Profesa Lipumba kugombea tena urais 2015

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemnadi Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kugombea kwa mara nyingine kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, huku yeye binafsi akitangaza neema kwa Watanzania ya kuwajaza fedha mifukoni.

Katika mkutano wa uzinduzi wa operesheni ya mchakamchaka kuelekea mwaka 2015 uliofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanga cha Ndege Morogoro, viongozi wengi wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, walimnadi Prof Lipumba jukwaani wakidai kuwa bado ni kiongozi anayestahili kugombea wadhifa huo kupitia CUF.

Awali kabla ya kufanyika kwa mkutano huo uliopambwa na shamra shamra za ngoma zilizoanza siku mbili kabla ya uzinduzi huo zikiambatana na baadhi ya wafuasi na wapenzi wa chama hicho kupita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Morogoro wakiperusha bendera, uliingia dosari baada ya kutanguliwa na mvua kubwa iliyokwamisha baadhi ya shughuli na kuchelewa kuanza kwa mkutano huo.

Mvua hiyo ilianza kunyesha Saa 9.40 jioni mara baada ya mabasi madogo takriban 15 yaliyowabeba wanachama, wafuasi na viongozi wa CUF kutoka Dar es Salaam kuwasili katika viwanja vya mkutano,hali ambayo iliwalazimu viongozi wa juu kuanza na zoezi la kufungua matawi ya jumuiya za vijana na jumuiya ya akinamama kabla ya kwenda kuhutubia.

Akizungumza katika mkutano huo, Profesa Lipumba alisema utatifi uliofanywa katika baadhi ya nchi duniani zikiwamo nchi za Brazil na Mexico umebaini kuwa njia nyepesi ya kumuondolea mwananchi umasikini ni kumpatia fedha taslimu.

Prof Lipumba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi,alisema kuwa jambo hilo linawezekana kufanyika nchini kwa kutumia teknolojia ya simu za mikononi na kuwapo kwa vitambulisho vya taifa vinavyotumia alama za vidole kama alama za ulinzi.

Alisema India yenye watu zaidi ya bilioni 1.2 imefanikiwa kutumia vitambulisho vya taifa katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhifadhi na usalama wa fedha zao na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho hivyo vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Mwenyekiti huyo wa CUF alisema chama chake kikipewa ridhaa na Watanzania ya kuongoza nchi kitatumia rasilimali zilizopo nchini za madini, gesi, mafuta, mbuga za hifadhi na maeneo ya utalii kuweza kuboresha miundombinu, lakini kuwapatia fedha taslimu wananchi ikiwa ni njia rahisi ya kupambana na umasikini.

NISHATI YA GESI
Mwenyekiti wa CUF alisema nchi nyingi duniani zilizopata nishati ya gesi na mafuta zimejikuta katika mgogoro mkubwa ikiwa usimamizi wa raslimali hiyo utawanufaisha wachache na kutolea mfano wa Nigeria. Profesa Lipumba alidai kuwa watafiti wamegundua kuwa gesi iliyogunduliwa Mtwara inafuti za ujazo trioni 33, kiwango ambacho kinaweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka 10 na kina uwezo wa kuingizia serikali wastani wa pato la Sh 6.5 bilioni (USD 4 milioni) mpaka Sh 8.1 bilioni (USD5 milioni) kwa mwaka.
 
Hawakati tamaa! Kweli Allah ana mambo yake. Hivi alipata % ngapi last election? Eti naye ni Profesa, hapimi alama Za nyakati! wasomi wa TZ, mhhh
 
Huyu inaonesha hata akichaguliwa kuwa raisi anaweza kukaa madarakani miaka 30 mpaka apinduliwe.
 
Kama raia yoyote prof Lipumba anayo haki ya kugombea urais. Chaajabu ni kipi? He has a very impressive resume and impeccable credentials. He went to Stanford, and I salute him for his outstanding services and expertise during his tenure at World Bank. For those naysers: How many times did Abe Lincoln lose before he won the election to become the US president?
 
Huyu inaonesha hata akichaguliwa kuwa raisi anaweza kukaa madarakani miaka 30 mpaka apinduliwe.
slaa nae na udokta wake wote akigombea tena ntamshangaa sana maana itakua ni dharau kubwa kwa wanachadema kwamba hakuna mwenye akili kama yeye ndani ya chadema!
 
slaa nae na udokta wake wote akigombea tena ntamshangaa sana maana itakua ni dharau kubwa kwa wanachadema kwamba hakuna mwenye akili kama yeye ndani ya chadema!

Acha kuropoka asubuhi asubuhi. Slaa kagombea mara ngapi na huyo Lipumba itakuwa mara ngapi? sitaki kuelezea uwezo wa mwenyekiti wenu "mwenye akili kuliko wote ndani ya CCM" ni kupoteza muda.
 
Mgombea wa KUDUMU wa nafasi ya urais kupitia chama cha wananchi(CUF).
 
Huyu Lipumba aende kwao Ilolangulu akagombee ubalozi wa nyumba 10. Akigombe tena atakuwa mjinga wa kutupwa!
 
