Professor Mkumbo na siasa za hovyo

Professor Mkumbo na siasa za hovyo

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,441
Wakati mwingine nikifikiria sababu ya Huyu Professor kupewa huo Uprofessor sipati jibu,inakuwaje msomi mwanasiasa apewe uprofessor na uwezo wake kimaamuzi ni mdogo kiasi hicho?hivi ni nani anayewapa au kuwatunukia watu uprofessor?ni viwango gani vinaangaliwa au level ya mtu?

vitendo anavyofanya huyu so called new professor vinasababisha sisi watazamaji wa mambo kujiuliza mara mbili,katoka CCM kaingia Chadema,kasababisha migogoro Chadema kafukuzwa,kaingia chama kingine na huko anasababisha tena migogoro,,,,,,,,,,,,

sasa huyu professor ina maana hana uwezo wa kuona mbali na kujua kuwa kuna kitu kinakuja?ina maana matukio yote yanayomtokea hana uwezo wa kushtuka mapema na kukaa pembeni ili asijadiliwe kwenye upuuzi?? mbona sisi watu wa kawaida tusio hata na hadhi ya kuitwa professor tunajua nini kinakuja kwa kusoma matukio??

Kitila Mkumbo bana ni aibu sana na kwa taarifa yako ni kwamba unaanza kufanya watu kuona uprofessor ni kitu cha kawaida sana kama jamaa mwingine aliyetufanya kuona Urais ni kitu cha kawaida sana,

acheni kuharibu fani hizi tuzitunze kwa vizazi vijavyo,Kitila usikubali kuwa sababu ya watu kudharau uprofessor tafadhali sana kaa pembeni kaka achia wenye uwezo na wapo wengi sana
 
Anayumba baada ya kutoswa CHADEMA bila kutarajia-alijona think tank ya chama.
 
rosemarie

U professor kwa waafrika hususan watanzania usikupe shida is just a title tu hakuna jipya.

Ulisikiliza mahojiano ya Tibaijuka na kafulila star TV?

Uliona Muhongo alivyokuwa akijibu hoja bungeni?

Unaweza ukaamini wale ni maprofessor?

Si hao tu wako wengi na huyo angekua na akili asingekubali kuendeshwa na Zitto Kama mtoto.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu unajua wakati mwingine......Haya,hebu mwenye Paper yoyote ambayo Kitila ameandika alete hapa halafu tuijadili hiyo Paper badala ya kumjadili yeye kama yeye maana Uprofesa wa mtu unajadiliwa kwa ku-challenge paper yake kwa hoja na yeye aje aitetee

Kwanza ni wapi tulikompima katika taaluma yake ya Saikolojia hadi tuseme uprofesa wake una mashaka? Maana yeye ni mwanasaikolojia kitaaluma sidhani kama application yake inafanana na elimu ya nyota sijui unajimu

Tuwe sasa na honest and intellectual debate ! ! !
 
Wakuu unajua wakati mwingine......Haya,hebu mwenye Paper yoyote ambayo Kitila ameandika alete hapa halafu tuijadili hiyo Paper badala ya kumjadili yeye kama yeye maana Uprofesa wa mtu unajadiliwa kwa ku-challenge paper yake kwa hoja na yeye aje aitetee

Tuwe sasa na honest and intellectual debate ! ! !

Wewe nae usomi wako Una Shaka!!!!

Elimu ni uwezo sio cheti wala makaratasi.....

Wangapi wanaandikiwa hizo paper?? yaani kwa ujanja wako wote unapima akili ya MTU kwa paper??
 
Ben Saanane sio lazima kuchalange uprofesa wake kwa paper tuu hata kwa hoja zake pia zinaweza kuleta mjadala. Mfano ile hoja yake kuhusu tafiti ya TWAWEZA na kauli za wanasiasa, ilikuwa ni tata na imeleta mshangao wa jee ni kweli mamlaka iliyomtunuku iliangalia uawezo wake au kulikuwa na jingine katika kipindi hiki kilichosukuma yeye kutunukiwa haraka haraka.
Huo ni mfano mmoja tuu wa hoja zake tata.
 
