Prof. Shivji ni mwalimu wangu pale Udsm na mimi ni miongoni mwa wale wanafunzi wabishi, waliobishana hadi na walimu wao!.
Baadhi ya tofauti tulizotofautiana na mwalimu wangu ni Prof. Shivji anakubali kuwa the end justifies the means, mfano Muungano ni halali na katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977 ni katiba halali hata kama njia zilizotumika sio halali!.
Kisheria, jambo likishafanyika ndivyo sivyo, huwa linakuwa halipo, tukiita "ab initio". Kupitia somo la sifa za mikataba, contacts, hati za muungano sio mkataba bali ni makubaliano tuu.
Pili kwa vile makubaliano hayo hayakuridhiwa na Baraza la Wawakilishi, then kiukweli kabisa bila mashaka wala kumung'unya maneno, " Muungano Si Halali" ab initio!. Vivyo hivyo kwa katiba yetu hii iliyopo sii halali kwa msingi kwa katiba iliyoundwa bila kufuata principles za constitutionalism sio constitutional halali!.
Kwenye somo la jana akielezea sifa za wajumbe wa tume ya kukusanya maoni alisisitiza wasiwe wanasiasa!. Hivi waliojaa mle ndani ni kina nani tukianzia kwa Jaji. Warioba!.
Kwa maoni yangu, Prof. Issa Gulamhusein Shivji ndiye aliyepaswa haswa kuwa mwenyekiti wa tume ile!.
JK aliogopa kumteua huyu jamaa kwa sababu ni mkweli mno hivyo angeweza kutupatia katiba nzuri ya kuikweli ambayo CCM ingepigwa chini hata kabla ya uchaguzi!.