Wakuu unajua wakati mwingine......Haya,hebu mwenye Paper yoyote ambayo Kitila ameandika alete hapa halafu tuijadili hiyo Paper badala ya kumjadili yeye kama yeye maana Uprofesa wa mtu unajadiliwa kwa ku-challenge paper yake kwa hoja na yeye aje aitetee
Kwanza ni wapi tulikompima katika taaluma yake ya Saikolojia hadi tuseme uprofesa wake una mashaka? Maana yeye ni mwanasaikolojia kitaaluma sidhani kama application yake inafanana na elimu ya nyota sijui unajimu
Tuwe sasa na honest and intellectual debate ! ! !
Kumshutumu mtu bila kuihoji kauli yake ni sawa na kupoteza muda...ikumbuke kuwa kila mmoja huwa na upekee katika kuwasilisha jambo na maana ya mzungumzaji hutofautiana na ya msikilizaji (implication). Ubaya na uzuri wa mtu upo kwa adhaniye. Kilicho kubaya kwa bwana A ndicho huwa kizuri kwa bibi Z na kinyume chake. Kuwa profesa ni mchakato mgumu na kueleweka katika jamii isiyo na uprofesa ni hatua ngumu zaidi. Wengi tunaojadili siasa na vyama bado hatuelewi hata definition sahihi ya siasa, tupo kama bendera...tujifunze kuzihoji kauli na mantiki zake na tusiwe wepesi wa kuwashambulia watu!!!