Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni; aanza kwa kasi!

Mkuu:

Nchi ni lazima iongozwe na sheria.

Kwenye tahariri yake na media Mama Tibaijuka alisema"wale waliochukua maeneo ya wazi ni bora wangejisalimisha sasa ili tuongee nao"

Kwenye sheria hii kauli haipo;kama ana ushahidi kuwa kuna watu wamechukua kiharamu ardhi iliyotengwa na serikali kwa shughuli za wazi basi yeye HAMNA KUONGEA NAO watu kama hao, anachotakiwa ni kuwapeleka mahakamani wakaonane Mahakama!

Au ni yale mambo ya EPA kwa mgongo wa ardhi?Unayemtuhumu kwa uharifu unamuita ofisini kwako kuongea nae nini?
 
Hii inanikumbusha mambo ya Mkwere na EPA, eti rudisheni pesa niwasamee. Kama wamevunja sheria wachukuliwe hatua za kisheria wao na hao maofisa wa ardhi, simple as that!
 
Waziri mpya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof Anna Tibaijuka jana aliibuka na kuwataka watu wote waliopora ardhi ya serikali na viwanja vya wazi na na kujenga katika maeno ya fukwe wajisalimishe haraka wizarani kwake kabla ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Kwa kuwa ni vizuri viongozi kama yeye wakaongoza kwa kuonyesha mifano ni vyema Prof Anna Tibaijuka akarejesha ardhi ya serikali zaidi ya ekari 100 aliyochukua katika ranchi ya utafiti wa magonjwa ya mifugo iliyoko wilaya ya Kinondoni.

Prof Anna Tibaijuka alitumia ardhi hiyo kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari ya wasichana iitwayo Barbro Johansen. Na mara tu alipochaguliwa kuwa Waziri wa Mifugo Mhe John Magufuli aliwahi kutoa wito na kuwataka wote waliomilikishwa ardhi za ranchi za taifa kurejesha ardhi husika kwa maslahi ya sekta ya mifugo.

Kana kwamba hiyo haitoshi, Prof Anna Tibaijuka akaingilia na kuchukua line ya maji iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya vijiji vilivyoko jirani na shule yake. Mpaka sasa wakazi wa vijiji hivyo ambao idadi yao inakua kwa kasi sana hawana huduma ya maji ya safi ya bomba.

Najua Prof Anna Tibaijuka anaweza kujitetea kuwa ardhi ilitolewa kwa ajili ya maslahi ya taifa. Lakini kama kweli ardhi hiyo ingekuwa ni kwa maskahi ya taifa na sio binafsi, ada zinazolipwa katika shule yake zingekuwa nafuu kuwawezesha watoto kutoka familia maskini waweze kumudu kuingia shuleni hapo. Raisi Jakaya Kiwete amewahi mara kadhaa kuzitaka shule binafsi kupunguza ada wananzotoza ili kuwawezesha watoto kutoka familia maskini kumudu kusoma katika shule hizo.

Aidha kama mradi huo ungelikuwa ni kwa ajili ya maslahi ya taifa na sio binafsi, wakazi wa vijiji jirani na shule hiyo wangepatiwa huduma ya maji safi ya bomba kutoka shuleni hapo hasa ikizingatiwa kuwa shule hiyo ilichukua line ya maji ya vijiji na hivyo kuwakosesha wanakijiji huduma hiyo.

Naomba kuwasilisha!!!!!!!!!!
nina wasi wasi na wewe umevamia maeneo ya wazi ndo mana unaanza kumsakama waziri kwa kauli yake
 
ninachosisitiza prof anna tibaijuka hana moral authority ya kutenda yale anayohubiriiri. Tatizo letu watanzania wepesi kusahau na kusamehe. Sis ni mama huyu huyu aliyteona mfumo wa ccm na umoja wa wananwake (uwt) hauwezi kuwakomboa wanawake wa tanzania kutoka lindi la umaskini na akaamua kuanzisha baraza la wananwale (bawata) na kisha serikali ya ccm kuifuta kwa kuogopa kusambaa kwake mpaka vijijini. Alienda mahakamani kupinga na mahakama kumpatia ushindi.

