Profesa Lipumba ni nahodha anayetoboa meli?

FrediusSnowden

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
269
224
Ukitaja moja kati ya watu mashuhuri katika nyanja ya kiuchumi huwezi kukosa jina la Mtanzania, ndugu Profesa Ibrahimu Lipumba. Ni moja kati ya wasomi nadra sana katika taifa letu na Afrika kwa ujumla kutokana na utashi wake katika masuala ya uchumi, anayesifika kwa kuchambua na kutoa ushauri katika nchi mbalimbali Afrika, Asia, Amerika na Ulaya. Moja kati ya ushauri wake ambao aliutoa juu ya hatari ambazo zinaweza kuipata Uingereza kama ikijitoa katika Umoja wa Ulaya umempatia umaarufu sana. Alipata kuwa kiongozi wa CUF kama mwenyekiti kwa muda wa miaka ishirini ambapo chama hicho kilikuwa moja kati ya vyama vikuu vya upinzani vikiwa na hoja nzito kwa serikali, na kwa upande wa Zanzibar kuwa mwiba mkali kwa CCM, ambapo jambo hilo lilipelekea kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Watanzania watakumbuka kuwa Profesa Lipumba alikuwa ni moja kati ya wanasiasa waliokuwa tishio kwa upandae wa upinzani, kwa sera na hoja mbalimbali hasa wakati wa kampeni, alijenga heshima kubwa kwa ujumla. Nilipokuwa niko mkoani Lindi kwaajili ya kusaidia wanawake wasiojiweza katika kampuni yetu (jina nalihifadhi) mwaka juzi 2014 nilizungumza na mama mmoja wa makamo ambaye alikuwa anashauri Profesa apumzike kugombea urais wa jamhuri ya muungano. Niliingiwa ushawishi wakujua nini hasa hoja ya mama yule; alifafanua kwa mapana mno hadi nikastaajabishwa na uchambuzi wake.

Nilimuuliza kwa nini unataka Profesa apumzike ilihali Maalim aendelee, si wapumzike wote? Mama alijibu kwa kusema, “Mwanangu huelewi siasa za hapa nchini kwa umakini nadhani kwa sababu wewe ni mgeni lakini wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 sisi watu wa Zenji tulimlaumu Maalim kuwa msaliti kama unakumbuka hasa wakina mama tulikuwa mstari wa mbele sana, nikiwemo mimi binafsi (anafikicha macho yake kisha anatema mate), mwanangu Mungu anisamehe kwani sikujua kwanini hali ile ilikuwa vile.” Namuuliza hali ipi mama? Anasema, “Lipumba alimzunguka Maalim na kupandikiza chuki dhidi yake, na bahati nzuri ni kuwa Maalim ni mtu wa watu mzee yule akagundua juu ya usaliti ila nadhani alikaa kimya na yeye akajua kuwa sasa lazima awe ngangari chama kisife.”

Kwa kuwa nilikuwa kikazi nikaona ni bora nisiendelee na mjadala ule mbao wafanyakazi wenzangu wanaweza kunifikiria vibaya. Nikaagana na mama yule maisha yakasonga mbele. Profesa alikuwa kama mmoja wa viongozi ndani ya UKAWA. Ilipata kusikika kuwa UKAWA itakufa maneno ambayo yalikuwa yanasemwa na baadhi ya viongozi wa CCM na wanachama wao, kumbe walikuwa wajua kuwa wana pandikizi lao! Inahuzunisha kama kweli Profesa ndivyo kama watu wanavyodhani “shushushu” ambaye ni “double agent”.

Kudhaniwa kuwa ni agent mpelelezi mwenye wajibu wa kukiua chama cha wananchi CUF haitiliwi shaka tangu wakati katibu wake alipomtilia shaka kwa kuwa alikuwa ni kinyume na mambo mengi ambayo kama chama walikuwa wanakubaliana. Haingii akilini kwa msomi kukuliana jambo na halafu baadaye unageuka kwa kusema hukusema hivyo au hamkukubaliana hivyo. Wakati wa mchakato wa kumpitisha Mh. Lowassa kuwa mgombea, Profesa alikuwepo na alitoa ushauri wa kupokelewa kwake CHADEMA, hadi hatua za mwisho kabisa Profesa aliuwepo, hamadi akaibuka kujitoa ili UKAWA isambaratike! “ajabu sana”, UKAWA haikusambaratika. Inasemekana kuwa alipewa fedha nyingi sana kwa kucheza ile deal. Ngoma ambayo aliicheza baada ya mwenzake aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA kucheza ngoma hiyohiyo.