Last edited by a moderator:
paper ambazo tutamuhukumu nazo ni makala zake kwenye magazeti yaani huyu prof. anaandika utumbo hata mtoto wa form one hawezi andika,amepotea au niseme amepagawa
Wakuu unajua wakati mwingine......Haya,hebu mwenye Paper yoyote ambayo Kitila ameandika alete hapa halafu tuijadili hiyo Paper badala ya kumjadili yeye kama yeye maana Uprofesa wa mtu unajadiliwa kwa ku-challenge paper yake kwa hoja na yeye aje aitetee

Tuwe sasa na honest and intellectual debate ! ! !
 
Mtu msomi anategemewa awe na michango chanya kwenye jamii,atoe mawazo ya kuisadia jamii na si hizi pumba ambazo hata mie niliyeishia form two nazing'amua!
 
Anayumba baada ya kutoswa CHADEMA bila kutarajia-alijona think tank ya chama.
Ninaposikia neno Profesa Tanzania napata kichefychefu. Kwangu Profesa wa Tanzania ni sawa na ebola. Sijui elimu yetu imekuwaje, ndiyo sababu lile gwiji la Sosholojia, Marehemu Sethi Chachage aliviita vyuo vikuu vya Tanzania, " elevated high schools.!!!'
 
mtu msomi anategemewa awe na michango chanya kwenye jamii,atoe mawazo ya kuisadia jamii na si hizi pumba ambazo hata mie niliyeishia form two nazing'amua!

kumbe ndivyo alivyo. Dah pole le profeseri.
 
mleta hoja umeongea mambo ya jumlajumla bila kusema kiufasaha hasa nini tatizo la prof Kitila
 
ninaposikia neno profesa tanzania napata kichefychefu. Kwangu profesa wa tanzania ni sawa na ebola. Sijui elimu yetu imekuwaje, ndiyo sababu lile gwiji la sosholojia, marehemu sethi chachage aliviita vyuo vikuu vya tanzania, " elevated high schools.!!!'

mkuu huo ndio ukweli kabisa,umemaliza, watu hawataki kuuskia, angalia hapa nchini wasomi wanavyozidi na matataizo yanaongezeka..

Maprof wetu hapa nchini ni shida kabisa, nadhani kuna shida sehemu, maana wengi wao ni wazuri wa kukalili makaratasi na matheory ukija katika maisha yao ni shida tupu. Halafu hao ndio wanakwambia kijana ukajiajiri wakati wao hata banda la kuku hawana wamekaria kuandika makaratasi tu, hakuna lolote. Wewe jiulize hii nchi ina maprof wangapi then relate na mchango wao katika maendeleo ya taifa hili.

Mimi ntabaki na kielemu changu hiki kidogo tu hiki as far naweza kufanya kilimo changu cha kisasa na navuna vya kutosha na nayamudu maisha inatosha sana. Hawa maprof wakishastaafu ndio wanaanza ufugaji wa kuku waki na stress mpaka basi... Elimu yetu ni shida, niliwahi kufanya kazi shirika mmoja na watu wanamasters lakini tulikuwa katika utendaji wa miradi yetu ilikuwa ni shida sana kuelewa hawa watu wanamasters kweli hata tukiandaa riport za miradi yetu hadi bodi ya wakurugrnzi walikuwa wakiwashaangaa hao wenye masters walikuwa wakihoji inakuwaje riport inakosa hata recommendation, umeshindwa kutimiza objectives 1,2... Hakuna sababu zozote wala way forwad, tangu hapo nikasema hizi elimu zetu ni kujaza mavyeti tupu... Hakuna lolote.... Wao hao maprof wanakwambia jiajiri wakati wao wenyewe wameajiajiri, heri hata mengi au bakheresa wakiniambia kujiajiri kunalipa ntawaelewa; uprof ni jina tu kama majina mengina kama ulevi, au ujambazi.,...

Wewe nae usomi wako Una Shaka!!!!

Elimu ni uwezo sio cheti wala makaratasi.....

Wangapi wanaandikiwa hizo paper?? yaani kwa ujanja wako wote unapima akili ya MTU kwa paper??

Sasa uprofesa wa mtu si unau-challenge huko kwenye journals huko.Yaani nisipokubaliana na hoja yako nitakua na elimu ya mashaka?

Kwako wewe and the likes ni kuwa wale waumini wa "Group thinking " na "Bandwagoning" elimu yao ipo juu au ndio ma-genius.

Au ndio wale wale wenye phobia na elimu kiasi kwamba ukisikia huyu ana cheti cha Kidato cha nne wakati wewe huna unaanza kumchukia.Kuna tabia mbaya sana imeibuka siku hizi na italigharimu taifa ile ya kuaminisha watu kuwa elimu siyo kitu kabisa.