Sasa ni kwanini hakuendeleza lile wazo lake la bawata, what changed ever since? Kilachobadilika ni thamani ya ardhi. Na yeye tayari alikwisha chotewa ekari 100 za serikali katika jiji la dar es salaam.


kwahiyo kutokana na kujichukulia chake mapema, akamua kuwatelekeza wanawake wa tanzania
.
 
The legality of the ownership of the land has nothing to do with school fees. If the land was acquired legally then thats fine, angeweza fungua gesti lakini kaweka shule na vyote vina lipa in tanzania gesti zinalipa zaidi probably. So the fact that she decided to build a private school, and since the Ministry of Education has a deficit of schooling facilities, demand exceeds supply.. this is a good thing. You cant just judge the fees without knowing her running costs, she provides employment to Tanzanians and educates our children, even if its those that can afford it, it just means that there are more places in public schools for those who cant afford private education. In the end, more kids go to school. This thread has no merit and these allegations are completely unjustifiable unless it can be shown that the land was acquired contrary to the law of the land. Anything below that pelekeni kwenye stori za baa
HAKUNA LEGALITY YOYOTE KATIKA KUBINAFSISHA ARDHI YA SERIKALI TENA KW MGONGO WA NYUMA. IS SHE THE ONLY ONE TO BULID A PRIVATE SCHOOL IN TANZANIA? IF ALL OTHER PRIVATE SCHOOLS DEVELOPERS ACQUIRE LAND AT THE MARKET PRICE, WHY ONLY SHE GETS THAT PREFERENCE?

hON JOHN MAGUFULI WHEN SERVING FOR THE NEWLY ESTABLISHED LIVESTOCK M INISTRY GAVE A DIRECTIVE THAT ALL LAND MEANT FOR LIVESTOCK RANCHES AND LATER DUBIOUSLY FEL YUNDER PRIVATE OWNERSHIP SHOULD BE REVERTED BACK. IS THAT NOT THE SAME GOVERNMNET AS SHE IS SERVING NOW. i STERSS THAT SHE LACKS THE MORAL AUTHORITY TO IMPELEMENT WHAT SHE PREACHES AS HER HANDS ARE SOAKED WITH DIRT
.

IF PROVIDING EMPLOYMENT IS AN ISSUE THEN ALL OTHERS PUBLIC LAND GRABBERS SUCH AS BEACH PLOTS, OPEN SPSCES ETC, AS SHE IS, DO ALSO PROVIDE EMPLOYMNET OPPORTUNITIES DURING CONSTRUCTION AND OPERATION OF THEIR BUSINSESSES, HENCE DO QUALIFY TO BE LEGAL OWNERS. BUT THAT DOES NOT DELETE THE FACT THAT LAND WAS A GOVERNMENT RANCH MEANT FOR SPECIFIC USES.

PRIVATOISATION OF THATA AMOUNTS TO MISUSE OF OFFICE TO ALL THOSE INVOLVED IN ITS PRIVATISATION EVEN IF IT WAS THE PRESIDENT
 
HAKUNA LEGALITY YOYOTE KATIKA KUBINAFSISHA ARDHI YA SERIKALI TENA KW MGONGO WA NYUMA. IS SHE THE ONLY ONE TO BULID A PRIVATE SCHOOL IN TANZANIA? IF ALL OTHER PRIVATE SCHOOLS DEVELOPERS ACQUIRE LAND AT THE MARKET PRICE, WHY ONLY SHE GETS THAT PREFERENCE?

hON JOHN MAGUFULI WHEN SERVING FOR THE NEWLY ESTABLISHED LIVESTOCK M INISTRY GAVE A DIRECTIVE THAT ALL LAND MEANT FOR LIVESTOCK RANCHES AND LATER DUBIOUSLY FEL YUNDER PRIVATE OWNERSHIP SHOULD BE REVERTED BACK. IS THAT NOT THE SAME GOVERNMNET AS SHE IS SERVING NOW. i STERSS THAT SHE LACKS THE MORAL AUTHORITY TO IMPELEMENT WHAT SHE PREACHES AS HER HANDS ARE SOAKED WITH DIRT
.