Kipindi cha nyuma kidogo baada ya tukio lile profesa alicheza karata ambayo wana intelijensia wa siasa wanaita matured act kwa kuvaa mwamvuli wa kuandamana na kushikwa na polisi, na kupigwa virungu (mchezo ambayo polisi wa kawaida hawakuielewa vizuri kwani ilikuwa too huge for them to understand, pia kwa watanzania na viongozi wengine wa upinzani) ili kufumbua macho ni kwamba tujiulize ukubwa wa maandamano yale na muda mpaka yanatokea utagundua kuwa ni muda mfupi mno kwa jambo kubwa kama lile kufanyika na kwanini yeye ndiye awe main act. Ilikuwa ni mbinu ya kujenga attention kwake kwa wakati ule ili aweze kuishika UKAWA (seeking for crown, bloody intellectual strategies ) kesi ile hadi leo haijulikani ilipo. Ukiangalia matukio yake ni vyema pia ukumbuke kuwa yeye ni profesa elimu ya juu inatumika.

Upingaji wa hoja za msingi na marudio ya mada moja kwa muda mrefu ilikuwa ni moja kati ya mambo ambayo waliokuwa wanaangalia kwa pembeni kuingiliwa na hofu na shaka kwa umoja huu kuwepo hadi leo hii. Baadhi yaa viongozi walipata kusikika wakisema kuwa kuna majadiliano makubwa mno na ubishanaji mkali juu ya kuufanikisha UKAWA. Ilionekana kuwa watu wawili walikuwa mwiba dokta na profesa. Kwa wakati ule CCM na vyama shirika vilikuwa vinangojea kwa hamu kubwa sana kusikia kuwa UKAWA imekufa. Naweza sema kuwa Mungu mkubwa haikufa.

Kwa maandishi na hoja za profesa Lipumba kujivua uenyekiti hadi sasa halijatoka moja ya sababu hiyo ni uwepo wa Mh. Lowassa kwenye UKAWA, kurudi kwake kwa gear hii ni wazi kuwa hana nia njema na CUF nitafafanua kama ifuatavyo;
Mosi ni kwamba alikuja wakati kikao kimeanza na shughuli kuendelea akiwa na genge la watu wachache wenye kuleta shari, huku kukiwa na usindikizwaji na afisa mwenye nguo za kiraia (ikumbukwe hawa ndio waliomdhalilisha hapo nyuma na wamemfungulia jalada). Pili alikuwa anajua kuwa jina lake halikuwepo katika wagombea wa uenyekiti kwa nini alikuja kufanya fujo na watu wale pamoja na kuharibu mali zilizokuwepo. Wachambuzi baadhi wametilia shaka watu ambao profesa amekuja nao kwa kuwa na nywele fupi kabisa ( wanausalama) wakionekana kuwa walikuwa na lengo moja la kufanya fujo. Walionekana wazi kuwa ni watu wenye mafunzo ya kupigana au kufanya fujo, wakiwa wanaongea jambo ambalo hawana hakika nalo yaani kuhusu aakidi ya wajumbe wa mkutano.

Kitendo cha profesa kupata kura 17 sawa na asilimia 2.7% ya kura zote ili agombee uenyekiti ni aibu kwake ambapo 97.3% sawa na kura 476 walimpiga nchi asigombee tena nafasi hiyo, jambo hili limemshushia hadhi yake mbele ya jamii na kimataifa pia japo kikao kile kiliahirishwa na alikuwa mwenyekiti wa kikao Ndg Julius Mtatiro. Watanzania wanapaswa kuepuka wanasiasa jamii ya Profesa Ibrahimu Lipumba ambao ni wanausalama wenye lengo la kuuwa demokrasia ya vyama vingi nchini.

