Zambia Malawi kuna reli inajengwa tokea Beira kwa taarifa tu baada ya kuchoshwa na unyanyasaji DarNi vyema tujitahidi sasa kuishi kwa faida ya watu wetu kama USA, kuwepo kwetu kwenye hizi jumuiya kuwe kwa faida ya watu wetu na sio kuishia kwenye makongamano, warsha, vikao nk.
Malawi, Zambia, Botswana ni land locked, hebu tutumie fursa yetu yakuwepo SADC kuboresha reli ya Tazara na kujenga KONTENA TERMINAL kubwa pale Tunduma na KONTENA zao zote zifike pale kupitia reli. Wanapoagiza mizigo yao kutoka Nje kupitia shirika lolote la Meli kuwe na Connection ya moja kwa moja KONTENA zipokelewe Tunduma na kila kitu kifanyikie pale na Dar es salaam port iwe transit port na pale Tunduma iwe destination port. Mizigo ya DRC hasa Katanga province yote itaishia kwenye hiyo terminal..
Hicho pia kinaweza fanyika Kigoma na Bukoba, Unajenga Kontena terminal kubwa na zinakuwa destination port kwa mizigo ya DRC hasa Kivu, Bukavu nk, Wanyarwanda na Waburundi pia watachukulia Kontena zao straight kwenye hizi terminal.
Miji ya MBEYA, TUNDUMA, KIGOMA NA BUKOBA Itkauwa Centre of business na mzunguko wake utakuwa mkubwa, kipato cha wakazi kitakwenda juu, watu watapata ajira nyingi, mikoa hiyo itaendelea kwa kasi, Dar es salaam Msongamano utapungua lakini pia Bandari itakuwa busy na mapato kuongezeka.. VERY SIMPLE IDEA TUJARIBU KUWA WABINAFI WA TAIFA LETU.