IF PROVIDING EMPLOYMENT IS AN ISSUE THEN ALL OTHERS PUBLIC LAND GRABBERS SUCH AS BEACH PLOTS, OPEN SPSCES ETC, AS SHE IS, DO ALSO PROVIDE EMPLOYMNET OPPORTUNITIES DURING CONSTRUCTION AND OPERATION OF THEIR BUSINSESSES, HENCE DO QUALIFY TO BE LEGAL OWNERS. BUT THAT DOES NOT DELETE THE FACT THAT LAND WAS A GOVERNMENT RANCH MEANT FOR SPECIFIC USES.

PRIVATOISATION OF THATA AMOUNTS TO MISUSE OF OFFICE TO ALL THOSE INVOLVED IN ITS PRIVATISATION EVEN IF IT WAS THE PRESIDENT

Yani haya yote hayakusemwa wakati anagombea ubunge, kuchguliwa waziri nk. Lakini leo hii anazungumzia viwanja vya matajiri basi imekua yeye ndio fisadi. Nilishasema wasemaji wa mafisadi ni wengi !

Swala la viwanja vya beach nina muunga mkono, sasa kama kuna mtu anataka kufungua mjadala mwingine na afungue. Hili swala linawagusa viongozi na wafanyabiashara (mafisadi) wengi. Akifanikiwa itakuwa vizuri, na kama **** issue ya kiwanja chake nayo tutaisimamia bila kujali yeye ni nani au alifanya nini..
 
Hapa sisiemu kama wewe si japo fisadi uchwala huingizi kichwa kikapenya!!!!! Kumbe anna naye ni fisadi uchwala ndiey maana akapenya, tena kwa kuingilia mlango wa uani-mlango batili-sikujua wala sikutarajia??????????????
 
yani haya yote hayakusemwa wakati anagombea ubunge, kuchguliwa waziri nk. Lakini leo hii anazungumzia viwanja vya matajiri basi imekua yeye ndio fisadi. Nilishasema wasemaji wa mafisadi ni wengi !

swala la viwanja vya beach nina muunga mkono, sasa kama kuna mtu anataka kufungua mjadala mwingine na afungue. Hili swala linawagusa viongozi na wafanyabiashara (mafisadi) wengi. Akifanikiwa itakuwa vizuri, na kama **** issue ya kiwanja chake nayo tutaisimamia bila kujali yeye ni nani au alifanya nini..

hakuna mtu anayepinga suala la beach plots na open spaces lisifanyiwe kazi. Lakini ninachotaka kutahadharisha hapa ni kuwa ni dagaa tu watakaonewa ila mapapa wa kuvamia ardhi za umma hawataguswa. Hii ndo hulka ya ccm. Kwanini niwaache watanzania wenzangi mkiwa na fake hopes wakati inafahamika wazi kuwa ndani ya ccm hawanyoosheani vidole. Hili suala la kuwaita ofisini wazungumze maana yake nini, wanazungumza nini. Si ndio mambo ya kukutana "kiraracha ya mzee wai nji hii".

Kwa kuwa waziri mwenye dhamana ya ranchi za serikali alikwisha toa kauli kuwa wote waliomilikishwa ardhi ndani ya ranchi za serikali walifanya hivyo kinyume cha taratibu na sheria, hivyo hata yeye aliipata ardhi hiyo kwa njia za rushwa. Hivyo anatakiwa kuirejesha. Hoja kuwa shule ni kwa maslahi ya taifa haina mashiko hata kidogo. Mabona wawekazaji wengine wa shule za msingi, sekondari na vyuo hulazimka kununua ardhi kwa bei ya soko ili kujenga huduma hizo?

Kama ni hivyo serikali itoe mwongozo wa kuwapatia ardhi za bure wote wanaotaka kujenga shule za msingi, sekondari na vyuo kama mchango wake katika huduma za elimu hapa nchini. Kwa kuwa katika ranchi husika ardhi imebaki basi itolewe kwa wawekezaji wengine kwa njia za wazi haraka iwezekanavyo kabala prof anna tibaijuka hajatumia madaraka yake kujimilikisha ardhi iliyosalia katika ranchi hiyo
.
 
