Elections 2015 Professor Jay kapita kura za maoni Ubunge Mikumi

chongchung

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
12,056
34,938
TWEET

SHARE

SHARE

COMMENTS


.
Stori ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa mkongwe wa Hip Hop Joseph Haule aka Professor Jay ambaye wiki zilizopita alishinda kura za maoni kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo katika Jimbo la mikumi Morogoro.Sasa leo Agosti 7, 2015 amekutana na ripota wa TZA na kupiga naye stori kuhusiana na mchakato wa kura za maoni jinsi ulivyofanyika.
.
‘Namshukuru Mungu kura za maoni zimeenda vizuri, niwapongezi tu watu wa CHADEMA kwa kutimiza demokrasia na tuliweza kupga kura na nimeweza kuibuka mshindi baada ya kupata kura 240 n Mpinzani wangu DR. Salvatory Makweta 18, Brendan Maro 15, Mkumbata 5 lakini niseme kwamba ule ushindi sio kuonesha Jay ameshinda au anajua sana nawashukuru sana watia nia wote walikuwa wana nguvu na wote walikuwa na uwezo’- Professor Jay
.
‘Baada ya kushinda kura za maoni nimepita kuwashukuru wananchi kwa kunichagua wajua wa kamati kuu zile za kata lakini pia nimewaomba watia nia wenzangu wahusike moja kwa moja kwenye hizi kampeni na kwa moyo wamekubali na ndio wataendeza kampeni zangu kwasababu naamini kupitia elimu zao kila kitu kitaenda sawa’ – Professor Jay
.
‘Pamoja nimechaguliwa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Mikumi kazi zangu za Muziki nitaendelea kuufanya kwasababu muziki ndio maisha yangu na nitakufa nikiendelea kufanya muziki ila nitakuwa sifanya kwa mashindano bali muziki wangu utakuwa wa Level juu kwa hiyo nitakuwa nafanya mara chache kwa level ya juu zaidi, mashabiki wangu watambue kuwa nipo kwaajili yao na sitawangusha’ – Professor Jay



 
Hivi ile hafla ya juzi ya wasanii kumuaga JK alialikwa? Maana Prof. J ni moja ya wasanii wakongwe na walioiweka Bongo flava kwenye ramani ya Tz.
 
Wewe Ni Msanii Ninaekukubali Toka Zama Za Utoto Wangu Nilikuwa Ninauwezo Wa Kuimba Nyimbo Zako Mwanzo Mpaka Mwisho Sasa Ndio Nakukubali Mwanzo Mwisho

kura "240" wakati hawa wenzetu anaeshinda kura za maoni unakuta amevuta mpaka kura "20,000",,, hii ina maana gani??
 
Ccm wanapiga wananchi wooooote hadi wanachama wa Chadema,unapewa kadi na mtu wakumchaguwa unaambiwa na unapewa na kitu kidogo aka takirima,unapiga kura yako ukimaliza ruksa kuchana kadi.chadema ni wajumbe tu na viongozi wa chama
Kata na mitaaaa.
 
Back
Top Bottom