Profesa Mkenda, shule za msingi hazina Walimu

Darren2019

JF-Expert Member
Nov 23, 2019
1,112
2,379
Kumekuwa na majadiliano mengi kuhusu elimu yetu, madhaifu yake na changamoto mbalimbali.

Licha ya kwamba kuna hatua mballimbali zinazochukuiiwa va serikali km ujenzi wa madarasa, elimu bila malipo, uboreshaji wa mitaala na kadhalika ila bado serikali haijagusa kiini cha matatizo.

Nimefanikiwa kuzunguka shule za msingi mbalimbali hapa wilayani Karatu mkoa wa Arusha, nlichoshuhudia ni masikitiko matupu.

Shule nyingi zina wanafunzi kwa wastani wa 60 kwa darasa na madarasa 8 yaani awali hadi darasa la 7, idadi ya walimu haizidi 6 kwa shule, kuna shule ina walimu wanne pamoja na Mwl Mkuu.

Hivi kweli tunatarajia kuwakomboa watoto wa maskini wa taifa hili kwa hali hii?

Kama mkoa wa Arusha uko hivi vipi huko Katavi, Kigoma na Mtwara?

Ndg zangu kama Mungu kakubariki kipato mpeleke mwanao shule binafsi tu, huku serikalini ni majanga matupu na angalau sekondari ila primary walimu ni hakuna.

Waziri wa elimu kilio hiki kikufikie.
 
Watoto wa walalahoi wapo tele mashuleni wanajitolea kuwasaidia wadogo zao hawalipwi kabisa ila.ajira ikitoka wanaajiri watoto wao na wajukuu hii NI aibu kwa serikali kwa kweli
 
Watoto wa walalahoi wapo tele mashuleni wanajitolea kuwasaidia wadogo zao hawalipwi kabisa ila.ajira ikitoka wanaajiri watoto wao na wajukuu hii NI aibu kwa serikali kwa kweli

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
Mkuu jana machozi yamenitoka kwa kweli, kuna shule nimefika iko mjini kabisa, kulikuwa na kikao cha wazazi na walimu, yaani kuna mwl mkuu na walimu watatu, ebu fikiria walimu watatu wafundshe awali mpaka drs la 7 na masomo yote kutwa kila siku, afu viongozi wako bize kuagiza mashangingi
 
Inasikitisha shule ina walimu 5. kuna darasa la Awali hadi la saba

Mwalimu mmoja anafundisha masomo hadi 12.
 
Inasikitisha shule ina walimu 5. kuna darasa la Awali hadi la saba

Mwalimu mmoja anafundisha masomo hadi 12.
Afu tunalalama ooh sijui mitaala sijui nini, afu nlichogundua idadi kubwa ya walimu wa primary wamestaafu miaka hii ya usoni ambapo serikali nayo imesuasua kuajiri, hali ni mbaya wakuu watoto wanaenda kucheza tu.
 
Aisee, hili ni kweli hasa walimu wa primary hakuna kabisa, Yani afadhali sekondary, Kuna shule zinasikitisha hasa za msingi.
Nilikuwa Komdoa Kijiji kinaitwa Hachwi kunashule Shikizi lakini haina walimu hata mmoja, kuna mwalimu anayejitolea muhitimu wa Darasa la Saba, wazazi wanalipa 1000 kila mwezi anafundisha darasa la 3,4
 
Unajua kitu ambacho sielewi kuhusu jamii ya mtanzania ni kuamini kuwa kujenga madarasa ndio hatua ya kwanza ya kuboresha elimu.

Kujenga madarasa ni hatua ya mwisho katika kuboresha elimu. Hatua ya kwanza ni kuwa na mfumo mzuri kuanzia uboreshani wa mtaala na mbinu za ufundishaji, masilahi ya walimu wanapikuwa kazini, ubora wa walimu wenyewe.

Haya yakipewa kipaumbele hata watu wakisomea kwenye mabanda yatayoezekwa na mabati au makuti watatoka wakiwa ni best students.

Ila hii ya kujenga madarasa ni kuwapa hawa wanasiasa matapeli mbinu za kurubuni raia na kujifanya wanafanya jitihada huku kiuhalisia ni upotezaji wa pesa za walipa kodi na misaada kila mwaka huku matokeo yake ni kuzalisha wasomi zero brain wasio na maarifa hata kidogo.

