Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, profesa Sifuni Mchome, aliweka hadharani muundo mpya wa upangaji wa madaraja ambapo alitangaza kufuta daraja la sifuri na kuanzisha daraja la tano.
Baadaye aliibuka Naibu Waziri wa Elimu,Philip Mulugo na kumkana Prof Mchome--kwamba ni muongo--hayo madaraja amejitungia mwenyewe akiwa na mkewe nyumbani kwake, kwa hiyo hakuna kitu kama hicho kilichotangazwa na Profesa!
Mh. William Lukuvi alimtetea vikali sana Mulugo (Serikali) kwamba yuko sahihi na kuonya kuwa Prof Mchome (Raia) ni muongo mkubwa! Lukuvi aliwataka wananchi wamuamini Mulugo kwa kuwa yeye ni Serikali tofauti na Prof Mchome ambaye ni raia wa kawaida. Hii inaleta picha kwamba madaraja mapya yaliyotangazwa na Prof Mchome ni mawazo yake binafsi na hayajawahi kujadiliwa na mtu yeyote ndani ya Wizara ya Elimu.
Kufuatia sintofahamu na kizungumkuti hiki, Profesa Mchome anapaswa kuachia ngazi kwa kulitangazia Taifa uongo kwa sababu anazozijua yeye. Yaani Profesa huyu aketi nyumbani na mkewe waamue kutunga madaraja mapya ya ufaulu na kuutangazia umma wa watanzania kinyume cha sheria halafu aachwe aendelee kuongoza wizara hii nyeti? Haiwezekani hata kidogo-- anapaswa kuachia ngazi mara moja.
Hatuwezi kukubali kuona Wizara ya Elimu ikiongozwa na profesa uchwara kama huyu Mchome.
Kwa serikali hii ya ccm usitegemee kitu kama hicho hii ni serikali kipofu, mambo kama hayo ya kufutwa kazi kwa mtu anayeboronga kazi au kuwajibiga utayaona kuanzia 2015 baada ya chadema kuongoza nchi. hapo ndipo patakuwa na kilio na kusaga menoWiki iliyopita Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, profesa Sifuni Mchome, aliweka hadharani muundo mpya wa upangaji wa madaraja ambapo alitangaza kufuta daraja la sifuri na kuanzisha daraja la tano.
Hatuwezi kukubali kuona Wizara ya Elimu ikiongozwa na profesa uchwara kama huyu Mchome.
Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, profesa Sifuni Mchome, aliweka hadharani muundo mpya wa upangaji wa madaraja ambapo alitangaza kufuta daraja la sifuri na kuanzisha daraja la tano.
Baadaye aliibuka Naibu Waziri wa Elimu,Philip Mulugo na kumkana Prof Mchome--kwamba ni muongo--hayo madaraja amejitungia mwenyewe akiwa na mkewe nyumbani kwake, kwa hiyo hakuna kitu kama hicho kilichotangazwa na Profesa!
Mh. William Lukuvi alimtetea vikali sana Mulugo (Serikali) kwamba yuko sahihi na kuonya kuwa Prof Mchome (Raia) ni muongo mkubwa! Lukuvi aliwataka wananchi wamuamini Mulugo kwa kuwa yeye ni Serikali tofauti na Prof Mchome ambaye ni raia wa kawaida. Hii inaleta picha kwamba madaraja mapya yaliyotangazwa na Prof Mchome ni mawazo yake binafsi na hayajawahi kujadiliwa na mtu yeyote ndani ya Wizara ya Elimu.
Kufuatia sintofahamu na kizungumkuti hiki, Profesa Mchome anapaswa kuachia ngazi kwa kulitangazia Taifa uongo kwa sababu anazozijua yeye. Yaani Profesa huyu aketi nyumbani na mkewe waamue kutunga madaraja mapya ya ufaulu na kuutangazia umma wa watanzania kinyume cha sheria halafu aachwe aendelee kuongoza wizara hii nyeti? Haiwezekani hata kidogo-- anapaswa kuachia ngazi mara moja.
Hatuwezi kukubali kuona Wizara ya Elimu ikiongozwa na profesa uchwara kama huyu Mchome.
mkuu mimi sioni mahali ambapo Lukuvi na Mlugo wameshinda badala yake naona utendaji mbovu usokuwa na tija na tena hauleti maana katika jamii.Kilichofanyika hapo ni Mulugo na Lukuvi kutaka 'kuokoa' jahazi baada ya kuona reaction ya watu kutokana na mfumo mpya uliotangazwa na katibu mkuu mchome.
Itakumbukwa kuwa mchome ndiye aliyeongoza tume ya iliyooundwa na waziri mkuu kuchunguza chanzo cha wanafunzi kutokufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana. Hata hivyo, ripoti ya tume hiyo haijawahi kutolewa hadharani, bali serikali imekuwa ikitumia baadhi ya vipengele vya ripoti hiyo kufanya maamuzi kama vile ilivyoamua kufuta matokeo ya kidato cha nne 2012 na kuagiza necta ipange upya. Itakumbukwa pia kuwa mmoja wa wajumbe wa tume hiyo aliamua kujiudhuru akilalamikia 'uchakachuaji' uliofanywa kwenye ripoti hasa baada ya kuona yanayotekelezwa si yale waliyokubaliana kwenye tume.
Cha kushangaza zaidi, ni pale mwenyekiti wa tume alipoteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara ili atekeleze yale aliyoyachunguza mwenyewe, au yale 'waliyochakachua'. Na sasa tumeona alivyoanza utelezaji rasmi ya ripoti yake. Kwa kifupi, mchome alitumiwa na wanasiasa na yeye akakubali kuuza 'weledi' wake kwa matakwa ya wanasiasa na kukubali kuficha ukweli. Hata hivyo alisahau kuwa, wanasiasa ni wanasiasa na sio wa kuamini muda wote maana hubadilika kulingana na upepo. Na siku sio nyingi tangu akibali kutumikia matakwa ya wanasiasa, tayari ukweli huu umeanza kudhihirika, kwa Lukuvi kumkana kuwa kauli yake sio kauli ya serikali, bali kauli ya Mulugo ndio kauli ya serikali.
Nilichojifunza, na ninachoendelea kujifunza ni kwa wasomi na watalaam mbalimbali kuwa waangalifu sana wanapodeal na wanasiasa. Wanasiasa wengi ni vigeugeu, hawaaaminiki na wanaweza kukuacha katika hali ya sintonfahamu baada tu ya kufanikisha malengo yao. Katika hili, Lukuvi na Mulugo ni washindi, lakini ni aibu kubwa kwa profesa msomi wa sheria!