuambia anapenda sana kufanya biashara ila tatizo ni fear, yaani mtu anashindwa biashara kabla hata ya kuifanya,

Kuingia katika Ujasirimali kunafananishwa na wale jamaa wanao vaa Mabomu na kwenda Kujilipua, ni lazima ujitoe mhanga,

Ni lazima Uchome Meli Moto, waturuki walivyo kuwa wakifika Pwan ya Mapigano enzi hizo, walikuwa wakichoma Moto meli zao zote zilizo wafikisha eneo la vita, hii ilimanisha kwamba hawana Optional nyingine zaidi ya Kushinda Vita, Why?
1. Wakishindwa bado watauwawa kwa sababu wameisha choma moto meli zao hivyo hawataweza kukimbia

- So iliwabidi washinde vita ili kuokoka, Na kweli walikuwa wanapambana kufa na kupona huku wakijua wanahitaji tu kushinda,

Katika Biashara kuna Chalengi nyingi sana, Ikiwemo kukatishana Tamaa, so unahitaji kuwatupilia mbali wale wote wanao kwamisha wewe kusonga mbele, Futa namba zao, Badili hata Namba kama ikibidi,

Utakapo kuwa unaingia kwenye Biashara utakuwa na Optional Moja tu ya Kupambana hadi tone la Mwisho, Make kule mtaani ulisha wafutilia mbali baadhi ya Marafiki, Umegombana na ndugu zako kwa sbabau ya Biashara, Umekosana na Wazazi, so ni lazima upambana kufa na kupona,

SO UNAHITAJI KUCHOMA MOTO MELI KABLA YA KUANZA SAFARI YA UJASIRIMALI

 
Mkuu Chasha, nakupa "LIKE", umeongea yote, yap, inabidi kuchoma meli zetu moto, tuingie ktk ujasiamali kwa lengo moja tu, USHINDI, na c kujaribu, ndipo utaona mafanikio.
Neno "USIOGOPE" or FEAR NOT, wataalamu wa Biblia wanasema limeandikwa mara 365, ni kwanini?
Mungu alijua woga ni siraha moja wapo ya shetani, hivyo akataka watu wake wasipotee, kila waamkapo waliseme neno hilo.
 
Ya mkuu kuaply inawezekana kabisa, Nex Milionare kasema ishu ni Uoga, Na hii iko hadi kwenye Mitihani, Utakumbuka wakati wa Paper, kabla hamjaanza paper huwa kuna uoga wa kufa mtu, Ila ukisha piga paper ya kwanza na yapili, baada ya hapo unaona ni sawa tu,

Kwenye Business ukiisha ingia uoga wote hukimbia, Ila Starting ndo kuna kazi sana ila Huna Budi Kuchoma Meli Moto,

Huwa na fikilia sana kuhusu Kuajiriwa na kujiajiri, kwa sababu ya Uoga mtu yuko tiyali kuajiriwa na kulipwa hata 80,000 kwa mwezi kuliko kujiajiri na kupata 600000 kwa Mwezi,

ILA KABLA YA KUONDOA UOGA NI LAZIMA KWANZA UKOSANE NA BAADHI YA WATU,

Watu hujenga uoga kwa sababu ya Kukatishana tamaa, Na nimakosa makubwa sana Kuenda Kuomba Ushauri wa Kuanza Biashara kwa Mtu ambaye anasubiria mshahara mwisho wa mwezi, huyu mtu ni lazima akupoteze, Watu walio ajiriwa huwa hawapendi kutoa Ushautri Postive kwa Mtu anaye taka kujiajiri, Mara nyingi hutoa Ushauri Negative na wa kukatisha tamaa, ilimuradi tu Muwe katika Jahazi moja,

Na hata Ndugu wa Karibu Mfano Wazazi, na Marafiki nao huongoza kwa kutoa Ushauri Negative, na wa kutisha, SO UNAPO ANZA HII SAFARI USIJARIBU KUOMBA USHAUR, MPKA PALE ITAKAPO BIDI LAKINI KAMA UNA INFORMATION ZOTE WEWE SONGA MBELE,

