Profesa Anna chupuchupu kukamatwa na PCCB

Bila shaka wewe ni yule mwanae mvaa vimini! Kule SIHA mzungu anatamba kuwabaka wanawake na kuua raia wasiokuwa na hatia, mvomero, kilombero, bagamoyo yote imechukuliwa na ndugu wawekezaji uchwara wa Mamako Anna... Huyo Stahili yake ni Pingu tu! Hakuna jinsi... Kuhusu ajira: unaonekana wewe ni mtumwa wa fikra, unaamini katika kuajiriwa badala ya kuwa mwajiri... siyo kosa lako bali umekuzwa kuwanyenyekea Wazungu na Mabasha zako...
RockSpider nafikiri tatizo kwako ni ajira tu. Kwa sababu wewe na wengine JF ndiyo ofisi yenu sioni ajabu kuja na nonsense issues kama hizi. Hivi kweli mnategemea kujenga familia zenu pamoja na nchi yenu kwa tabia kama hizi? Sijui wewe unatokea kanda gani ya nchi hii? Hebu jaribu kuwa innovative ktk mambo ya kujenga familia yako kuliko kuifanya JF ofisi ya tumbo lako!
 
Katika hali isiyo ya kawaida leo aliyekuwa waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka ameponea chupuchupu baada ya vijana wa PCCB Wilayani Muleba kuvamia nyumbani kwakwe ghafla baada ya kupata tetesi kuwa alikuwa akigawa hongo kwa vijana wa mjini hasa wachuuzi wa ndizi ambao walikuwa wamejumuika kwake baada ya kuwaarika.

Alibainika mapema leo asubuhi kuwa profesa Anna anakikao na vijana hao na mwaliko wao uliambatana na ahadi ya pesa. Baada ya vijana wa PCCB kujulishwa kuhusu mchezo huo walijipanga kuhakikisha wanafanya kazi yao lakini taarifa za PCCB kujipanga zilimfikia Profesa kabla hajaanza kutoa rushwa.

PCCB walipovamia nyumbani kwake Kagabiro walikuta kundi la vijana na walipowapekua vijana hao hawakuweza kupata pesa hizo maana profesa alikuwa keshatonywa mapema kuhusu mtego wa PCCB.

Toka waziri huyo atemeshwe kibarua chake amekuwa kijijini kwao akifanya kila liwezekanalo kuwashawishi wananchi wa kada mbali mbali kwamba yeye ameonewa na kila baada ya vikao amekuwa na kawaida ya kutoa pesa kuanzia tsh 5000 hadi 25000 kulingana na hadhi ya mtu.

Juzi alifanya mkutano na watendaji, wenyeviti wa matawi wa CCM na makatibu wao ambapo baada ya kikao kwasababu walikuwa wengi waliambulia shs5000 na wengine 6000.

Watu wanajuuliza kweli na profesa anatimza ahadi zake kwa wananchi kupitia hongo kwa viongozi au ndo mambo ya ESCROW yameanza kufanya kazi?

Muleba tumebaki midomo wazi.

OLImfera.NOYEJURA.
 
Haya Makubwa! Mimi mwenyewe niliudhuria semina ile ya Wafanyabiashara ya Ndizi wilayani Muleba. Semina ile ilitokana na maombi ya wafanyabiashara hawa kupitia mratibu wao Bwana Evodius (0754766621), siku ya tarehe 02.jan.2015 kwenye kikao cha viongozi wa chama wa Matawi na Kata.

Katika semina ile wafanyabiashara walimueleza Mbunge kuwa wanasumbuliwa na masoko, kwani wakipeleka Ndizi kule Dsm, Mwanza, Igunga n.k. Huishia kuwaachia Ndizi zile kwa mikopo bila kupewa hela taslimu na kurudi nyumbani kusubili hela nyumbani na wakati mwingine huishia kutapeliwa.

Waliomba Mbunge awatafutie mawakala ambao wanaweza kuwasimamia kuchukua Ndizi bila mikopo. Hapa rushwa ilitokea mlango gani?. Ni maajabu sana hata ukifuatilia PCCB, Muleba hata Bukoba, hakuna Ofisa yoyote aliyefika pale, sijui bwana Kagugu habari yako ina ukweli kiasi gani?

