Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni; aanza kwa kasi!

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
16
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amewataka wananchi waliopora viwanja na maeneo ya wazi nchini na kujenga, wajisalimishe kwa mazungumzo, kwa sababu huenda wakaokoa hata matofali kabla hatua zaidi hazijachukuliwa.

Profesa Tibaijuka alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya wizara hiyo na kueleza kuwa masuala ya ardhi yasipofanyiwa kazi, sekta nyingine zitazorota.


"Umefika wakati sasa, tunataka kubadilisha mwonekano wa miji ... na kwa wanaosema wanatumia jeuri ya pesa, tutawashughulikia, lakini baada ya kufanya utafiti wa kutosha, kwa sababu hatuwezi kukurupuka, hivyo waliopora viwanja tunawataka wajisalimishe," alisema Profesa Tibaijuka ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia Makazi (UN-Habitat).


Alisema, migogoro ya ardhi hawataimaliza bila wananchi kuwasaidia na kwa sasa, watarudisha askari wa ardhi ili kuhakikisha wanapunguza migogoro ikiwamo ya wanaojenga holela na katika maeneo ya wazi.


Tibaijuka alisema, kati ya hekta 900,000 ni asilimia mbili tu ya maeneo ndiyo yaliyopimwa, hivyo wizara yake itahakikisha inapimwa, ili miji iwe katika hali inayotakiwa kwa sababu kwa sasa hairidhishi.


Aidha, Profesa Tibaijuka alisema si maendeleo yote yanahitaji fedha, hivyo kwa muda huu waliopewa na Rais, kuna mambo ambayo watayafanyia kazi kwa haraka ikiwamo kuandika majina ya mitaa yote.


"Watu wengi hawatambui mitaa wanayoishi inaitwaje, kwa sababu wala haina majina na unakuta anashindwa kabisa kuelekeza, lakini tukiiandika tutawasaidia, hivyo tutafanya jambo hili kwa haraka maana haihitaji fedha," alifafanua mbunge huyo wa Muleba Kusini.


Katika hatua nyingine, alisema kuna upungufu wa nyumba milioni tatu nchini, hivyo wanapaswa kujenga miji kwa kuboresha nyumba zilizopo na kuzijenga ambazo hazina viwango na kuziuza kwa wananchi.


"Wananchi wanatakiwa kutambua wanahitaji nyumba au ardhi, lakini watambue kama ni viwanja lazima waende nje ya mji, ila kama ni nyumba zipo ila zinahitaji maboresho na tutafanikiwa, kwa kuwa na benki za nyumba na mikopo ya nje, kwa sababu sekta binafsi pekee hazitaweza bila kuwa na fedha ... tuwaachie wahandisi wetu wajenge nyumba sisi tununue," alisema.


Alisema, watafanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na Ofisi ya Mazingira ili kuhakikisha miji inakuwa safi na salama; na kuboresha bonde la Mto Msimbazi, Dar es Salaam, ambalo limefanya hali ya hospitali ya Taifa Muhimbili kuwa mbaya.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Patrick Rutabanzibwa, alikiri baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki kugawa maeneo ya wazi na kueleza kuwa tayari ameanza kuwachukulia hatua za kisheria, ikiwamo kufanya mabadiliko ya vitengo kwa nia ya kuboresha utendaji kazi.


"Uvamizi wa maeneo ni mtandao wa watu wa wizarani na manispaa nami nimejitolea kuwashughulikia na tayari kuna waliokuwa wamepora viwanja na nimewataka wavirudishe na wengine walipora na kuwauzia wafanyabiashara wakubwa," alisema Rutabanzibwa.


Pia alisema wamesimamisha ujenzi wa eneo la wazi katika hoteli ya Palm Beach na kuahidi kufanya kazi bila kuhofia kashfa, kwani zipo tuhuma amevumishiwa na amezipeleka kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


Kwa upande wao, mawaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mary Nagu (Uwekezaji na Uwezeshaji) na William Lukuvi (Sera, Uratibu na Bunge), waliripoti rasmi katika Ofisi ya Waziri Mkuu na kuzungumza na wakuu wa idara, vitengo na taasisi chini ya Ofisi hiyo.