Wasalimuni ndugu wote hapo Bongo!
 
kwa hiyo ulitaka aungane na akina lowassa ambaye alikuwa karibu na wafanya biashara akina rostam? hiv nyie watu mnafikiriaga nini? mbona siwaelewi? hamjiulizi kwanini mpaka akina slaa walijiondoa na akina mnyika mpaka kesho wako kimya kuliko zamani?

jaribuni hata kidogo kuwa wazalendo wa nchi sio siko zote kuwa wazalendo wa matumbo yenu tu.
 
Nimefurahi kusikia MH.LIPUNMBA ni mwanausalama asante mkuu.
 
Asante sana mkuu , umeandika yale ambayo Maalim Seif alikuja kuyafahamu baadaye ,

Swali la kujiuliza ni je kabla lipumba hajaingia cuf alikuwa wapi na alifanya nini ? Hii ni HOME WORK kwa Great thinkers wote .

Mungu ibariki Tanzania .
 
kwa hiyo ulitaka aungane na akina lowassa ambaye alikuwa karibu na wafanya biashara akina rostam? hiv nyie watu mnafikiriaga nini? mbona siwaelewi? hamjiulizi kwanini mpaka akina slaa walijiondoa na akina mnyika mpaka kesho wako kimya kuliko zamani?

jaribuni hata kidogo kuwa wazalendo wa nchi sio siko zote kuwa wazalendo wa matumbo yenu tu.
Hao wazalendo wako kwanini uzalendo wao ulikuja baada ya kulipwa mamilioni ya hela ?
 
Erythrocyte najua unampenda sana lowassa. hata mimi nampenda sana tu na tena ni kiongozi mzuri na mfuatiliaji. na bado naamini lowasa angeweza kuwa kiongozi mzuri sana kuliko hata Magufuli kwa nafasi ya urahisi. na magufuli akabaki na kazi yake ya uwaziri ambayo bila kumung'unya maneno ameifanya vizuri na kiasi Fulani kwa ufanisi sana katika miaka 20 aliyokuwa kwenye nafasi hiyo.
Tatizo la lowassa ni hilo tu la ufisadi na hata timu iliyomzunguka ya akina Rostam, karamagi na wengineo ambao kimsingi ni wafanyabiashara. (naamini ninaposema wafanya biashara unanielewa-daima wako after profit).
nyie hapa kutwa kucha mlikuwa mkimtukana lowassa kila siku kuwa ni fisadi. leo hii yuko huko kwenu kabadilika nini? si yuleyule?
tatizo lenu mko kichama, kikanda, kikabila na pengine kidini Zaidi kuliko masilahi mapana ya nchi hii. binafsi nilimnyima lowassa kura yangu sio kwa sababu namuona ni kiongozi mbaya katika utendaji bali kwa sababu ya historia yake na ya watu waliomzunguka katika kuliibia taifa.
na ujue kwamba kukatwa kwa lowassa hakujaanza leo. hayati mwl. nyerere ambaye ni muasisi wataifa hili aliliona mapema ndo maana 1995 akala kichwa.
kuhusu akina Prof. Lipumba na Dr. Slaa kupewa pesa hizo ni porojo tu. hazina tofauti na zile za Mh. Lowassa kuuziwa chama na akina mbowe na genge lake.
 
Asante sana mkuu , umeandika yale ambayo Maalim Seif alikuja kuyafahamu baadaye ,

Swali la kujiuliza ni je kabla lipumba hajaingia cuf alikuwa wapi na alifanya nini ? Hii ni HOME WORK kwa Great thinkers wote .

Mungu ibariki Tanzania .
CV yake ipo humu. itafute acha uvivu.
 