Kuhusu kikao cha viongozi wa CCM, ngazi ya Matawi,Kata na Wilaya, huu ni utaratibu ambao umekuwepo tangu Mwaka 2011. Utaratibu kila mjumbe huwa anawezeshwa nauli ya tsh.5,000
Na Tsh.10,000 kwa wale wajumbe wa visiwani walioudhuria pale. Kikao cha juzi Mgeni rasmi alikuwa
Ktb/CCM/Mkoa. Hivi rushwa ilitokea mlango gani?

Bwana Kagugu mbona hajatoa taarifa ya semina ya TASAF, iliyofanyika Naflini Hotel Muleba, ambapo Mkuu wa Wilaya alikuwa mgeni rasmi, Wajumbe wote K/Ulinzi na Usalama, Madiwani wote, na Mbunge mwenyewe waliudhuria na kupewa posho ya 180,000, ambayo Mbunge hakuichukua?. Hivi PCCB walitoka wapi?. Ushauri wangu hata kama mtu humpendi, sio vema na haki kutoa habari ya uongo. Bwana Kagugu, put your brain in gear before opening your mouth.

1. Kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia mijadala katika jukwaa hili, ni kosa kubwa kumtambua mchangiaji kwa jina lake halisi. Mods, nadhani huyu Ndugu denis charles anastahili kufungiwa indefinitely.

2. Aliyeleta mada i.e. Kamugunga amesema kikao tajwa kilichokuwa na lengo la kutoa hongo kilifanyika nyumbani kwa Anna Tibaijuka. Sasa nakuuliza, vikao vya viongozi wa CCM na TASAF hufanyika nyumbani kwa Mbunge? Je, kikao na wachuuzi wa ndizi kinasimama kama kikao halali cha CCM na hivyo kuhalalisha malipo ya posho ulizosema? Kama wachuuzi wa ndizi ndio waliomba kikao, kwa nini walipwe posho? Kwa nini baada ya kupata tetesi kuwa PCCB walikuwa wanafuatilia kikao hicho, kwa nini aliacha kulipa posho? Kubwa zaidi, Mbunge anapata wapi pesa za kulipa watu wanaoshiriki vikao vyake posho?

3. Je, tofauti ya posho inayolipwa na Mbunge na rushwa ni nini? Je, asipolipa posho, watu wataacha kushiriki vikao vya Mbunge?
 
Haya ndiyo matokeo ya kukubali kufanya Kazi na waswahili wa kibongo,Mama Tiba alikuwa na heshima kubwa UN angalia sasa anavyochafuliwa,Yote haya yanampata baada ya kukubali kufanya Kazi na yule mswahili wa M.s.o.g.a!
 
Kama unagombea hiyo ni haki yako, lakini sio vema kwenda kwa staili ya kuongea uzushi husiokuwa na chembe ya ukweli. Kama huo ndo mkakati wako, you better finetune your strategy.
 
1. Kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia mijadala katika jukwaa hili, ni kosa kubwa kumtambua mchangiaji kwa jina lake halisi. Mods, nadhani huyu Ndugu denis charles anastahili kufungiwa indefinitely.

2. Aliyeleta mada i.e. Kamugunga amesema kikao tajwa kilichokuwa na lengo la kutoa hongo kilifanyika nyumbani kwa Anna Tibaijuka. Sasa nakuuliza, vikao vya viongozi wa CCM na TASAF hufanyika nyumbani kwa Mbunge? Je, kikao na wachuuzi wa ndizi kinasimama kama kikao halali cha CCM na hivyo kuhalalisha malipo ya posho ulizosema? Kama wachuuzi wa ndizi ndio waliomba kikao, kwa nini walipwe posho? Kwa nini baada ya kupata tetesi kuwa PCCB walikuwa wanafuatilia kikao hicho, kwa nini aliacha kulipa posho? Kubwa zaidi, Mbunge anapata wapi pesa za kulipa watu wanaoshiriki vikao vyake posho?

3. Je, tofauti ya posho inayolipwa na Mbunge na rushwa ni nini? Je, asipolipa posho, watu wataacha kushiriki vikao vya Mbunge?

Oh! Kama rules and regulations haziruhusu mchangiaji kutambulika kwa jina basi niombe msamaha kwa hilo.