My brother ,wake up! Hakuna taifa litakalojengwa bila kuwekeza kwenye elimu bora ya watu wake.

Pia msomi hatakiwi kujenga hoja za kisayansi kwa kufuata hisia za watu au mihemko vinginevyo tutakua na wasomi watakaoendelea kutulisha takwimu za uongo tu kama wale wanaodanganya kuwa uchumi unakua.Kuna matusi umeandika hapo juu ingawa hujui kuwa ni matusi....

Anyways,I think i should ignore you to avoid the escalation of your vituperation.
 
we dada hebu nyoosha maelezo tatizo hasa la Prof Kitila ni lipi? na linaondoje uhalali wa yeye kuwa Prof?
Au kwa sababu Mnapenda kusikia vinavyowafurahisha tu? hamtaki kisikia msivyovipenda hata kama ndio ukweli wenyewe!!
 
Sasa uprofesa wa mtu si unau-challenge huko kwenye journals huko.Yaani nisipokubaliana na hoja yako nitakua na elimu ya mashaka?

Kwako wewe and the likes ni kuwa wale waumini wa "Group thinking " na "Bandwagoning" elimu yao ipo juu au ndio ma-genius.

Au ndio wale wale wenye phobia na elimu kiasi kwamba ukisikia huyu ana cheti cha Kidato cha nne wakati wewe huna unaanza kumchukia.Kuna tabia mbaya sana imeibuka siku hizi na italigharimu taifa ile ya kuaminisha watu kuwa elimu siyo kitu kabisa.

My brother ,wake up! Hakuna taifa litakalojengwa bila kuwekeza kwenye elimu bora ya watu wake.

Pia msomi hatakiwi kujenga hoja za kisayansi kwa kufuata hisia za watu au mihemko vinginevyo tutakua na wasomi watakaoendelea kutulisha takwimu za uongo tu kama wale wanaodanganya kuwa uchumi unakua.Kuna matusi umeandika hapo juu ingawa hujui kuwa ni matusi....

Anyways,I think i should ignore you to avoid the escalation of your vituperation.

Usilete porojo kijana hapo umejibu off point....

Kuwa ignored na wewe kwangu is not an issue....

Nimekuuliza kisomi Sana elimu ya MTU inapimwa kwenye makaratasi au uwezo wake?

Yaani nikitaka kupima uwezo Wa professor Maghembe inanibidi nikaangalie paper alizoandika??

Kuna anaepata u professor bila kuandika papers?

Je kuna anae andika paper dhaifu akapewa u professor??

Je wote wanao present academic papers ni za kwao? Wameandika wao? Kama ndiyo vipi walionyang'anywa hilo daraja kwa kuwasilisha paper ambazo ama waliiba... Waliandikiwa au kunakili kwa wenzao??

Kukushangaa ndo ionekane phobia??

Wangapi wamescore madaraja ya juu kwenye karatasi lakini practice ya kwenye hayo makaratasi imewashinda ktk real life??

Msomi mzima unakuja hapa kusema ati tukitaka kujua thamani ya u professor wake tusome paper zake?

Nikuulize swali wangapi wanaweza kwenda soma hizo papers ktk jamii? Je wangapi wanaweza ona mchango wake ktk jamii??

Njia nzuri ni IPI?? Kutumia elimu yako kwa faida ya watu na watu waithaminishe elimu yako kwa matokeo chanya ktk jamii..

Au utembee na papers ili watu waupime usomi wako na thamani yake?

Unakimbilia kutoa maelezo marefu yasiyo na tija nyie ndo wale mkipewa challenges mnakimbilia kusema wivu wivu Mara kijicho bila hoja...

Elimu ni uwezo sio cheti...

Thamani ya elimu haipimwi kwenye vyeti Bali kwa kuitumia ili ilete matokeo chanya kwenye jamii inayotuzunguka....

Rejea machapicho ya J. K. Nyerere juu ya education for self reliance.....
 
Tanzania ilipata kuwa na Professor mmoja tuu wa ukweli,nae si Mwingine bali ni Professor Philemoni Sarungi pekee hao wengine sijui Muhongo,Kapuya,Maghembe,Tibaijuka,Mkumbo ni uchwara a.k.a wachumia tumbo wapo kundi moja na Professor Maji Marefu.
 
Back
Top Bottom