Ukitaja moja kati ya watu mashuhuri katika nyanja ya kiuchumi huwezi kukosa jina la Mtanzania, ndugu Profesa Ibrahimu Lipumba. Ni moja kati ya wasomi nadra sana katika taifa letu na Afrika kwa ujumla kutokana na utashi wake katika masuala ya uchumi, anayesifika kwa kuchambua na kutoa ushauri katika nchi mbalimbali Afrika, Asia, Amerika na Ulaya. Moja kati ya ushauri wake ambao aliutoa juu ya hatari ambazo zinaweza kuipata Uingereza kama ikijitoa katika Umoja wa Ulaya umempatia umaarufu sana. Alipata kuwa kiongozi wa CUF kama mwenyekiti kwa muda wa miaka ishirini ambapo chama hicho kilikuwa moja kati ya vyama vikuu vya upinzani vikiwa na hoja nzito kwa serikali, na kwa upande wa Zanzibar kuwa mwiba mkali kwa CCM, ambapo jambo hilo lilipelekea kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Watanzania watakumbuka kuwa Profesa Lipumba alikuwa ni moja kati ya wanasiasa waliokuwa tishio kwa upandae wa upinzani, kwa sera na hoja mbalimbali hasa wakati wa kampeni, alijenga heshima kubwa kwa ujumla. Nilipokuwa niko mkoani Lindi kwaajili ya kusaidia wanawake wasiojiweza katika kampuni yetu (jina nalihifadhi) mwaka juzi 2014 nilizungumza na mama mmoja wa makamo ambaye alikuwa anashauri Profesa apumzike kugombea urais wa jamhuri ya muungano. Niliingiwa ushawishi wakujua nini hasa hoja ya mama yule; alifafanua kwa mapana mno hadi nikastaajabishwa na uchambuzi wake.

Nilimuuliza kwa nini unataka Profesa apumzike ilihali Maalim aendelee, si wapumzike wote? Mama alijibu kwa kusema, “Mwanangu huelewi siasa za hapa nchini kwa umakini nadhani kwa sababu wewe ni mgeni lakini wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 sisi watu wa Zenji tulimlaumu Maalim kuwa msaliti kama unakumbuka hasa wakina mama tulikuwa mstari wa mbele sana, nikiwemo mimi binafsi (anafikicha macho yake kisha anatema mate), mwanangu Mungu anisamehe kwani sikujua kwanini hali ile ilikuwa vile.” Namuuliza hali ipi mama? Anasema, “Lipumba alimzunguka Maalim na kupandikiza chuki dhidi yake, na bahati nzuri ni kuwa Maalim ni mtu wa watu mzee yule akagundua juu ya usaliti ila nadhani alikaa kimya na yeye akajua kuwa sasa lazima awe ngangari chama kisife.”

Kwa kuwa nilikuwa kikazi nikaona ni bora nisiendelee na mjadala ule mbao wafanyakazi wenzangu wanaweza kunifikiria vibaya. Nikaagana na mama yule maisha yakasonga mbele. Profesa alikuwa kama mmoja wa viongozi ndani ya UKAWA. Ilipata kusikika kuwa UKAWA itakufa maneno ambayo yalikuwa yanasemwa na baadhi ya viongozi wa CCM na wanachama wao, kumbe walikuwa wajua kuwa wana pandikizi lao! Inahuzunisha kama kweli Profesa ndivyo kama watu wanavyodhani “shushushu” ambaye ni “double agent”.

Kudhaniwa kuwa ni agent mpelelezi mwenye wajibu wa kukiua chama cha wananchi CUF haitiliwi shaka tangu wakati katibu wake alipomtilia shaka kwa kuwa alikuwa ni kinyume na mambo mengi ambayo kama chama walikuwa wanakubaliana. Haingii akilini kwa msomi kukuliana jambo na halafu baadaye unageuka kwa kusema hukusema hivyo au hamkukubaliana hivyo. Wakati wa mchakato wa kumpitisha Mh. Lowassa kuwa mgombea, Profesa alikuwepo na alitoa ushauri wa kupokelewa kwake CHADEMA, hadi hatua za mwisho kabisa Profesa aliuwepo, hamadi akaibuka kujitoa ili UKAWA isambaratike! “ajabu sana”, UKAWA haikusambaratika. Inasemekana kuwa alipewa fedha nyingi sana kwa kucheza ile deal. Ngoma ambayo aliicheza baada ya mwenzake aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA kucheza ngoma hiyohiyo.

