Prof Shivji na mihadhara ya katiba ITV

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Wakuu jana nimeangalia mhadhala juu ya katiba ulioendeshwa na Prof. Shivji kupitia ITV, lazima nikiri mzee huyu mbali ya kuwa na weredi wa kupindukia kwenye medani ya sheria na katiba ni mzalendo wa kutukuka. Anaelimisha vizuri sana suala zima la maana na umuhimu wa katiba, historia ya katiba, mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

Jana ilikuwa kipindi cha pili mhadhala utaendelea tena jumatano saa tatu kamili usiku, ni live itv. Fuatilieni wakuu.
 
Huyu ni katika wale wachache, kipenzi cha Mungu, hajui unafiki, anatoa yote kwa moyo wa kizalendo. Na anastahili heshima kweli. Ameelezea bunge la katiba, linavyopatikana na historia ya katiba ya Tanganyika na Tanzania. Sikuambulia pa kumkosoa. Nafikiri kipindi kinahitaji yafuatayo
1. Kiendelee wakati wote wa mchakato wa katiba
2. Kiongezewe masaa hadi mawili
3. Tume yenyewe ipewe semina na Huyu proffesor
4. Tumtafutie Tuzo kubwa huyu proffesor.
 
Kipindi cha kwanza nilikiona mzee yuko deep na anajua alichokuwa anafanya!
Alituasa tusipo itikia wito katiba itaundwa na wachache ili kuja kuongoza majority!
 
Ni ukweli usiofichika kuwa Prof. Shivji amebobea katika fani yake. Wasiwasi wangu ni kuwa je watawala wanafurahia mihadhara hii?
 
Wahindi woote wangekuwa hivi tungekuwa mbali.
HAKIKA NI MZALENDO
HANA PUNJE YA UNAFKI.
 
Hivi kwa nini huyu Profesa hakuteuliwa kwenye tume ya Warioba? Huwa najiuliza sipati jibu.

Sio mbaya, ila apewe vipindi vingi sana kuelimisha umma. Huyu mle ndani ya tume, asingeweza kuelewana na wajumbe. Huyu anatakiwa kutoa semina kwa wajumbe wa tume na bunge. Kurekebisha mambo fulani fulani. Hasa wabunge wa CCM ambao wameonyesha upeo wa chini katika masula ya kutunga katiba.
 
Wakuu jana nimeangalia mhadhala juu ya katiba ulioendeshwa na Prof. Shivji kupitia ITV, lazima nikiri mzee huyu mbali ya kuwa na weredi wa kupindukia kwenye medani ya sheria na katiba ni mzalendo wa kutukuka. Anaelimisha vizuri sana suala zima la maana na umuhimu wa katiba, historia ya katiba, mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

Jana ilikuwa kipindi cha pili mhadhala utaendelea tena jumatano saa tatu kamili usiku, ni live itv. Fuatilieni wakuu.

Nasikia vitakuwa vipindi vitano tu, nawashauri ITV watengeneze DVDs nyingi za mihadhara hiyo na kuziuza kwa bei poa kwani ni rejea muhimu sana kwa wanaopenda kuijua katiba na ambayo haiwezi kupatikana kokote kwingine.
 
Hapana, ITV wamuombe Prof kuendelea na maada mbalimbali za katiba. Hili la DVD sawa lakini ni kwa wachache sana. Sasa wabuni mkakati wa Radio one na Prof shivji. Waacheni TBC walale.
 
Wakuu jana nimeangalia mhadhala juu ya katiba ulioendeshwa na Prof. Shivji kupitia ITV, lazima nikiri mzee huyu mbali ya kuwa na weredi wa kupindukia kwenye medani ya sheria na katiba ni mzalendo wa kutukuka. Anaelimisha vizuri sana suala zima la maana na umuhimu wa katiba, historia ya katiba, mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

Jana ilikuwa kipindi cha pili mhadhala utaendelea tena jumatano saa tatu kamili usiku, ni live itv. Fuatilieni wakuu.

Mkuu tunashukuru sana kwa taarifa, pia kutokana na maendeleo ya IT, siku hizi ingekuwa ni kusaidia jamii kama unge-record na ku-post youtube kwa wale waliokosa mijadala iliyopita au ambao hawana access na ITV kwa sasa (Wapo out of scope of ITV)
 
jibu ni kwamba ccm na ukweli ni mafuta na maji havichanganywi

Kweli, nakumbuka hata wale wanafunzi wake waliopo bungeni, baadhi walimkejeli. Corruption despair rational decision making. Haki na rushwa ni kama maji na mafuta. Lakini hata hao CCM hawaelewi kitu, wanahitaji shule kutoka kwa Prof. Wakielewa kidogo tu watabadilika.
 
wazanzibar nao! eti mzanzibari!
Kwani kuna tatizo gani akiwa mzanzibari? Sisi hatuangalii mzanzibari, tunaangalia mtanzania!
Maana nyie kila kitu mzanzibari wy?.
 
Back
Top Bottom