Mawaziri hao waliwataka watendaji kufanya kazi kwa ubunifu, ushirikiano, upendo, uwazi na bidii zaidi, ili kukidhi matarajio ya wananchi.


Nagu alisisitiza umuhimu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji bila ngojangoja ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wawekezaji.


Alisema hakuna uchumi duniani uliofanya vizuri bila uwekezaji, iwe wa kutoka nje au ndani ya nchi husika. Alibainisha kuwa Watanzania ndio wanatakiwa kushika hatamu ya uchumi wao.


Lukuvi alisisitiza watendaji kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa kasi zaidi ili kuongeza ufanisi na hatimaye kufikia malengo ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taifa kwa jumla.


Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu aliwaambia watendaji wakuu wa wizara hiyo kuwa anawapa uhuru wa kufanya uamuzi wenye tija na ufanisi na atakayeshindwa atajiondoa mwenyewe.


Alizungumza na wakurugenzi wakuu wa idara za uchukuzi na wa taasisi mbalimbali akijitambulisha kwao rasmi na kuanza kazi.


Nundu aliwataka kufahamu dhima waliyonayo katika kuendeleza sekta ya uchukuzi ili katika kipindi cha miaka mitano ijayo, fursa zilizomo zitumike vyema pamoja na kuboresha huduma za usafiri.


Aliwataka kupeana ushauri ili wasonge mbele, kuwa wadilifu na waaminifu huku wakitoa huduma kwa dhati na kwa wakati muafaka.


"Hakikisheni mnawajibika kulingana na wakati, katika suala la uchukuzi hatupo peke yetu ulimwenguni, zingatieni matakwa ya wateja," alisema Nundu na kuongeza:


"Fanyeni kazi kila mmoja kwa madaraka aliyonayo, toeni uamuzi wenye tija bila upendeleo na hata ubinafsi na hiyo iwe ahadi yenu kwetu," alisema.


Alisema, anatarajia kuimarisha kampuni ya reli, kwa lengo la kuipa uwezo wa kutoa huduma bora kwa kusafirisha abiria na mizigo ya ndani na nchi jirani, na kuendelezwa kama mhimili wa mpango wa maendeleo wa eneo la ukanda wa kati.
 

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,165
The tone is just same ol. one, only that the person is different! We have our popcorns ready mama Tiba.
 

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Huyu mama kumbe naye Hana tofauti na JK? Anadhani bado tunahitaji kutangaziwa kwamba kuna vigogo waliohodhi viwanja na maeneo ya wazi? Kwa nini asitutatangazi amerejesha viwanja na maeneo ya wazi mangapi na bado mangapi. Atuambie amechukua hatua gani kwa maafisa wa wizara yake na halmashauri waliofanya huo ufisadi.

Kubwa zaidi atutangazie kufuta hati ya "kuuza" eneo la Kigamboni na raia wake. Atutangazie hatua alizochukua dhidi ya ardhi ya loliondo iliyouzwa kwa waarabu na wananchi kufukuzwa, kupigwa, kuuawa, kuchoma nyumba na kuteketeza mali na mifugo yao.

Tunakaka atutangazie baada ya kutekeleza na alishindwa pia atutangazie. Asiendeleze usanii wa JK
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,518
6,110
huyu mama bana...eti wajisalimishe?anacheza tu hakuna la maana hapo analoongea
 

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,276
17,055
Waanze kujisalimisha CCM....pale Mango Garden ni open space na wao wamepatwaa...pale opposite na Meridien mwananyamala ni open space wamepatwaa....pale Kishamapendo Ilala ni open sapace na walipatwaa...list ni ndefu sana...Sinza ndio balaa kabisa
 

Diehard

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
449
321
Usisahau pale masaki nyumba za sitta na wenzake, Rose Garden hivi ni eneo la nani huwa linakuwa na sheshe za msimu kisha kimya
 

Tekelinalokujia

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
353
40
Drama za kuelekea 2015 zimeanza, JK alipoanza that time aliwapeleka hawa mabwana AR kwenye ile hoteli ya kitalii kuwapa darasa tukajua kazi pevu itaanza kumbe wapi walikua wanakula goodtime tuu.
 

