Profesa Anna chupuchupu kukamatwa na PCCB

KAMUGUNGA

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2013
Posts
238
Reaction score
269
Katika hali isiyo ya kawaida leo aliyekuwa waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka ameponea chupuchupu baada ya vijana wa PCCB Wilayani Muleba kuvamia nyumbani kwakwe ghafla baada ya kupata tetesi kuwa alikuwa akigawa hongo kwa vijana wa mjini hasa wachuuzi wa ndizi ambao walikuwa wamejumuika kwake baada ya kuwaarika.

Alibainika mapema leo asubuhi kuwa profesa Anna anakikao na vijana hao na mwaliko wao uliambatana na ahadi ya pesa. Baada ya vijana wa PCCB kujulishwa kuhusu mchezo huo walijipanga kuhakikisha wanafanya kazi yao lakini taarifa za PCCB kujipanga zilimfikia Profesa kabla hajaanza kutoa rushwa.

PCCB walipovamia nyumbani kwake Kagabiro walikuta kundi la vijana na walipowapekua vijana hao hawakuweza kupata pesa hizo maana profesa alikuwa keshatonywa mapema kuhusu mtego wa PCCB.

Toka waziri huyo atemeshwe kibarua chake amekuwa kijijini kwao akifanya kila liwezekanalo kuwashawishi wananchi wa kada mbali mbali kwamba yeye ameonewa na kila baada ya vikao amekuwa na kawaida ya kutoa pesa kuanzia tsh 5000 hadi 25000 kulingana na hadhi ya mtu.

Juzi alifanya mkutano na watendaji, wenyeviti wa matawi wa CCM na makatibu wao ambapo baada ya kikao kwasababu walikuwa wengi waliambulia shs5000 na wengine 6000.

Watu wanajuuliza kweli na profesa anatimza ahadi zake kwa wananchi kupitia hongo kwa viongozi au ndo mambo ya ESCROW yameanza kufanya kazi?

Muleba tumebaki midomo wazi.
 
Tunamsubiri aje akanushe. Ni member humu. Aibu kwa Tiba na lichama lao.
 
Katika hali isiyo ya kawaida leo aliyekuwa waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka ameponea chupuchupu baada ya vijana wa PCCB Wilayani Muleba kuvamia nyumbani kwakwe ghafla baada ya kupata tetesi kuwa alikuwa akigawa hongo kwa vijana wa mjini hasa wachuuzi wa ndizi ambao walikuwa wamejumuika kwake baada ya kuwaarika.

Alikuwa akigawa hongo ili wampe huduma gani?
 
hongo ndani ya ccm ni sawa na maji baharini yakikosa bahari sii bahari tena, mama gawa tu kila kitu
 
Ukiacha Hilo li kashfa la Escrow tu hata Haya matokeo ya uchaguzi sm yamewashtua CCM wengi wanagunia tumboni,Ila kwa hadhi ya huyu mama Nadhani angefuata nyayo za Salim A.S Haya mambo ya kuabishana mchana kweupe awaachie kina Lusinde,nini hasa anataka mpk agawe hongo kiasi hicho?
CCM NI LAANA INAYOLITAFUNA TAIFA.
 
Anadhalilisha maprofesa wenzake waliotulia except prof. Muongo na yule aliyepuliziwa perfume ya uprofesa na wachina ili wapate gesi na meno ya tembo.
 
hahahaa kipindi kama hiki ccm wanahangaika sana, kule chato magufuli tumeambiwa alikuwa anagawa sahani na kupakulia watu msosi lol!
 
Quite right, she must be very careful.

Aje akanushe kama ni uzushi. Pigeni simu Muleba mkajulishwe mshike mshike wa leo nyumbani kwake. Huyu mama anazidi kutudhalilisha na ni aibu tupu kwa wanaMuleba.
 
Anadhalilisha maprofesa wenzake waliotulia except prof. Muongo na yule aliyepuliziwa perfume ya uprofesa na wachina ili wapate gesi na meno ya tembo.

hahahahahahah! mkuu hebu zisamehe mbavu zangu, kwamba kapuliziwa perfume ya uprof wa kichina, kwhyo akiondoka madarakan na harufu inaisha siyo!
 
Katika hali isiyo ya kawaida leo aliyekuwa waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka ameponea chupuchupu baada ya vijana wa PCCB Wilayani Muleba kuvamia nyumbani kwakwe ghafla baada ya kupata tetesi kuwa alikuwa akigawa hongo kwa vijana wa mjini hasa wachuuzi wa ndizi ambao walikuwa wamejumuika kwake baada ya kuwaarika.

Alibainika mapema leo asubuhi kuwa profesa Anna anakikao na vijana hao na mwaliko wao uliambatana na ahadi ya pesa. Baada ya vijana wa PCCB kujulishwa kuhusu mchezo huo walijipanga kuhakikisha wanafanya kazi yao lakini taarifa za PCCB kujipanga zilimfikia Profesa kabla hajaanza kutoa rushwa.

PCCB walipovamia nyumbani kwake Kagabiro walikuta kundi la vijana na walipowapekua vijana hao hawakuweza kupata pesa hizo maana profesa alikuwa keshatonywa mapema kuhusu mtego wa PCCB.

Toka waziri huyo atemeshwe kibarua chake amekuwa kijijini kwao akifanya kila liwezekanalo kuwashawishi wananchi wa kada mbali mbali kwamba yeye ameonewa na kila baada ya vikao amekuwa na kawaida ya kutoa pesa kuanzia tsh 5000 hadi 25000 kulingana na hadhi ya mtu.

Juzi alifanya mkutano na watendaji, wenyeviti wa matawi wa CCM na makatibu wao ambapo baada ya kikao kwasababu walikuwa wengi waliambulia shs5000 na wengine 6000.

Watu wanajuuliza kweli na profesa anatimza ahadi zake kwa wananchi kupitia hongo kwa viongozi au ndo mambo ya ESCROW yameanza kufanya kazi?

Muleba tumebaki midomo wazi.

Cc: Anna Tibaijuka
 
Last edited by a moderator:
Uhitaji uthibitisho mwingine kuwa nchi inaongozwa na wahuni. Huyu mama ndiye aliyejiita jembe la Kikwete. Maana yake yeye na profesa mwenzie wa kichina ndugu moja kwenye rushwa.
 
Back
Top Bottom