Maendeleo ni jambo mtambuka na halizuiliki. Maendeleo yanataka utayari na spirit ya kujitoa kuyatafuta. Huwezi force maendeleo huku ukiwa busy na mizaha ya kisiasa ili ujipatie kipato cha kuishi na familia yako kwa kula kula posho, mshahara mnene, na kujiwekea ulinzi kupitia sheria kandamizi.

Changamoto sasa zinaanza kujidhihirisha wazi wazi. Taifa linafeli na raia tumeshashtuka. Mimi ningekuwa ni hawa viongozi kama akina mzee kinana na makamba.....aaaaaah mapema napiga Bilioni moja yangu nakwenda shamba kujilimia nabakia kuwa mshauri tu na mtoa nasaha kwa niaba ya raia.

Ila hii kutaka uishi kwa kupiga madili kila siku ya mamilioni na uishi kwa dhuruma ya kuchomoa vihela vya miradi ya serikali wanayowaletea raia wa kipato cha chini ni kujitafutia laana tu uzeeni.

Muda kweli huwa unakuja na majibu. CCM hili jumba bovu litawaangukia. Wale watoto mliokuwa mnasema ni taifa la kesho wameshakuwa madingi sasa na hamtaki kuwaachia walitumikie taifa lao. Hivi mnadhani watawaacha muwadhurumu na watoto na wajukuu zao?!

Muda mizaha michezo umekwisha fikia tamati. Ni muda muafaka sasa wa kujitafakari na kutafuta njia salama ya kuachia wanaoweza washike usukani tujenge taifa hili ninyi hii kazi imewashinda period michezo ni mingi sana hampo serious.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumekuwa na majadiliano mengi kuhusu elimu yetu, madhaifu yake na changamoto mbalimbali.

Licha ya kwamba kuna hatua mballimbali zinazochukuiiwa va serikali km ujenzi wa madarasa, elimu bila malipo, uboreshaji wa mitaala na kadhalika ila bado serikali haijagusa kiini cha matatizo.

Nimefanikiwa kuzunguka shule za msingi mbalimbali hapa wilayani Karatu mkoa wa Arusha, nlichoshuhudia ni masikitiko matupu.

Shule nyingi zina wanafunzi kwa wastani wa 60 kwa darasa na madarasa 8 yaani awali hadi darasa la 7, idadi ya walimu haizidi 6 kwa shule, kuna shule ina walimu wanne pamoja na Mwl Mkuu.

Hivi kweli tunatarajia kuwakomboa watoto wa maskini wa taifa hili kwa hali hii?

Kama mkoa wa Arusha uko hivi vipi huko Katavi, Kigoma na Mtwara?

Ndg zangu kama Mungu kakubariki kipato mpeleke mwanao shule binafsi tu, huku serikalini ni majanga matupu na angalau sekondari ila primary walimu ni hakuna.

Waziri wa elimu kilio hiki kikufikie.
Waalimu hawatoshi kwa sababu mpaka wawasomeshe watoto,na vitukuu vyao ndo waajiri kufundisha watoto wetu ndo maana ajira kwa waalimu hakuna
 
Mkuu jana machozi yamenitoka kwa kweli, kuna shule nimefika iko mjini kabisa, kulikuwa na kikao cha wazazi na walimu, yaani kuna mwl mkuu na walimu watatu, ebu fikiria walimu watatu wafundshe awali mpaka drs la 7 na masomo yote kutwa kila siku, afu viongozi wako bize kuagiza mashangingi
Hiyo mbona hata hapa kwetu shida ni waalimu,vyoo,na madawati watoto wetu wakaa chini
 
Matokeo ya sensa yakitangazwa kwa uwazi labda wanasiasa watashtuka kuweka mipango ya badae.

Namanisha, idadi ya wanafunzi na watoto wanaotarajia kujiunga na shule za msingi ni kubwa sana kuliko nguvu kazi ya walimu hasa katika shule za msingi.
 
Mkuu jana machozi yamenitoka kwa kweli, kuna shule nimefika iko mjini kabisa, kulikuwa na kikao cha wazazi na walimu, yaani kuna mwl mkuu na walimu watatu, ebu fikiria walimu watatu wafundshe awali mpaka drs la 7 na masomo yote kutwa kila siku, afu viongozi wako bize kuagiza mashangingi

Kwa kweli sijui tumelogwa na nani
 
KARIBU VUNJA BEI WORKSHOP GOBAA
IMG_20220826_194316.jpg
 
Back
Top Bottom