Prof. Shivji: Kwanini zoezi liwe la haraka kuwahamisha? Ni kweli Wamaasai wameshirikishwa?

ALT

Member
Oct 6, 2021
78
90
Heri ya siku kuu na mapumziko,

Nikiwa nafatilia ITV leo katika kipindi cha Dakika 45, profesa shifji kajadili mambo mengi, ika mimi naleta la wamasai kuhamishwa Ngorongoro.

Anasema mwaka 1958 walihamishwa kutoka serengeti kwenda Ngorongoro kwa ahadi ya kutokuja kuhamishwa tena na serikali ya kipindi hicho ya kikoloni. Hii ilikuja baada ya serengeti kutangazwa hifadhi ya kitaifa.

Anaendelea kusema kwamba, kuhusu wamasai kutengewa eneo maalum kuhamia uko, anahoji ni kweli wameshirikishwa? Maana anaona baadhi wanasema hawajashirikishwa huku baadhi wakikiri kushirikishwa.

Juu ya hoja ya hifadhi kuhofiwa kutoweja kwa ongezeko la watu, anahoji basi mamlaka zinyumbue.

Kati ya watu walioongezeka, tujue wamasai ni wangapi na wasio wamasai ni wangapi. Anaamini si kweli walio ongezeka wengi ni masai.

ANAMALIZIA KWA KUHOJI, "KWANINI ZOEZI LIWE LA HARAKA? KWANINI LISIPEWE MUDA KUFANYIKA KWA IFANISI?

Kwa mtazamo wangu, naona kuna kitu hakiko sawa. Profesa kasema kazunguka Tanzania nzima miaka hiyo ili kuishauri serikali juu ya maswala ya ardhi.

KUNA HARUFU MBAYA YA UOZO KWENYE HII PROJECT.

TAZAMA VIDEO YAKE HAPA

Naendekea ku u crop itapanda punde

Updates...

Hii simu ninayotumia( samsung galaxy) hainipi option ya ku crop video walau iwe ya dakika moja, maana ni dakika tatu na ushee ni ni mp4 yenye ukubwa wa mb 480. Mwenye clip fupi ashee haoa, zaidi nime screen shot picha tu.

VideoCapture_20220502-223206.jpg
 
Huwa namuelewa sana Prof Shivji, niseme tu issue ya Ngorongoro kuwahamisha wa masai ni wizi mtupu ni vile watanzania wengi ni wapole hawatakagi kupambana ama kupambania haki zao.

Zoezi lipewe muda watu waeleweshwe hasara na faida Kisha maamuzi yafanyike.
 
Acheni uonevu wa kuwapuuza wazawa kwa maslahi na anasa za waarabu na wazungu. Loliondo ni makazi ya wamasai na wanyama. Waachwe waendelee mpaka nature itakapoamua vinginevyo.
 
Shivji ni Profesa mnafki,mwoga na asiye na msimamo. Tangu enzi za kutafuta katiba mpya niliacha kusikiliza wala kusoma habari inayohusu Shivji. Hata hii sijaisoma maana najua akipewa chochote atabadili msimamo
 
Huyu Professor alipewa deal kufanya utafiti kuhusu mpango wa Ardhi nchini akiwa na wabobezi wenzake katika tasnia ya sheria wakaandika taarifa Yao na vitabu vingi vya kufundishia pamoja na mswada wa sheria vikapita bila kupingwa na kupigiwa makofi mengi.

Matokeo yake tunayo hakuna haja ya kuvaa miwani kuona kama matatizo ya Ardhi yalipatiwa ufumbuzi au la

Hawa wasomi Wetu wanamchango mkubwa Sana Kwenye matatizo tunayoyapata sasa.

Wametuachia laana kwenye elimu za Ngazi zote bila hivyo tungepata wanazuoni wenye kuweza kufanya utafiti na kuyapatia ufumbuzi mambo mbalimbali yanayoikabili nchi yetu.

Shida kubwa ni Elimu katika nchi hii mfumo wa utoaji elimu umegubikwa na Unyonyaji,upendeleo,Rushwa,udanganyifu,uonevu,Utendaji na uzandiki hali inayopelekea Wanafunzi Wetu kufuzu kile kilicho nje ya matarajio yetu na kuzalisha walimu wa hovyo mno.
 
Watawala hawaoni aibu kuwafurahisha mabeberu kwakua wanajua hapa pakiwashinda watakimbilia kujificha huko walikoweka fedha zetu walizozificha kwa kutuuza.
 
  • Thanks
Reactions: ALT
Hebu wahame, hiyo hifadhi inaingiza mabilioni yanayosaidia taifa. Unakaaje sehemu ambayo huruhusiwi kujenga nyumba? Huruhusiwi kulima
 
Hebu wahame, hiyo hifadhi inaingiza mabilioni yanayosaidia taifa. Unakaaje sehemu ambayo huruhusiwi kujenga nyumba? Huruhusiwi kulima

Watalii wengi wanapenda kuoba utalii wa wanadamu waishio na wanyama pori. Nadhani wamasai wanachochea sana kua kivutio katika hiyo hifadhi.
 
Huyu Professor alipewa deal kufanya utafiti kuhusu mpango wa Ardhi nchini akiwa na wabobezi wenzake katika tasnia ya sheria wakaandika taarifa Yao na vitabu vingi vya kufundishia pamoja na mswada wa sheria vikapita bila kupingwa na kupigiwa makofi mengi.

Matokeo yake tunayo hakuna haja ya kuvaa miwani kuona kama matatizo ya Ardhi yalipatiwa ufumbuzi au la

Hawa wasomi Wetu wanamchango mkubwa Sana Kwenye matatizo tunayoyapata sasa.

Wametuachia laana kwenye elimu za Ngazi zote bila hivyo tungepata wanazuoni wenye kuweza kufanya utafiti na kuyapatia ufumbuzi mambo mbalimbali yanayoikabili nchi yetu.

Shida kubwa ni Elimu katika nchi hii mfumo wa utoaji elimu umegubikwa na Unyonyaji,upendeleo,Rushwa,udanganyifu,uonevu,Utendaji na uzandiki hali inayopelekea Wanafunzi Wetu kufuzu kile kilicho nje ya matarajio yetu na kuzalisha walimu wa hovyo mno.

Jana kakiri, wasomi wengi akiwepo yeye hawajafanya sehemu yao ya kutatua changamoto za wananchi wengi walio maskini.
 
Back
Top Bottom