Kipindi cha nyuma kidogo baada ya tukio lile profesa alicheza karata ambayo wana intelijensia wa siasa wanaita matured act kwa kuvaa mwamvuli wa kuandamana na kushikwa na polisi, na kupigwa virungu (mchezo ambayo polisi wa kawaida hawakuielewa vizuri kwani ilikuwa too huge for them to understand, pia kwa watanzania na viongozi wengine wa upinzani) ili kufumbua macho ni kwamba tujiulize ukubwa wa maandamano yale na muda mpaka yanatokea utagundua kuwa ni muda mfupi mno kwa jambo kubwa kama lile kufanyika na kwanini yeye ndiye awe main act. Ilikuwa ni mbinu ya kujenga attention kwake kwa wakati ule ili aweze kuishika UKAWA (seeking for crown, bloody intellectual strategies ) kesi ile hadi leo haijulikani ilipo. Ukiangalia matukio yake ni vyema pia ukumbuke kuwa yeye ni profesa elimu ya juu inatumika.

Upingaji wa hoja za msingi na marudio ya mada moja kwa muda mrefu ilikuwa ni moja kati ya mambo ambayo waliokuwa wanaangalia kwa pembeni kuingiliwa na hofu na shaka kwa umoja huu kuwepo hadi leo hii. Baadhi yaa viongozi walipata kusikika wakisema kuwa kuna majadiliano makubwa mno na ubishanaji mkali juu ya kuufanikisha UKAWA. Ilionekana kuwa watu wawili walikuwa mwiba dokta na profesa. Kwa wakati ule CCM na vyama shirika vilikuwa vinangojea kwa hamu kubwa sana kusikia kuwa UKAWA imekufa. Naweza sema kuwa Mungu mkubwa haikufa.

Kwa maandishi na hoja za profesa Lipumba kujivua uenyekiti hadi sasa halijatoka moja ya sababu hiyo ni uwepo wa Mh. Lowassa kwenye UKAWA, kurudi kwake kwa gear hii ni wazi kuwa hana nia njema na CUF nitafafanua kama ifuatavyo;
Mosi ni kwamba alikuja wakati kikao kimeanza na shughuli kuendelea akiwa na genge la watu wachache wenye kuleta shari, huku kukiwa na usindikizwaji na afisa mwenye nguo za kiraia (ikumbukwe hawa ndio waliomdhalilisha hapo nyuma na wamemfungulia jalada). Pili alikuwa anajua kuwa jina lake halikuwepo katika wagombea wa uenyekiti kwa nini alikuja kufanya fujo na watu wale pamoja na kuharibu mali zilizokuwepo. Wachambuzi baadhi wametilia shaka watu ambao profesa amekuja nao kwa kuwa na nywele fupi kabisa ( wanausalama) wakionekana kuwa walikuwa na lengo moja la kufanya fujo. Walionekana wazi kuwa ni watu wenye mafunzo ya kupigana au kufanya fujo, wakiwa wanaongea jambo ambalo hawana hakika nalo yaani kuhusu aakidi ya wajumbe wa mkutano.

Kitendo cha profesa kupata kura 17 sawa na asilimia 2.7% ya kura zote ili agombee uenyekiti ni aibu kwake ambapo 97.3% sawa na kura 476 walimpiga nchi asigombee tena nafasi hiyo, jambo hili limemshushia hadhi yake mbele ya jamii na kimataifa pia japo kikao kile kiliahirishwa na alikuwa mwenyekiti wa kikao Ndg Julius Mtatiro. Watanzania wanapaswa kuepuka wanasiasa jamii ya Profesa Ibrahimu Lipumba ambao ni wanausalama wenye lengo la kuuwa demokrasia ya vyama vingi nchini.

Wasalimuni ndugu wote hapo Bongo!
jinsi kulivyo na usaliti katika kizazi hiki tungekuwa hatujapata uhuru sijui kama tungepata maana mkoloni angetununua sana
 
Nafuu Lipumba angekuwa ni nahodha anayendesha meli akiwa ndani ya meli kwa kuwa angeweza kuzama na abiria wake,tatizo Lipumba ni nahodha anayeendesha meli kwa remote wakati yeye akiwa nje meli itakapozama watakao kufa ni abiria yeye ataendelea kuwa salama.
 
