Prof. Palamagamba Kabudi atangaza Tanzania kuwa M/Kiti na mwenyeji wa mkutano 39, wa SADC

nimecheka sana niliposoma jana mahala eti tunawakaribisha wawekezaji toka Rwanda...imagine?

aisee hii nchi inakoelekea siko kabisa!
Kwa akili yako wewe muwekezaji ni nani?

Yani mzungu alitutawala a kaondoka na akili zetu kiasi kwamba hata vijana waliozaliwa juzi nao akili zao zilishaondoka na mzungu!

Kwamba kwako wewe muwekezaji ni mzungu tu kutoka ulaya basi.

Akili kisoda hizi.
 
Sasa Kabudi anashuka na history ya kuanzishwa kwa SADC, ilianzishwa na Mwalimu Nyerere baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

P

Haaahaaa ningeshangaa kama asingetoa historia na methali za hapa na pale. Ukimsikiliza kabudi sio kiongozi wa mawazo mapya bali ni mtu wa historia na amejikita kwenye propaganda zaidi. Kila akiongea na watu anadhani hawajui lolote kuhusu hayo mambo hivyo hujikuta anatoa historia na kuishia kwenye vitisho visivyo na tija. Hapo piga ua, lazima amuongelee Magufuli kama rais bora kwenye hiyo jumuiya na wengine wote wanapaswa kumuiga yeye. Hizo ndio sifa za siasa za tumbo.
 
Kwa akili yako wewe muwekezaji ni nani?

Yani mzungu alitutawala a kaondoka na akili zetu kiasi kwamba hata vijana waliozaliwa juzi nao akili zao zilishaondoka na mzungu!

Kwamba kwako wewe muwekezaji ni mzungu tu kutoka ulaya basi.

Akili kisoda hizi.
hahahaaaa... maji yanapanda Mt Kilimanjaro siyo?

Bashite bana!
 
Press Conference imeanza kwa intro kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.

Kwenye utambulisho,
Waziri Kabudi, amemtambulisha, Emanuel Buhohela ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari, Wizara ya Mambo ya Nje.

P
Sikuwahi kujua hapo kabla km mtumishi Junior Private anaweza kuteuliwa kwenye post ya Mkurugenzi serikali
 
Ndio maana tunabaki masikini kwa kutegemea kwamba mzungu ndio atakuletea ajira bila kuangalia kwamba hapo hapo ulipo kaa kuna fursa za ajira. Pumbavu Kabudi sana
hahaaaaaa... naona unawaita kina Kabudi.

mimi siyo masikini by the way - thanks to FDI kutoka magharibi kabla ya awamu ya kipumbavu haijaingia madarakani.
ila kwa mwendo huu wa sasa wa ki-Kabudikabudi tusipofanya kitu October 2020 lazima nitaingia kwenye bracket ya umatonya aisee - na sitakubali!
 
Sasa ni kipindi cha maswali na majibu.
Maswali yameulizwa na waandishi 5.
Kabudi anaanza kujibu.
P
 
Haaahaaa ningeshangaa kama asingetoa historia na methali za hapa na pale. Ukimsikiliza kabudi sio kiongozi wa mawazo mapya bali ni mtu wa historia na amejikita kwenye propaganda zaidi. Kila akiongea na watu anadhani hawajui lolote kuhusu hayo mambo hivyo hujikuta anatoa historia na kuishia kwenye vitisho visivyo na tija. Hapo piga ua, lazima amuongelee Magufuli kama rais bora kwenye hiyo jumuiya na wengine wote wanapaswa kumuiga yeye. Hizo ndio sifa za siasa za tumbo.

Wewe umemwelewa vilivyo. Siku zote kila aliyeko mbele yake ni mtu wa kufundishwa!
 
Swali la Kwanza lilitoka kwa Abdalah Idrissa Majura, amezungumzia timu ya Taifa imeondoka kinyonge, amejibiwa kesho Spika kesho anaongoza timu ya wabunge kwenda Misri kuishangilia Taifa Stars.

P.
 
Swali la pili lilitoka kwa Balile, aliuliza kuhusu mambo ya jalalani, amejibiwa, akasome mistari fulani ya Bibilia. Kumbe Kabudi ni mtoto wa Rev. Canon Aidan Mwaluko Kabudi.
P.
 
Tena Mkurugenzi wa ITV/Radio One, Joyce Mhavile, na Mhariri Mkuu, Stephen Chuwa, wapo.
ITV ni chungu cha kupika vipaji, kuanzia Betty Mkwasa, Godwin Gondwe, Charles Hillary, Susan Mungi, Ahamed Kipozi, Aboubakar Liongo, Millard Ayo na wengine wamepikwa ITV/Radio One.
P
Kwahiyo ITV/RADIO ONE ni Chuo cha Habari?
 
Swali la tatu lilitoka kwa Scolastika Mazula,
wataunda a task force, ya waandishi ambao watapigwa msasa hadi waive.
P.
 
Wanabodi,
Niko hapa ukumbi wa JNCC, kuhudhuria press conference ya Waziri Kabudi.

Karibuni

Paskali.

UPDATE
Press Conference imeanza kwa intro kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.

Kwenye utambulisho,
Waziri Kabudi, amemtambulisha, Emanuel Buhohela ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari, Wizara ya Mambo ya Nje.

Pia Prof Kabudi, amejitambulisha kama mwandishi wa habari, na akawashukuru waalimu wake 4, waliomfundisha uandishi wa habari, ambao tuko nao hapa, hawa ni Wallece Maugo, James Mpinga, Richard Mngazija na Henri Muhanika.

Pia akataja waandishi wenzake kina Dr. Harison Mwakyembe, Dr. Mlimuka, wote walikuwa waandishi wakatimkia kwenye sheria.
Huyu mzee sijui Nini kimetokea

Naona ummat Muhammad umeamua kumuona ndivyo-sivyo
 
Back
Top Bottom