Labda nifafanue kwamba mimi niliamua kujitambulisha kwa jina langu, kama njia mbadala ya kudhibitisha kile nilichokisema kuwa ni cha kweli, na niwe tayari kuwajibika.

Aiingii akilini mtu mzima kuibuka na hoja ya kipuuzi na ya uongo kabisa, halafu uongo huo uachwe bila ya ufafanuzi wa kina na wa ukweli. Niamini kuwa maelezo yangu yamejitosheleza nini kilifanyika jana, na kama kuna mtu hanaamini taarifa yangu, nitarajie kuwa atakuja na ushahidi wake kukanusha kile nilichokisema. Hakuna rushwa yoyote, wa PCCB, na katika hali ya kawaida wajumbe wote wanaoudhuria kikao kama kile kuwarudishia nauli zao sio rushwa wala kitu cha ajabu.

Haijalishi kikao kimefanyika kwa nani?. Hebu tujaribu kupunguza miemko ya giliba zisizokuwa na maana.
 
1. Hujaelewa. Aliyeleta mada amejitambulisha kama Kamuguna. Wewe ukamtambua kama Bwana Kagugu. Kwa Mimi msomaji, ulichokifanya hapa ni kutuambia kuwa Kamuguna = Bwana Kagugu (Jina halisi). Hili ni kosa kubwa katika jukwaa hili hata kama so kweli kuwa Kamuguna wa JF ni Bw. Kagugu wa Muleba.

2. Watu mkishazoea rushwa na kukosa maadili mnajisahau na kuhalalisha maovu. Mnakuwa vipofu, which is expected. Vikao rasmi vya chama na TASAF vifanyike nyumbani kwa mbunge na washiriki walipwe "posho" halafu unasema haijalishi? Kwa ufahamu wako rushwa/corruption/graft/kickback ni nini? No wonder huyu mama alipokea mabilioni kutoka kwa mfanyabiashara na bado hakuona tatizo. Kwamba Rais atamshangaa kama atajiuzulu kwa kupokea "mchango" kutoka kwa mfanyabiashara.

3. How often do you think about your own thinking? Do yourself a little favour and embark on some sort of self-assessment.
 
Bila shaka wewe ni yule mwanae mvaa vimini! Kule SIHA mzungu anatamba kuwabaka wanawake na kuua raia wasiokuwa na hatia, mvomero, kilombero, bagamoyo yote imechukuliwa na ndugu wawekezaji uchwara wa Mamako Anna... Huyo Stahili yake ni Pingu tu! Hakuna jinsi... Kuhusu ajira: unaonekana wewe ni mtumwa wa fikra, unaamini katika kuajiriwa badala ya kuwa mwajiri... siyo kosa lako bali umekuzwa kuwanyenyekea Wazungu na Mabasha zako...

Hii inaonyesha akiri zako zilivyo finyu na hata usaidiweje kwani train ilishaondoka mapema kabisa. Kama ni kuongelea maswala ya ardhi basi kaongee na mkuu wa nchi pamoja na serikali. Huyu mama anatekeleza yale yaliyopitishwa na chama chako CCM na si zaidi ya hapo. Inaonekana wewe ni kati ya wale wanaolipwa kuendelza uchafu wa kuwachafua baadhi ya watu kwa ajenda ambazo masikini wewe huzijui kwani what matters kwako ni tumbo tu. Na ni bahati mbaya kuwa unachokiongea ukifahamu ndiyo maana unaingiza na private issues kwani mtoto wake akivaa vimin inaangiaje hapa kwenye issue hii isiyokuwa na mshiko? Jaribu kujifunza kuwa mtu wa kutumia akiri kuliko kusukumwa na njaa ya tumbo lako. Na kama uipata nafasi ya kuijiangalia kwenye kioo utagundua wewe ulivyo na jamii inavyokuona kuwa wewe ndiyo wale wale ....................!!
 
1. Kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia mijadala katika jukwaa hili, ni kosa kubwa kumtambua mchangiaji kwa jina lake halisi. Mods, nadhani huyu ndugu denis charles anastahili kufungiwa indefinitely.