Wananchi wenyewe wa nchi Hii wamezidi umbulula, hata uwapiganie ni sawa na kujiumiza Mwenyewe, why don't I look for my own?
 
Erythrocyte najua unampenda sana lowassa. hata mimi nampenda sana tu na tena ni kiongozi mzuri na mfuatiliaji. na bado naamini lowasa angeweza kuwa kiongozi mzuri sana kuliko hata Magufuli kwa nafasi ya urahisi. na magufuli akabaki na kazi yake ya uwaziri ambayo bila kumung'unya maneno ameifanya vizuri na kiasi Fulani kwa ufanisi sana katika miaka 20 aliyokuwa kwenye nafasi hiyo.
Tatizo la lowassa ni hilo tu la ufisadi na hata timu iliyomzunguka ya akina Rostam, karamagi na wengineo ambao kimsingi ni wafanyabiashara. (naamini ninaposema wafanya biashara unanielewa-daima wako after profit).
nyie hapa kutwa kucha mlikuwa mkimtukana lowassa kila siku kuwa ni fisadi. leo hii yuko huko kwenu kabadilika nini? si yuleyule?
tatizo lenu mko kichama, kikanda, kikabila na pengine kidini Zaidi kuliko masilahi mapana ya nchi hii. binafsi nilimnyima lowassa kura yangu sio kwa sababu namuona ni kiongozi mbaya katika utendaji bali kwa sababu ya historia yake na ya watu waliomzunguka katika kuliibia taifa.
na ujue kwamba kukatwa kwa lowassa hakujaanza leo. hayati mwl. nyerere ambaye ni muasisi wataifa hili aliliona mapema ndo maana 1995 akala kichwa.
kuhusu akina Prof. Lipumba na Dr. Slaa kupewa pesa hizo ni porojo tu. hazina tofauti na zile za Mh. Lowassa kuuziwa chama na akina mbowe na genge lake.
Japo umejichanganya kwenye maelezo yako , lakini naomba unitendee haki kwenye jambo moja tu , Naichukia ccm na walio ndani yake , na naipenda Chadema na makamanda wake wote , mimi si mpenzi wa mtu mmoja mmoja .
 
kwa hiyo ulitaka aungane na akina lowassa ambaye alikuwa karibu na wafanya biashara akina rostam? hiv nyie watu mnafikiriaga nini? mbona siwaelewi? hamjiulizi kwanini mpaka akina slaa walijiondoa na akina mnyika mpaka kesho wako kimya kuliko zamani?

jaribuni hata kidogo kuwa wazalendo wa nchi sio siko zote kuwa wazalendo wa matumbo yenu tu.
Lipumba Slaa hawakujiondoa wenyewe bali walinunuliwa na membe adui mkubwa wa Lowasa, cha ajabu mwenzake Slaa pesa zake kawekeza vizuri lakini Lipumba pesa yake alikula na michepuko zikaisha sasa kabuni mladi mpya wa kula pesa za CCM na kwenda kudhoofisha CUF , Uprofesa wa Lipumba kwa sasa umejikita kwenye siasa za maji taka, Taaluma kichwani imeyeyuka amesahau alichosomea kabakia na elimu Dunia kichwani.
 
naona pumba/ushuzi tu humu. ukweli ni kwamba hao ni wazalendo wa kweli wataifa hili. hivi hujiulizi ni kwa nini hata mnyika yupo kimya sana siku hizi? tafakari.
labda nikuulize swali moja tu; hivi unaamini kweli kuwa lowassa aliuziwa chaggadema na mbowe na genge lake?
 
Japo umejichanganya kwenye maelezo yako , lakini naomba unitendee haki kwenye jambo moja tu , Naichukia ccm na walio ndani yake , na naipenda Chadema na makamanda wake wote , mimi si mpenzi wa mtu mmoja mmoja .
swali langu dogo tu kwako; lowassa yule mliyekuwa mkimtukana ccm amebadilika nini akiwa chadema mpaka mnamsifia kwa kiwango cha juu kiasi hiki?
 
Huyu anafaa kuwa Gavana wa Benki kubwa nchini ama pale Hazina atupe uzoefu na kuinua uchumi
 
Back
Top Bottom