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Profesor Tibaijuka atamweza Mahanga?
Katika serikali ya Tanzania kumekuwa na mtindo wa kulindana kati ya viongozi, ndiyo maana hata wakati ajenda za mafisadi na ubadhilifu mwingine wa mali za umma ulipofumuka, viongozi waliopaswa kuchukua hatua walifyata mkia.

Sasa jana (kupitia ITV news ya saa mbili usiku) Professor Tibaijuka ambaye aliteuliwa kuwa waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi alisema “wale wote waliovamia maeneo ya wazi, wajisalimishe”. Mahanga ambaye ni naibu waziri katika serikali ya kikwete ni mmoja wa wananchi wanaoongoza katika kuvamia maeneo mengi ya wazi. Sasa kwa wakazi wa Tabata, wanafahamu pale Bima, kushoto ipo Nyantare Social Hall na Nyantare Bar. Zikiwa zimekamata eneo lililokuwa la wazi na lina ukubwa unaokadiriwa kuwa kama meta kati ya 400 na 600! Hilo lilikuwa eneo la wazi, kwa sasa ni kitega uchumi cha mheshimiwa!

Pale Segerea, anajenga ghorofa katika eneo la wazi. Sasa Tibaijika ataweza kumkabili kiongozi mwenziwe na kumbomolea vitega uchumi vyake?

Yetu macho, tunasubili kuona nani atamvika paka kengere!!
 

mujusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2010
237
58
Kweli kabisa. Hii shighuli ya maeneo ya wazi na kugawa maeneo ya Fukwe kwa Dar es Salaam ni mfupa uliowashinda Fisi wengi. Katika kipindi toka awamu ya tatu hili jambo limeshindwa na tumezidi kuona open space zinaendelea kuporwa. Kwani hata hilo eneo la Palm Beach limeporwa na kujengwa kip[indi kipi? maeneo yenyewe wanatoa hao hao na ya hao hao. Mama atizame asije akajiuzuru mapema au kuomba ahamishwe Wizara. Vita anayotaka kuingia ni kali ina hitaji support kubwa na ama sivyo watu watamjaji kwa kauli yake.
mnaanzaga kwa mkwara, mwisho prrraaagggghhhhh...
 

Ndeusoho

Member
Jan 26, 2010
46
5
Suala la Rose Garden ni kwamba Mheshimiwa Magufuli alikosa uadilifu wakati akiwa Wizara ya Ardhi. Suala hilo lilishafanyiwa kazi kitaalamu na kiutawala na Makamba akiwa mkuu wa mkoa na likafikia mwisho lakini Magufuli kwa sababu zake alilazimisha wataalamu waandike alichotaka. Msisahau kuwa aliwahi kuzuia Boat isisafirishwe kwa kisingizio cha uzito lakini mizigo ya migodini ambayo ni mizito mara mia ikawa inapita.
 

Ndeusoho

Member
Jan 26, 2010
46
5
Atakapokuta viwanja 85% ni ofisi za CCM na nyumba za vigogo hatakuwa na moto huo. Hilo lilimshinda Magufuli licha ya kukabidhiwa orodha ya viwanja vya wazi vilivyovamiwa nchi nzima. Watanzania kinachotutafuna ni unafiki hasa kwenye itikadi za vyama na maamuzi ya Baraza la Mawaziri. Endapo Baraza la Mawaziri lingeweka bayana umuhimu wa kurejeshwa kwa maeneo ya wazi hili lingewezekana. Lakini kwa dhambi ya ubinafsi na ulafi walio nayo maslahi ya umma kamwe hayawezi kuwekwa mbele. Profesa amuulize Magufuli aliyafanyia nini yale majina aliyopewa na orodha ndefu ya viwanja vilivyovamiwa??
 