Mimi nadhani Tibaijuka anatakiwa aanze kuwataka maafisa wake waliohusika na hizi sakata za ardhi wajiuzulu kisha ndio awafuate waliouziwa. akianza na waliouziwa, muda wake utaisha kabla hajatimiza lengo lake kwani waliouza ndio ambao anatarajia watekeleze maagizo yake.

in other words, she is hitting the nail from the wrong end.
 
Kauli ya Prof. Tibaijuka kuhusu wale waliojenga nyumba zao ufukweni na kuweka uzio unaowazuia wananchi kwenda kupumzika huko beach kumewafanya wale waliouziwa fukwe hizo enzi za Mayor Londa waanze kujenga kwenye fukwe hizo kwa haraka haraka kwa kuogopa kuwa watafutiwa milki za viwanja hivyo.Kibaya zaidi viwanja hivyo sehemu za mbezi beach mwisho wa Sykes Close viko karibu sana na bahari na inawabidi hata kuikata mikoko sehemu inapopumulia bahari wakati ikifulika na sasa wanajitahidi kufukia sehemu za bahari na kifusi ili waanze ujenzi. Ujenzi wa sehemu hizi utawazuia kabisa watu wa kawe na Mbezi kuweza kwenda beach kitu ambacho si cha busara. Ningeshauri kwa Mheshimiwa waziri kusitisha ujenzi sehemu zote za ufukweni mpaka hapo viwanja hivyo vitakapohakikiwa ama sivyo wananchi na hasa vijana watakosa sehemu za kupumzikia na uhalifu unaweza kuongezeka katika jamii. Naomba kuwasilisha
 
Very difficult to fight that war, the system is rotten from the core, therefore, to fight from the margins is ineffective!
 
It might be difficult to fight the war but not impossible to win it!! Nadhani kwa sehemu alizozielezea Ndinani hapo Mbezi Beach kwa Sykes kama kweli hawa mafisadi wataruhusiwa kujenga kwenye wet land ambako wanakata mikoko na kufukia kifusi it will be an enviromental disaster bahari ikifurika; si hivyo tu ujenzi huo ukiruhusiwa utaziba sehemu iliyobakia kwa watu kwenda beach kwani sehemu zingine zote ufukweni zimezungushiwa kuta. Sasa wananchi watakwendaje beach wakati wenye fedha wametaifisha bahari? Wahusika walishuhulikie hili mapema iwezekanavyo wakishirikiana na Mbunge Halima Mdee kwani watu tulimchagua kurekebisha haya madhambi ya meya mtaafu Salum Londa!!
 
Manyoni wampigia magoti Prof. Tibaijuka

Imeandikwa na Jasmin Shamwepu; Tarehe: 10th December 2010 @ 22:50

WAKAZI wa Manyoni mkoani Singida, wamemwomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kuyatembelea maeneo ya Majengo na Kipondoda wilayani humo ambako wamedai kuwa uongozi wa halmashauri umewapora ardhi wakazi wa maeneo hayo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema kuwa mgogoro uliopo katika maeneo hayo kama usipopatiwa ufumbuzi unaweza kusababisha kutokea kwa machafuko.

Mmoja wa wajumbe aliyejitambulisha kwa jina la Peter Shiyo alidai kuwa uporaji huo wa ardhi uliongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Mosses Matonya.

Alisema halmashauri hiyo iliwapora wananchi wa maeneo ya Majengo na Kipondoda ardhi yao na kuwauzia Waarabu kwa madai kuwa ni wawekezaji wakati hakuna vikao vya Serikali ya Kijiji ambavyo vimekuwa vikiidhinisha wawekezaji hao kupewa eneo.

Shiyo alisema kutokana na hatua hiyo kuna uwezekano mkubwa wa watu wa maeneo hayo kuzua machafuko na ili yasitokee ni vyema waziri mwenye dhamana ya ardhi, kuingilia kati ili kuweza kunusuru mgogoro unaoweza kujitokeza.