2. Aliyeleta mada i.e. Kamugunga amesema kikao tajwa kilichokuwa na lengo la kutoa hongo kilifanyika nyumbani kwa anna tibaijuka. Sasa nakuuliza, vikao vya viongozi wa ccm na tasaf hufanyika nyumbani kwa mbunge? Je, kikao na wachuuzi wa ndizi kinasimama kama kikao halali cha ccm na hivyo kuhalalisha malipo ya posho ulizosema? Kama wachuuzi wa ndizi ndio waliomba kikao, kwa nini walipwe posho? Kwa nini baada ya kupata tetesi kuwa pccb walikuwa wanafuatilia kikao hicho, kwa nini aliacha kulipa posho? Kubwa zaidi, mbunge anapata wapi pesa za kulipa watu wanaoshiriki vikao vyake posho?

3. Je, tofauti ya posho inayolipwa na mbunge na rushwa ni nini? Je, asipolipa posho, watu wataacha kushiriki vikao vya mbunge?

mwache uzushi wa kijinga.ebu kumbuka kuna hela ya stanbic, kwa nini mnahanghaika na mtu ambaye ni fourth part?hatimaye tutawachukulia kuwa m wachawi na swala sio escrow.na wewe mleta mada u mjinga na haujitambui na umejaa wivu,fitina na husuda.
 
So, hapa unamtetea "mtu ambaye ni fourth part" [sic]? Au unasema na waliochukua hela Stanbic kwa sandarusi nao wanastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine? Kwa maneno mengine unauliza, kwa wengine walioshirikiana na Tibaijuka hawajachukuliwa hatua? Haya ni maswali sahihi.

Na utakuwa " mtu ambaye ni fourth part" [sic] na mgao wako ukawa US$ 1,000,000?

Anayetuhumiwa ni Anna Tibaijuka. Je, wewe ni Anna Tibaijuka? Au msemaji wake?
 
So, hapa unamtetea "mtu ambaye ni fourth part" [sic]? Au unasema na waliochukua hela Stanbic kwa sandarusi nao wanastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine? Kwa maneno mengine unauliza, kwa wengine walioshirikiana na Tibaijuka hawajachukuliwa hatua? Haya ni maswali sahihi.

Na utakuwa " mtu ambaye ni fourth part" [sic] na mgao wako UKAWA US$ 1,000,000?

Anayetuhumiwa ni Anna Tibaijuka. Je, wewe ni Anna Tibaijuka? Au msemaji wake?

Mbona HAUELEWEKI HOJA UNAYOJARIBU KUJENGA?KWANZA FAHAMU KUWA TIBAIJUKA SIO MTUHUMIWA WA ESCROW NA AMEFUKUZWA KAZI SIO KWA SABABU ANAHUSIKA NA UCHOTWAJI WA HELA YA ESCROW.ISITOSHE HATA KAMA HELA YA ESCROW ILIKUWA YA UMMA BADO KUNA WAHUSIKA WENGI WA MOJA KWA MOJA AMBAO NADHANI NDO MNGEKOMAA NAO BADALA YA KUSHUPAA NA MTU MMOJA KILA SIKU.HYO INAONESHA KUWA TUTAKUWA NA AJENDA BINAFSI.
 
Nimekuelewa. Tatizo lako ni kwa nini watu wanakomaa na Tibaijuka pekee wakati wahusika wa moja kwa moja ni wengi? Hili ni swali zuri. Rais aliahidi wote walioshiriki kwa namna yoyote ile watachukuliwa hatua. Huyu mama suala lake lilikuwa rahisi kwa kuwa lilikuwa dhahiri mno.

Na watu walimwamini sana huyu mama. Alikuwa na heshima kubwa nje na ndani ya nchi. Hata hapa JF aliheshimika sana. Sasa hathubutu kukanyaga hapa. Amebaki kutuma mamluki tu. Wengi hawakutarajia aje kuwa kama kina Chenge na kushiriki kuibia wananchi. Amewaangusha wengi. Na ndio maana unaona watu "wanashupaa na mtu mmoja".