Watu wanaongea mengi kwa kukurupuka au kufikili kwa kutumia miguu, hebu wekeni CV za hao wanao tegemewa kugombea hiyo nafasi tuone nani bora? hivi wajuwa kuwa MAALIM SEIF-phD, JUMADUNI-phD, achana na sifa bwerere za uzoefu wa siasa za nchi hii tangu WAHAI WA BABA WA TAIFA. Hii nchi ni yetu sote ukiangalia watu kwa ubaguzi wa KAILA hatufiki na tutakomoka wote kwanini watu wasifikilie sifa na uadilifu badala yake wapo tayari kulipitisha hata kama akiwa FISADI au MZINZI inimradi tu nampenda? kama vipi wekeni WNA CCM, CDM na CUF na CV zao kamili kisha tudiscus sio kuwadhihaki baadhi kama hivi halafu wachangiaji wengi HAWAJUI academicaly waa politicaly wanaye changia hoja yake "TUWE WAADILIFU WATANZANIA TUTAFANIKIWA, SIO MAJUNGU JAMANI"
 
cuf ni lipumba na Lipumba ni cuf. bila Lipumba cuf haina mgombea urais.

........
Na Ashton Balaigwa




Lipumba%2830%29%282%29.jpg


Mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba


Makamu wa kwanza wa rais wa Serikali ya Umoja wa kitaifa ya Zanzibar, Seif Shariff Hamad, amemtangaza Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao.

Aidha CUF imewatangazia neema Watanzania kuwa endapo itachukua madaraka katika uchaguzi huo itawajaza fedha mifukoni ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaondolea umasikini.

Makamu huyo wa kwanza wa rais alisema hayo katika mkutano wa uzinduzi wa oparesheni ya mkachamchaka kuelekea mwaka 2015 (V4C), uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege, manispaa ya Morogoro.

Alisema Profesa Lipumba bado ni kiongozi shupavu anayestahili kugombea wadhifa huo kupitia CUF katika uchaguzi ujao kwakuwa anakubalika ndani ya chama hicho pamoja na kwa wananchi.

Alisema kuwa operesheni za V4C zilizoanza Mei mwaka jana zitaendelea nchi nzima kwa viongozi wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho na wafuasi wake kupita kila kata na wilaya mbalimbali wakihamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho.

Makamu huyo wa Serikali ya umoja wa kitaifa alisema kuwa malengo ya CUF ni kujenga umoja wa kitaifa na kuhakikisha kuwa wananchi wote pasipokujali mwenye nacho na asiyekuwanacho wanapata haki sawa na hizo ndiyo sera za CUF.

Kwa upande wake, Profesa Lipumba, akizungumza katika mkutano huo alisema
utatifi uliofanywa katika baadhi ya nchi duniani zikiwamo nchi za Brazil na Mexico umebaini kuwa njia nyepesi ya kumuondolea mwananchi umasikini ni kumpatia fedha taslimu.

Profesa Lipumba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi, alisema jambo hilo linawezekana kufanyika nchini kwa kutumia teknolojia ya simu za mikononi na kuwapo kwa vitambulisho vya taifa vinavyotumia alama za vidole kama alama za ulinzi.

Alisema chama chake kikipewa ridhaa na watanzania ya kuongoza nchi kitatumia raslimali zilizopo nchini za madini, gesi, mafuta, mbuga za hifadhi na maeneo ya utalii kuboresha miundombinu lakini kuwapatia fedha taslimu wananchi ikiwa ni njia rahisi ya kupambana na umasikini.

Ikiwa Profesa Lipumba atagombea tena mwaka ujao, itakuwa ni mara ya tano kwake kwa kuwa amekuwa akiwania nafasi hiyo tangu mwaka 1995 lakini hajawahi kushinda.
 
Ndugu wana jf sitak kurudia kutaja upuuz alioufanya huyu jamaa hv majuzi ila nachotaka kujua hv 2015 Prf Lipumba atagombania tena urais kwa mara ya tano Mfululizo?? Bila hata aibu Je? Safar hii atakuja na lipi jipya?
NAOMBA KUWASILISHA
 
Maalim Sefu anagombea Zanzibarna yeye anagombea Bara. Katiba inaruhusu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Agombee hata na 2025. Kwake Ruksa kwa sababu Waislamu wanaruhusiwa....Hebu achukue maneno yake akamlishe Cadrinali Pengo kanisani
 
toka mtoto hajazaliwa 95", na 2015 atapiga kura ni LIPUMBA tu anagombea URAIS bado, kwani hakuna mwingine huko CUF...?????!!! :heh:
 
Ndugu wana jf sitak kurudia kutaja upuuz alioufanya huyu jamaa hv majuzi ila nachotaka kujua hv 2015 Prf Lipumba atagombania tena urais kwa mara ya tano Mfululizo?? Bila hata aibu Je? Safar hii atakuja na lipi jipya?
NAOMBA KUWASILISHA

Kwani inakuathiri vipi kama humpi kura yako?
 
Back
Top Bottom