Ukisikia mtu ana ongea na kusema ana mpango wa kujiua au kunwa Sumu, Ujue huyo hatakaa afanye hivyo, Ila mwenye nia ya Kujiua hujiua bila watu kutarajia,

So wewe fanya kile ambacho watu hawakutarajia,
 
mii sikubaliani. wages are better than profits sababu,

1.profit hubadilika lakini mshahara wako ni constant (ukiacha cases za kupandishwa cheo),

2 ofisi ni lazima inilipe mshahara wangu kwanza kabla haijajua imamake profit au loss kiasi gani) kwahiyo mshahara wangu umepewa kipaumbele. mshahara wangu upo

3. mshahara upo pale pale hata kama kuna siku ambazo hukuzalisha/kuuza katika mwezi wakati profit huweza kushuka kama hakuna mauzo.

4. kupokea wage hakukupi stress. huna mawazo ya kucover costs zozote za uzalishaji, ikifika mwisho wa mwezi unasmile tu. ni tofauti na kama ungekuwa unaearn profit, lazma umake sure umelipa gharama zote za uzalishaji including wages.

nani anabishaaaaaaa????
 

Mkuu wewe unapotoka sana, ukiwa kama Mjasirimali, Pamoja na kwamba Mshahara wako ni Profit, bado Malupu lupu mengine utayapata kama aloance ya Safari, na kazalika,

Profit unayo pata ni baada ya wewe kuwa umetoa cost zote ikiwemo matumizi yako ukiwa katika shuguri za biashara, wakati Mshahara ndo kila kitu

Hapo kwenye Red, labda unazungumzia mishahara ya huku Bongo, Ila kwa wenzetu watu wanalipwa kwa saa, unalipwa kadri unavyo fanya kazi na si vinginevyo, ukiugua hakuna kulipwa,
 

'UNAHITAJI KUCHOMA
MOTO MELI KABLA YA
KUANZA SAFARI YA
UJASIRIMALI'!much thnxs mkuu,nitachoma meli yangu,god bless u
 
Kweli profits are better than wages but sometimes you may need wages to make profit.
 
'UNAHITAJI KUCHOMA
MOTO MELI KABLA YA
KUANZA SAFARI YA
UJASIRIMALI'!much thnxs mkuu,nitachoma meli yangu,god bless u

Ya mkuu ni Kuchoma Meli Moto au Kufanya kama Mungu alivyo waagiza Rutu na Familia yao kufanya wakati wanaondoka SODOMA NA GOMORA, Mungu aliwaagiza wanapo ondoka SODOMA wasitazame nyuma, Mungua lifahamu fika endapo hawa watu wange tazama tazama nyuma hakika wangerudi Kwenye ule mji, that is why aliwaonya kuhusu kutazama nyuma,

Kwneye Biashara unapo anza ni Kuwa kama Rutu na Familia yake isipo kuwa Mke wake aliye Tazama nyuma kukumbuka starehe za ule mjia na akageuka kuwa nguzo ya Nchumvi,

Kwenye Ujasirimali kuna chalengi nyingi sana ambazo bila kuamua kuangalia mbele tu hutaweza kufanikiwa kabisa, Kuingia kwenye Biashara kunamaanisha kuna vitu vingi sana utavikosa, Mfano

1. Hutaweza kuwa na washikaji zako vijiweni tena

2. Hutakuwa na muda wa kwenda viwanja mara kwa mara
3. Familia yako inaweza kukosa malezi yako make utakuwa bise sana

4. Hutaweza kwenda kutembelea Ndugu zako mara kwa mara kama ulivuo kuwa ukifanya,

Na zingine nyingi, so SAFARI HII INAHITAJI USITAZAME NYUMA, Make kutazama Nyuma utakumbuka Starehe za Mtaani, Washikaji wako, Mechi za Uingereza na mengine mengi, Utakumbuka Malupulupu ya kazini, utakumbuka Gari la kazini lililo kuwa likikufuata nyumbani,

SO NI KUWA KAMA RUTU WAKATI AKIONDOKA SODOMA NA GOMORA,"Hakuna kutazama Nyuma"

 
Huu uzi umenipa moyo wa ujasiri. Asanteni wote mliochangia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…