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
19
Wabongo ni watu wa ajabu kweli kweli!!!! Utaona pamoja na vitisho na mikikimikiki yote hii ya prof tiba ni kama ndiyo anawachochea-we kaa tu utakuja ona miezi si mingi!!!!!!!!!!!! Unajua sababu kubwa?-usoni anawaona wenye pesa lakini atakapoanza hatua za kuingia ndani atashtuka kukuta EL, AC, RA, JK, Kingunge, yusufu,ridhwani, miraji, januari, lukuvi, +orodha ndefu sana!!! atafyata na kunyamaza kimya na ndiyo mwisho!!!!!!!!!!! Usichezee bongo-ndiyo mazao ya laana!!!
Kwani nani ni mgeni kwa pombe????-kwani pombe wa leo na yule wa jana kuna tofauti?????
Haya-sisi wengine yetu macho na kelele kupitia JF!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
48,615
18,546
Prof tiba
walianza wakina magufuli hao hao wa leo hii na tanroads...tunarudisha nyumba zote za serikali akaishia kugawa kwa mdogo wake aliekuwa ameajiriwa just 3 months serikalini
mungu akupe mngojezi kwenye matamshi watanzania ni wabaya sana kwenye kumbukumbu hasa unapofanya kosa;;si vibaya kusema lakini matendo ndio yanayowaaibisha watu..mungu akutie nguvu mama
 

Ndeusoho

Member
Jan 26, 2010
46
5
Kazi bado ni pevu. Maeneo ya wazi ni moja. Huko Sinza na Ubungo kuna waliojenga juu ya njia ya bomba la majitaka na majisafi pia. Tena wengine wameuziwa na watumishi wa wizara yako. Na hili la watu kuishi ju ya mabomba ni la hatari kubwa kuliko hata uvamizi wa viwanja vya wazi. Je unajua juu ya watu waliziba barabara ili wajenge nyumba zao kwa hasara ya ubora wa miji yetu. Nadhani inabidi uwe na ratiba kwa sababu hiyo wizara ni kichaa. Kama huamini bado kidogo utagundua kuwa Master Plan ilikuwa imetenga eneo la kujenga reli toka Ubungo hadi Wazo. Hivi unadhani hizi foleni za kijinga zingekuwepo kama reli hiyo ingejengwa. Kazi unayo lakini nenda kwa awamu kwa vile mengine ni magumu kutokana na kikulacho kuwamo nguoni mwako.
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
48,615
18,546
kazi bado ni pevu. Maeneo ya wazi ni moja. Huko sinza na ubungo kuna waliojenga juu ya njia ya bomba la majitaka na majisafi pia. Tena wengine wameuziwa na watumishi wa wizara yako. Na hili la watu kuishi ju ya mabomba ni la hatari kubwa kuliko hata uvamizi wa viwanja vya wazi. Je unajua juu ya watu waliziba barabara ili wajenge nyumba zao kwa hasara ya ubora wa miji yetu. Nadhani inabidi uwe na ratiba kwa sababu hiyo wizara ni kichaa. Kama huamini bado kidogo utagundua kuwa master plan ilikuwa imetenga eneo la kujenga reli toka ubungo hadi wazo. Hivi unadhani hizi foleni za kijinga zingekuwepo kama reli hiyo ingejengwa. Kazi unayo lakini nenda kwa awamu kwa vile mengine ni magumu kutokana na kikulacho kuwamo nguoni mwako.


yaani in general akifwata masterplan hadi ikulu inatoka pale ilipo
pole mama ilo jitahdi ulinywe kavukavu ndio uongozi
 

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
19
The list continues-atawakuta ben na anna, siti, salama, ongeza na wewe waliosahauliwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!Hizi ni viini macho whereas at the end of the day we are ten years backward in maendeleo-from 12 million maskinis to 15 millions as at 2015!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! We unafikiri kwa nini wamekubali aibu yote ya kuiba kura, ni ili wale-sasa nani ataondoa tonge kwenye midomo yao!!!!!!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom