Prof Shivji: Katiba mpya siyo mwarobaini wa matatizo ya watanzania

Wewe machaga, matakwa ya watu huwa yanaheshimiwa kwa shinikizo la watu kwa umoja wao.

Marekani wana katiba bora sana, mbona kuna mambo kufanyika mpaka waandamane. South Afruca ni vile vile na Kenya.

Hivi mnafikiri katiba inashika bunduki na kutishia watu wafuate matakwa ya watu?

Haya COVID-19 wako bungeni kinyume na katiba hii hii mbovu, mmefanya nini ?

Kila mtu anataka vitu vizuri akiwa amekaa amekunja nne, anakunywa wine.

Haya, Hata hiyo katiba mpya ikiwa unavyotaka, ikivunjwa makusudi mtafanyaje ?
Nadhani uelewa wako wa mambo ni mdogo. Katiba ikiwa nzuri haiwezi kutoa nafasi ya kuvunjwa na anayeivunja akasalimika. Akitokea rais mshenzi kama Magufuli akakatiza mikutano ya vyama kwa ujinga na woga wake, mahakama na bunge vitamuwajibisha kwa sababu katiba imeviweka huru. Hii katiba tuliyonayo inawafanya wabunge na majaji wamtii rais kwa sababu ndiye bosi wao.
 
Kwa hiyo, unataka kusema nchi ikiwa na katiba mbaya ndiyo inayofanya vizuri? Soma Katiba Inayopendekezwa (na Tume ya Warioba) utaona imetoa mwongozo gani kwa wabunge wasio 'perform'.
Nimekuuliza maswali unaniletea ngonjera. Eti nirudi kwenye rasimu, what is rasimu?? Si ni mikaratasi tu!

Taja hizo nchi zenye katiba nzuri na zinafanya vizuri
 
Huyo shivji kasaidia nini nchi mbali na kufundisha wanafunzi wanaopita tu UD

Bora hata kezilahab
 
Huyu mzee anazeeka vibaya. Kwahiyo mwarobaini ni katiba mbovu inayobinya demokrasia? Kwani yeye nani?
 
Halafu haya ni maelezo ya mleta thread. Nina uhakika profesa alizungumzia hili jambo kwa muktadha mwingine lakini hawa wakageuza. Hawa wengi wao ni wachumia tumbo wanaonufaika na mfumo huu wa kubebana na wanajua mambo yakibadilika hawawezi kupata tena vya bure.

Nawajua vizuri huwa ni mabingwa wa kubadili maana, ili kubeba matamanio yao.
 
Naona maana ya mfumo wa vyama vingi vya siasa haueleweki kabisa kwa Watanzania wengi. Kwao ni bora tungebaki na CCM tu huku tukiomba Mungu tupate viongozi wanaowajibika toka kwenye chama hicho!

Hawaelewi kuwa wanasiasa huwa makini pale wanapojua kuwa wasipowajibika basi mfumo makini utawaondoa madarakani kupitia kwenye uchaguzi halali. Wananchi wengi watawapigia kura ya hapana na kutoa fursa kwa wengine kufanya kinachotakiwa. Nao wakishindwa wanaondolewa hivyo hivyo. Inapofikia wananchi wanaweza kuwajibisha wanasiasa kupitia sanduku la kura, basi kuanzia Rais na Bunge umakini huwa wa hali ya juu.

Nguzo kuu za mfumo huu wa vyama vingi ni katiba sahihi inayohakikisha uwepo wa Tume Huru ya uchaguzi, Bunge huru na mahakama huru. Bila hivyo mnabakia na udikteta wa dola na maendeleo ya propaganda.

Haya madai ya kwamba wanaodai katiba mpya wana uchu wa madaraka yanatolewa na Wanapropaganda wa chama tawala kuonyesha vyama vya upinzani ndivyo vyenye uchu wa madaraka si CCM! Lengo ni kuhakikisha CCM inaendelea kuwa madarakani kwa udikteta wa dola bila kutishiwa na challenge ya kutolewa hata ikiharibu kiasi gani.

Inashangaza unakuta hata wadau wanaoheshimika kwa michango yao hapa JF wanapiga debe hiyo bs. Sisi tusahau kabisa habari ya maendeleo for good; tuendelee na propaganda za kuabudu viongozi.
 
Naam, Mtu yeyote anayetaka yaliyofanywa na Mwendazake yaendelee anafanya kazi ya shetani. Ukiwa na hofu ya Mungu hauwezi kusapoti ufedhuli huo. Kama unajiamini kwa nini uogope katiba inayotoa haki ya ushindani sawa? Hawa wapizani wakikubali kwenda kwenye uchaguzi kwa katiba hii hii, basi turudi tu kwenye chama kimoja.
Wanafahamu fika kuwa bila kufanya ufedhuli kwenye box la kura hawatoboi
 
M
Msomi nguli wa Tanzania Prof Issa Shivji amelichambua dai la katiba mpya na kusema halina tija wala si mwarobaini wa matatizo yanayowakumba watanzania kwa sasa.
Prof Shivji amesema wanasiasa wanapenda madaraka na siyo siasa safi na kuwatumikia wananchi, ametolea mfano kwa vita ya madaraka inayoendelea nchini Kenya na Afrika Kusini licha ya kubadili katiba mara kwa mara.View attachment 1838690

Mkuu,
Badala ya screaming headline, ungetuletea article nzima.
 
Msomi nguli wa Tanzania Prof Issa Shivji amelichambua dai la katiba mpya na kusema halina tija wala si mwarobaini wa matatizo yanayowakumba watanzania kwa sasa.
Prof Shivji amesema wanasiasa wanapenda madaraka na siyo siasa safi na kuwatumikia wananchi, ametolea mfano kwa vita ya madaraka inayoendelea nchini Kenya na Afrika Kusini licha ya kubadili katiba mara kwa mara.View attachment 1838690
Sina hakika haya ni maoni ya Issa Shivji labda iwekwe sauti ya mahojiano.

Maana mtaji wa ccm umebaki ni uongo na propaganda.

Hii ni kampeni chafu na uongo mtupu

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom