figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Staa wa Hip Hop na Mbunge wa Mikumi, Joseph ‘Professor jay’ Haule, wiki hii anatarajia kuachia wimbo wake mpya aliyochanganya mahadhi ya Hip Hop na Singeli aliyomshirikisha Shollo Mwamba.
Akizungumza na ripota wa Timesfm.co.tz, Jay, amesema wimbo huo unaitwa kazi kazi ukiwa na lengo la kuwahamasisha waliokata tamaa kuamini kuwa kila kitu kinawezekana ukifanya kazi kwa bidii.
“Ndiyo maana unaitwa kazi kazi na video tumeirekodi kule kule kwenye watu wenye changamoto na waliokata tamaa kuwahamasisha zaidi, uwanja wa fisi, kama kipande kinahitaji m*laya tumewatumia wahuisika kweli.
“Nmechanganya na Singeli ili kuipa sura mpya Singeli, watu wa singeli wanaonekanaga wahuni, muziki wa kihuni sasa nataka tuwasaidie kwa sababu ni aina yetu ya muziki wa hapa nyumbani, tumewatumia wakabaji kweli kwenye video na watu walifurahi kumuona Mbunge ameingia maeneo yao” Amesema.
Wimbo huo umetayarishwa na Mensen Selekta, Video imeongozwa na Kwetu Studio na ‘kazi kazi’ itaachiwa rasmi Ijumaa wiki hii.