Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni; aanza kwa kasi!

huyu mama anaahngaika tu mi hata sielewi anachofanya ...atashindwa kazi sasa hivi awaulize wenzake waliotangulia sio anapiga piga makelele tu..aende sinza aone CCM ilivovamia maeneo ndo aje kuuza nyago kwenye TV
 
Jamani kumbukeni Tibaijuka yuko pale kutenda na kutimiza ya yule aliyempeleka, aliyempeleka ni JK, hapa hatuwezi kupata jipya, zaidi ni kwamba ataendeleze yaleyale ya watangulizi wake. Ndani ya CCM hakuna kiongozi anayeweza kutenda yaliyo safi hata kama yeye ni msafi, kwani msingi wa chama chake na wakubwa zake ni michafu na inanuka uvundo.
 
Hmmm...tutaona kama hii si nguvu ya soda maana naona kama ameanza kazi kwa pupa.

Vunja hiki, bomoa kile....kipya kipi hapo? Muda si mrefu huenda naye akaja na siku saba zake...
 
Mama Tibaijuka, Chapa kazi na uonyeshe competence yako. Wizara hiyo imeoza na Watanzania walisha poteza matumaini hususani baadya kuona Magufuri waliyemtegemea kupigwa changa la macho ktk uuzaji wa nyumba za serikali. Watanzania wana matarajio mengi juu yako na ukifanikiwa hapo urais 2015 huooooooooooooooooooooooooooooo! ukatae mwenyewee
 
Utagundua kuwa profssor Tibaijuka anatazamia majibu kwa dr Kikwete. Dr JK aliomba wale wezi wa pesa za EPA ambao hawakuvunja milango wala kufuli za BOT wajisalimishe.

Sasa sijui tuseme haya ni maombi au ni amri.

Teh Teh

ni maombi,mafisadi wakimkodolea macho anatulia kimya.
 
Na mtu nayemiliki VIWANJA VINGI VYA WAZI DAR ni CCM, Maeneo yote ya wazi ni mali yao sasa unategemea nini?

hapa kuna hoja,mama ana anapaswa haichunguze ccm pia. Maana viwanja vingi,parking space nyingi eti mali ya ccm,au umoja wa vijana. Kuna usanii apo!
 
Tatizo nchi hii mtu akiwa kiongozi anafanya lolote analotaka, kwani hata viongozi ngazi ya kata wanauza maeneo yaliyoachwa wazi bila hofu yoyote. Sheria za nchi hii zimegeuka mitaji ya watu, uongozi wa kupeana kindungu umekosa uwezo wa kusimamia sheria.

Tibaijuka hawezi kufanya lolote la maana, kila atakapo gusa atakutana na wakubwa zake au jamaa za wakubwa zake
 
Vema akabomoa ambapo kuna mradi wa kujenga makazi mapya maana fidia ni wazi, kama ni kwa ajili ya sehemu za wazi itakua ni kuwaonea waliojenga maana hawakuzuiwa kujenga. Kuwabomolea bila fidia itakuwa sawa na wa Kilosa waliokumbwa na mafuriko - hivyo sioni kwa nini serikali isiwape fidia. Serikali itakua wamewasababishia hasara na mateso waliokua wanaishi sehemu hizo.

Uzembe wa kulinda hizo sehemu zisijengwe uliletwa na serikali hiyo hiyo ya CCM. Hata hiyo maeneo ambayo CCM ilijichukulia kuwapa fidia CCM itakua ni wizi wa wazi maana wao ndio walikua waangalizi wa mali zetu na badala ya kulinda wakajichukulia.
 
Unaandika nini wewe!
Miji yote Duniani ina maeneo ya wazi. Kwingine hupandwa hata miti ikawa misitu kati kati ya jiji. Inaitwa breathing space.

Sasa wewe unasema eti walinunua kihalali. Hakuna halali hapo. Unaijua sheria yetu isemavyo? Unamjua mtu mwenye uwezo wa kubadili matumizi ya ardhi nchi hii ni nani?

Andika yaliyo na muelekeo. Mtu binafsi huwezi kununua eneo la wazi ukasema eti ni halali. Hata upewe na Rais, ni makosa.

mchunguzi,mimi naongea kutokana na kauli ya mama tiba mwenyewe. Kasema wajanja wametumia mwanya huo kufanya usanii,kama haujamsikiliza ni hekima ukahoji ilikuwaje akanena ivo kuliko kunikolomea kwa usanii ambao mama mwenyewe kasema upo. Labda kama unapinga alichodai prof.Tibaijuka,usikimbilie keyboard chunguza kwanza. Kumbuka Magufuli alitia mkwara kama uo mwanzoni alipochaguliwa na mkapa,alipochunguza akakuta viongozi waandamizi ndo wana ekari mpaka 800 kule kibaha na mkuranga. Naye akalalama kama mwenzio kwa kusema tu" wizara niliyopewa ni ngumu". Weka kumbukumbu mkuu,mafisadi wamo umo umo serikalini. Mkuu jina lako lina maana kwa kihaya na kiswahili,kwa kiswaili ni direct mchunguzaji,sasa mbona hufanyi ivo? Maana nyingne kwa lugha ya kwenu ni kurudisha vitu vilivohuzwa kwa uhuni au kisanii,'kuchungura'. Mbona sasa jina lako liko makini lakni unanjibu kisanii?
 
