Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Tathmini ya utekelezaji wa mipango mitatu ya maendeleo ya miaka mitano imebaini mafanikio makubwa ya kiuchumi yaliyopatikana kupitia Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu (LTPP) 2025, hususan kuongezeka kwa pato la mtu mmoja mmoja.
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu, Februari 2, 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 6.2 kwa kipindi cha miaka 20 mfululizo kati ya mwaka 2002 na 2024, huku mfumuko wa bei ukiendelea kudhibitiwa ndani ya wigo wa asilimia 3 hadi 5.
Amesema mafanikio hayo yamechochea kuongezeka kwa wastani wa pato la mtu mmoja kutoka dola za Marekani 453 mwaka 2000 hadi kufikia dola 1,277 mwaka 2024. Aidha, kiwango cha umaskini kimepungua kutoka wastani wa asilimia 36 mwaka 2000 hadi asilimia 26 mwaka 2022.
Kutokana na mafanikio hayo, Tanzania ilifikia hadhi ya uchumi wa pato la kati la chini (Lower Middle Income Country) mwaka 2020 baada ya kufikia wastani wa pato la mtu mmoja la Dola.