Profesa Lipumba kugombea tena urais 2015

Ndugu wana jf sitak kurudia kutaja upuuz alioufanya huyu jamaa hv majuzi ila nachotaka kujua hv 2015 Prf Lipumba atagombania tena urais kwa mara ya tano Mfululizo?? Bila hata aibu Je? Safar hii atakuja na lipi jipya?
NAOMBA KUWASILISHA


ni mahesabu ya magamba tu.wasomi wengine wanavyoamua kufanya usanii mkubwa hivi ni jambo la kusikitisha sana.profesa anawaambia watanzania kwamba yuko cuf kwa matembezi lakini yeye hasa ni mtu wa umagambani. viongozi na wanachama wa cdm wanapashwa kufanya utafiti wa kujua nani mpinzani na nani siye.serious.
 
Ndugu wana jf sitak kurudia kutaja upuuz alioufanya huyu jamaa hv majuzi ila nachotaka kujua hv 2015 Prf Lipumba atagombania tena urais kwa mara ya tano Mfululizo?? Bila hata aibu Je? Safar hii atakuja na lipi jipya?
NAOMBA KUWASILISHA

Atachukua fomu akipitishwa na chama chake kama kawa anagombea. Ni hilo tu au umetumwa kuleta mengine?

Huyu ni mtaalamu wa uchumi bhana!
 
huyu pandikizi muacheni ila kila kitu kitajulikana na kitawekwa wazi pale ambapo watanzania wataamua kuchagua chaguo lao CDM.
 
Ndugu wana jf sitak kurudia kutaja upuuz alioufanya huyu jamaa hv majuzi ila nachotaka kujua hv 2015 Prf Lipumba atagombania tena urais kwa mara ya tano Mfululizo?? Bila hata aibu Je? Safar hii atakuja na lipi jipya?
NAOMBA KUWASILISHA
Bila shaka atagombea! Role Model wake ni Profesa mwanzake wa Uchumi Abdoulaye Wade; babu mwenye miaka 87 (au zaidi ya hapo). Babu Wade alianza kugombea Urais nchini Senegal mwaka 1978 (consecutively) na miaka ya mwanzao yote alikung'utwa hadi alipokuja kuupata mwaka 2000.
 
Wakristu walisema watashinda kwa maombi, kwa njia ya maombi akina Lipumba wamejikuta wakiropoka misikitini kuwa Mwaka 1995 aligombea ili kuwakilisha waislam, hahaha go to hell
 
Salaam wana JF.nimetafakari sana ju ya umuhimu wa prof lipumba kuwemo bungeni.
1.prof lipumba ana kila sifa ya kuwa mwakilshi wa watu bungen.
2.prof lipumba amekua akitoa mawazo mazuri sana ju ya mustakabali wa nchi yetu,ila kwa kuwa anayatoa nje ya system ni vigumu mno mawazo yake kufanyiwa kazi.tumeona akina tundu lissu,mnyika,lugola,filikunjombe na mbowe wanavyochangamsha bunge kwa kuipa serikali changa moto ju ya utendaji wake na namna ya kuendesha nchi kwa ujumla.
3.pia ni njia nzuri ya kutangaza chama cha wananchi (cuf)pamoja na yy mwenyewe prf lipumba.maana kwa sasa chama cha cuf hakina mbunge machachari a
nayeweza kufikisha mtazamo wa cuf ju ya uendeshaji nchi bungeni.
4.rejea chamacha chadema kimejitangaza sana kupitia bunge hasa pale katibu mkuu wao mh dr slaa alipoibua tuhuma nzito ikiwemo ya EPA,Meremeta,tangold,mafisadi papa 11 (list of shame)na nyingine nyingi zilizo itikisa serikali mpaka kurudisha hela za epa.
Mwisho nataka kukumbusha kua ww umesomeshwa na hela za walipa kodi kwa kufanya hivyo utakua umelipa fadhila kwa taifa lako,kuliko kung'ang'ania urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambao kusema ukweli chama chako hakijajipanga vizuri huku bara iliuweze kushinda .pr lipumba tafuta jimbo tafadhali.nawasilisha.
 
Mkuu ushauri wako ni murwa sana, je atashinda huo ubunge? Maana nasikia jimboni kwake maccm yamejaa na kutamalaki sana, pia je urais atagombea nani?
 
Na Ashton Balaigwa


Lipumba%2830%29%282%29.jpg

Mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba


Makamu wa kwanza wa rais wa Serikali ya Umoja wa kitaifa ya Zanzibar, Seif Shariff Hamad, amemtangaza Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao.

Aidha CUF imewatangazia neema Watanzania kuwa endapo itachukua madaraka katika uchaguzi huo itawajaza fedha mifukoni ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaondolea umasikini.

Makamu huyo wa kwanza wa rais alisema hayo katika mkutano wa uzinduzi wa oparesheni ya mkachamchaka kuelekea mwaka 2015 (V4C), uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege, manispaa ya Morogoro.

Alisema Profesa Lipumba bado ni kiongozi shupavu anayestahili kugombea wadhifa huo kupitia CUF katika uchaguzi ujao kwakuwa anakubalika ndani ya chama hicho pamoja na kwa wananchi.

Alisema kuwa operesheni za V4C zilizoanza Mei mwaka jana zitaendelea nchi nzima kwa viongozi wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho na wafuasi wake kupita kila kata na wilaya mbalimbali wakihamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho.

Makamu huyo wa Serikali ya umoja wa kitaifa alisema kuwa malengo ya CUF ni kujenga umoja wa kitaifa na kuhakikisha kuwa wananchi wote pasipokujali mwenye nacho na asiyekuwanacho wanapata haki sawa na hizo ndiyo sera za CUF.

Kwa upande wake, Profesa Lipumba, akizungumza katika mkutano huo alisema utatifi uliofanywa katika baadhi ya nchi duniani zikiwamo nchi za Brazil na Mexico umebaini kuwa njia nyepesi ya kumuondolea mwananchi umasikini ni kumpatia fedha taslimu.

Profesa Lipumba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi, alisema jambo hilo linawezekana kufanyika nchini kwa kutumia teknolojia ya simu za mikononi na kuwapo kwa vitambulisho vya taifa vinavyotumia alama za vidole kama alama za ulinzi.

Alisema chama chake kikipewa ridhaa na watanzania ya kuongoza nchi kitatumia raslimali zilizopo nchini za madini, gesi, mafuta, mbuga za hifadhi na maeneo ya utalii kuboresha miundombinu lakini kuwapatia fedha taslimu wananchi ikiwa ni njia rahisi ya kupambana na umasikini.

Ikiwa Profesa Lipumba atagombea tena mwaka ujao, itakuwa ni mara ya tano kwake kwa kuwa amekuwa akiwania nafasi hiyo tangu mwaka 1995 lakini hajawahi kushinda.
hata mimi naunga mkono Lipumba kugombea ubunge badala ya urais,napendekeza agombee Tabora mjini
 
Back
Top Bottom