Lets wait and see
Well said kazin

I think we have bigger problems kwa sasa kama watanzania kuliko viwanja vya bichi ambayo havigusi hata silimia 0.05 ya watanzania... kama huyu mama anafanya kazi kwa media, basi na yeye ataangukia pua ileile ya ritha mlaki

Binafsi ningetegemea mama atulie, asome ramani ya nchi yake, aje atueleze national human settlement strategic plan hata ya miaka mia na kama hawezi aombe wadau

Tuna matatizo ya mitaro, urban plan with infrastructure plans kwa kila miji na vitongoji, mabadna kwenye njia za kiusalama na mizunguko ya hewa nk.

Kila wilaya kwa sasa kuna uvurugaji wa mpango mji sasa akikomalia media ataaibika

nasikitika sana
 
Nilimsikia Mama akiongea jana, i could not believe kama yeye anaweza kuongea vile. Yaani the way she talks huwezi amini ni Waziri coz hakuwa anapangilia maneno yake, anarudia rudia vitu huoni "authority" katika alichokuwa anaongea....mmmhh sijui. Huyo ni Prof nasikia. May be she is organised when in English lakini jana mmh, sijui wengine kama mlimsikiliza...
 
Kwa kawaida yetu watanzania si mda mrefu tutamuona huyu mama mbaya na huwa hafikirii yale ayafanyayo
Ngoja tusubili.
 
Huyu mama amekuja kujiharibia cv yake kwa hii serikali ya Mkwere!
 
Jamani kumbukeni Tibaijuka yuko pale kutenda na kutimiza ya yule aliyempeleka, aliyempeleka ni JK, hapa hatuwezi kupata jipya, zaidi ni kwamba ataendeleze yaleyale ya watangulizi wake. Ndani ya CCM hakuna kiongozi anayeweza kutenda yaliyo safi hata kama yeye ni msafi, kwani msingi wa chama chake na wakubwa zake ni michafu na inanuka uvundo.
Tutaona kama anaweza nyang'anya mtu aliyeko madarakani kiwanja.. sanasana wataishia kuwafuata watu walitoka zamani madarakani. Sio kwamba watu walivamia, ila walikuwa wakiuziwa na maafisa wa ardhi pale wizarani. Angeanza kushughulika na hao maafisa wa wizarani kwanza. Inatushangaza mpaka sasa hajaona huozo pale wizarani!
 
Enzi zile tulifundishwa kwenye skuli zetu kwamba:
1.Bbinadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
2. Cheo ni dhamana
3. Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa
4.

Nadhani chama kilichoko madarakani ambacho ndicho kiliasisi mafundisho hayo hapo juu kitengeneze kanuni zingine, kwa mfano:
1. Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe (wana support ya maandiko matakatifu kwenye hili)
2. Penye udhia penyeza rupia
3. Ujanja kuwahi na kupata
4.

Muda si mrefu Professor ataomba ulinzi wa JWTZ maana police kwa sasa ni walinzi wa Mafisadi
 
Na pale Palm Beach nasikia wajanja wameshaweka uzio. Mwisho jiji lote la DSM litafanana na Bombay, no open space.

Jasusi,salaam! Pale palm beach mama Tibaijuka kasema wabomoe tangu jana,amekariri kuwa mkapa alishafuta umiliki wa space ile. Kwa pale nakubali katoa msimamo kuwa waanze kuvunja ukuta ule,ila ilikuwa aibu mwarabu yule ana jeuri.
 
Kwa kawaida yetu watanzania si mda mrefu tutamuona huyu mama mbaya na huwa hafikirii yale ayafanyayo
Ngoja tusubili.
i think she needs to come up with a comprehensive plan kuliko crisis management... she ahs five year to work so crisis management itamchosha hata kabla ya june mwakani
 
Nilimsikia Mama akiongea jana, i could not believe kama yeye anaweza kuongea vile. Yaani the way she talks huwezi amini ni Waziri coz hakuwa anapangilia maneno yake, anarudia rudia vitu huoni "authority" katika alichokuwa anaongea....mmmhh sijui. Huyo ni Prof nasikia. May be she is organised when in English lakini jana mmh, sijui wengine kama mlimsikiliza...

nilimsikia prof.utadhani aidha ana mdahalo au anamkomoa mtu,yani full kujirudia rudia. Na alivovaa na kitambaa kichwani basi ungedhani ni mpita njia anahojiwa. Simchukii mama ila huo ndo ukweli. Labda atatulia maana ata sku mia bado ktk uwaziri wake.
 
Back
Top Bottom