Alisema inashangaza kuona kuwa wapo watu ambao wameporwa mashamba zaidi ya hekari nne lakini Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani amekuwa akiwaamuru kuondoka katika maeneo hayo kwa madai kuwa wanatakiwa kupewa wawekezaji bila kuwapatia maeneo mbadala ya kuishi.

Mkazi mwingine alisema suala la viwanja limefikia hatua mbaya zaidi kwani hata katika sehemu ambazo zinajulikana kuwa ni za wazi, zimeuzwa kwa watu wanaodaiwa kuwa wawekezaji na mwananchi wakijaribu kuhoji wanafokewa na viongozi wa halmashauri.

Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Mosses Matonya alipoulizwa juu ya tuhuma zinazomkabili juu ya uporaji na ugawaji wa viwanja kiholela alidai kuwa ni tuhuma za kisiasa na kwamba wanaotakiwa kuulizwa ni madiwani wa maeneo husika na si yeye. "Kwangu hayo ni mambo madogo.

Mimi ni mwanasiasa na ninaendelea na siasa, masuala ya fidia kama ni ndogo ama ni kubwa kinachotakiwa ni kumtafuta bwana ardhi waongee naye, kila mtu ana mdomo wa kuongea anachokitaka, mimi nimeishazoea maneno,hivyo siogopi kitu chochote juu ya hilo," alisema
Matonya.
 
Mama Ana Tibaijuka mbunge wa Muleba Waziri anaeshughulia makazi,baada ya kuhoji uuzwaji wa Open spaces kwa wenye nazo ambao wengi wao aliwaita mafisadi ila juhudi za mwanzo zikagonga kisiki, ameibuka na kulalama kuwa genge la Wajanja serikalini waliopima miji waliacha viwanja eti wakaviita "viwanja vya wazi au open space".

Huu ni ufisadi mtakatifu kwa kuwa viwanja ivi vikiuzwa huwezi kumpokonya aliyenunua maana ni halali. Kama viwanja ivi vingeachwa kwa ajili ya matumizi ya viwanja vya michezo,au viwanja vya garden n.k basi wanunuzi wangetishiwa lakini wakinunua kiwanja cha wazi ambacho hakijapangiwa matumizi basi ni halali yao. Hii imekuja baada ya prof. Tibaijuka kutia mkwara eti mafisadi walionunua viwanja vya wazi waende waelewane walau wakomboe matofali,sasa wanamcheka kwa kuwa wamenunua kihalali.

Kweli mjini shule,watu wanacheza na maneno pamoja na sheria kwa ilo mama ataisoma namba! Hii inanikumbusha wakati ule fisadi alipoweka dhamana ya "sheep" yenye thamani ya mil.80
badala ya "ship".

Asingekuwa judge kugundua basi Serikali ya Tz ilikuwa imenyweshwa sumu takatifu. Prof. Ana Tiba, bongo noma; nenda uendako dunia nzima, ukirudi bongo utazidiwa kete tu!

Ama kweli mjini shule.
 
Ni vigumu kwangu kukubaliana na maelezo hayo. Nijuavyo miji mingi inayo " master plan" inayoelezea matumizi yanayo kusudiwa kwa kila eneo. Hata pale ambapo hakuna master plan kuna kitu kinachoitwa "DD plan;" ambayo pamoja na mambo mengine inaonyesha sehemu za wazi. Mtu anapopewa au kuhusiwa sehemu hiyo wahusika wote wanakuwa wamekwenda kinyume na kanuni za mipango miji, hivyo kitendo hicho hakiwezi kuwa halali. Kama na wewe ni mhusika umeliwa, labda mafisadi wamzidi nguvu mama wa watu.
 
Kwa nini kiwanja cha wazi kiuzwe? Kikiuzwa kitabaki cha wazi? Na kama kinauzika logic ya kukifanya cha wazi mwanzoni kabisa ilikuwa ni nini?
 
Tusipobadili ufikiri, Watanzania hata tuletewe Mungu au shetani kutuongoza hatutaokoka na shida za dunia hii
 
Back
Top Bottom