Akiwa kama mwanachama hapa, kwa nini tangu sakata hili lianze hajaja kutoa ufafanuzi wake hapa? Wakati anajiunga, aliahidi kutumia jukwaa hili kufafanua mambo mbalimbali. Tulimpongeza kwa ujasiri huo. Sasa ni nini kimetokea?
 
anagawa pesa za escrow ameshafukuzwa na JK hizo pesa atapeleka wapi .Mwigulu alisema bungeni watazilipia kodi hizo pesa 31.12.2014 lakini mpaka leo 07.01.2015 yupo kimya
 
Nimekuelewa. Tatizo lako ni kwa nini watu wanakomaa na Tibaijuka pekee wakati wahusika wa moja kwa moja ni wengi? Hili ni swali zuri. Rais aliahidi wote walioshiriki kwa namna yoyote ile watachukuliwa hatua. Huyu mama suala lake lilikuwa rahisi kwa kuwa lilikuwa dhahiri mno.

Na watu walimwamini sana huyu mama. Alikuwa na heshima kubwa nje na ndani ya nchi. Hata hapa JF aliheshimika sana. Sasa hathubutu kukanyaga hapa. Amebaki kutuma mamluki tu. Wengi hawakutarajia aje kuwa kama kina Chenge na kushiriki kuibia wananchi. Amewaangusha wengi. Na ndio maana unaona watu "wanashupaa na mtu mmoja".

Akiwa kama mwanachama hapa, kwa nini tangu sakata hili lianze hajaja kutoa ufafanuzi wake hapa? Wakati anajiunga, aliahidi kutumia jukwaa hili kufafanua mambo mbalimbali. Tulimpongeza kwa ujasiri huo. Sasa ni nini kimetokea?

Ni KWELI LAKINI KWA KUFANYA HIVYO TUNAWAPA WENGINE UNAFUU NA MARA ZOTE HIYO NDIYO MBINU YA SERIKALI.MJADALA WOTE WA ESCROW UMEHAMIA KWA TIBAIJUKA TUNGALI HATUJUI HATA SENTI MOJA YA HELA ILIYOTOKA STANBIC ILIENDA WAPI.NA HELA HII NDO KUBWA SAN, ZAIDI YA BIL13O.
 
Katika hali isiyo ya kawaida leo aliyekuwa waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka ameponea chupuchupu baada ya vijana wa PCCB Wilayani Muleba kuvamia nyumbani kwakwe ghafla baada ya kupata tetesi kuwa alikuwa akigawa hongo kwa vijana wa mjini hasa wachuuzi wa ndizi ambao walikuwa wamejumuika kwake baada ya kuwaarika.

= kuwaalika
 
Mapovu ya nini Dada? Umewahi kumsikia Halima Mdee akimchana chana huyu Jambazi wa ESCROW kiasi cha kumfanya aachie ushuzi mwembamba? Unafikiri wote tunalishwa na huyo mamako aliekoswakoswa kunaswa na PCCB jana? Mradi wa kigamboni na hisa zake za ESCROW unafikiri hazijulikani?... Tuepushie mashuzi hapa jamvini ...
Hii inaonyesha akiri zako zilivyo finyu na hata usaidiweje kwani train ilishaondoka mapema kabisa. Kama ni kuongelea maswala ya ardhi basi kaongee na mkuu wa nchi pamoja na serikali. Huyu mama anatekeleza yale yaliyopitishwa na chama chako CCM na si zaidi ya hapo. Inaonekana wewe ni kati ya wale wanaolipwa kuendelza uchafu wa kuwachafua baadhi ya watu kwa ajenda ambazo masikini wewe huzijui kwani what matters kwako ni tumbo tu. Na ni bahati mbaya kuwa unachokiongea ukifahamu ndiyo maana unaingiza na private issues kwani mtoto wake akivaa vimin inaangiaje hapa kwenye issue hii isiyokuwa na mshiko? Jaribu kujifunza kuwa mtu wa kutumia akiri kuliko kusukumwa na njaa ya tumbo lako. Na kama uipata nafasi ya kuijiangalia kwenye kioo utagundua wewe ulivyo na jamii inavyokuona kuwa wewe ndiyo wale wale ....................!!
 
Bandugu ili tanzania ifike mahali pale wote tunapenda, vita dhidi ya rushwa lazima iwe ya wote bila kujali vyeo, vyama, udini na mengineyo.
 
Kwa nini hizo hela anazogawa asiwawekee kwenye account zao za benki?
 
Back
Top Bottom