Aliyekupa wewe na familia yako ni Mungu, usitutoe thamani sisi watoto wa wakulima na wavuvi. Mshukuru Mungu wewe ni mboga saba.
*Tunasomeshwa kwa tabu ada ya A'level mpk wazazi wanashindwa. Wazazi wetu hawawezi kutulipia ada ya vyuo, tukikosa mikopo tutakosa elimu.
*Taifa linahitaji wasomi hata kama watakuwa wengi.
Huyo mama mwezio naogopa kuchangia mana, wizara imemshinda mpaka bas anajikubali mwenyewe na uprof, tatizo Elim hapimwi kwa ubunifu bali kwa kukalili, alishindwa Kaz ndio alijiuzur huu mwaka unaisha sector ya Elim haieleweki, Mara hatua 2 mbele tatu nyuma daahaa cjuwi lkn
Mkuu kuna hulka nyingine kwenye bongo zetu wanadamu ni rahisi sana kurecord na kukumbuka mabaya na kuyatumia kuconclude jambo na wepesi wa kuyasahau mazuri,narudi tena na mfano wa family pattern,hata kama mume au mke atatenda mema kwa kiwango gani,linaweza kutokea baya moja na mke au mume huyo ambaye amekuwa akienjoy mazuri ya mwenzake na baya hilo hilo akalitumia kuconclude kuwa mwenza wake hafai bila hata kurejea ya nyuma,ila wakati ndio ufumbuzi wa reality,ni mapema sana kusema kashindwa na mwisho wa siku asilimia kubwa ya watakaoweka ushabiki pembeni watamkubali.Hapana Mkuu
Huyu kaisha shindwa
Kama hotuba yake ya leo madudu kabisa
Rais anajiaifu kunyima watoto wetu mikopo sababu tu wamesema private schools?
Why hasemi tu ukweli kama HAZINA ni nyeupe?
Mnamlaumu sana huyu mama lakini unamlaumu yeye kwenye issue ya mikopo wakati Serikali kuu ndio inapaswa kutoa fungu kwa ajili ya mikopo,unamaanisha kwamba yeye ndio amegoma kutoa fedha ?Hahahaa, hilo nalo neno.
-Kaveli-
GPA imebadilikaje sijaelewaHapo kwenye GPA 3.0 si mmepewa takwimu juzi tuu kwamba kila wa watatu wanne ana hewa kichwani. Sasa watatowa wapi wakufikia GPA 3.5?
Kwani hujasoma taarifa za serikali walishusha from 3.5 to 3.0 kama wamepandisha tena hizo taarifa sina.GPA imebadilikaje sijaelewa
Jamaa linakera sana2020 huyu hawezi shinda
Kuna watoto mm nawajua wamesomeshwa private schools na makanisa na misikiti
na Taasisi hizi za dini zinajitoa ukifika form 6 sababu wanajua serikali itatoa mkopo!
Magufuli kaisha shindwa,imebaki porojo tu
Ndalichako hakuishindwa NECTA ila siasa ndo zilifanya awekwe kando.Huyu mama NECTA kulimshinda akaondoshwa.
Wizi wa mitihani
Upendeleo
Uliua kabisa morali ya wanafunzi.
JK alimuondoa....kwani alishindwa.
Sasa tumempa mzigo mwengine...hauwezi
Nilihuzunishwa sana na lile agizo alilotoa la kutaka wanafunzi wote wa O- level wasome masomo ya sayansi. Taifa linapata hasara mbili:
1. Wanafunzi hao wengi wanaokataa masomo ya sayasi wana uwezo mdogo sana! Kuwalazimisha wasome masomo tisa au kumi ni kuwatwisha msalaba mzito kuliko aliobebeshwa Yesu. Hivyo tutarajie daraja sifuri kuongezeka in geometric progression.
2. Serikali itatumia gharama kubwa wakati wa mitihani. Hii ipo hivi:
a) Mitihani itafanyika kwa siku nyingi zaidi hivyo gharama za usimamizi zitaongezeka. Ikumbukwe kwa sasa mitahani ya kitadato cha nne inamalizika wiki ya kwanza kwa kuwa inafanyika kwa siku saba.
b) sambamba na (a) hapo juu, pia gharama za usimamizi zitaongezeka.
c). Serikali itatumia gharama kubwa kuandaa mitihani ya sayansi. Hii ipo hivi:
(i) kutakuwa na ongezeko la ghaarama za kuchapisha na kusafirisha mitihani.
(ii) gharama za kununua vifaa vya sayansi zitaongezeka. Hii itaanzia gharama za kununua vifaa na kemikali za mazoezi, na wakati wa mitihani husika.
Swali la msingi, JE KUNA HAJA GANI YA KULIPIA GHARAMA ZISIZO NA TIJA???
Ni vyema waalimu wangepewa 'mamlaka' ya kuwashauri kwa juhudi zao zote wanafunzi wenye uwezo wa kusoma masomo ya sayansi, ndio wasome masomo ya sayansi.
Nahisi waliomshauri Waziri ni wale wanaonyenyekea vyeo na kuogopa kuonekana wanam-drive waziri.
Tukumbuke ya kwamba serikali inatoa harama za Elimu Bure kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo shule husika, na fungu hilo haliongezeki lulingana na mahitaji ya ziada yatokanayo na 'matamko' ya viongozi.
Sitarajii tija kubwa katika Elimu zama za Elimu Bure.
Huyo mama mwezio naogopa kuchangia mana, wizara imemshinda mpaka bas anajikubali mwenyewe na uprof, tatizo Elim hapimwi kwa ubunifu bali kwa kukalili, alishindwa Kaz ndio alijiuzur huu mwaka unaisha sector ya Elim haieleweki, Mara hatua 2 mbele tatu nyuma daahaa cjuwi lkn
We mwenyewe ushajitambua? 'kilio chako' ni cha nini?
Sasa twende kwenye point:
1. Culture ipi hiyo? kuwa specific.
2. Universal minimum entry qualification into University, ni ipi?
3. Amefanya kazi kwenye sector ya elimu kwa muda mrefu, shida na matobo yote ya elimu yetu anayajua vyema. Ghafla kupandisha GPA to 3.5, then ghafla kushusha to 3.0... sio kukurupuka huko?
4. Serikali ifute Loan??!! are you serious? nchi hii wananchi maskini ndiyo the majority kuliko wenye uwezo. Hata huko developed countries kwenyewe, wanatoa Students Loan grants. Acha kuandika kama vile huna kichwa. Si ajabu wewe mwenyewe ulisoma kwa huo huo mkopo, leo hii unatapika uharo wako hapa eti Serikali ifute Loan.
5. Kwenye inshu ya kupunguza uzazi, una hoja. Kwamba watu wanafyatua tu watoto kwa wingi wakati wazazi hawana uwezo hata basic needs tu. Ndiyo maana kuna baadhi ya nchi, mfano Finland, elimu ni completely FREE kabisa hadi University! coz wana population ndogo sana.
Lakini kwa upande mwingine, ishu ya population is immaterial in this regard. Tujiulize, kuna nchi nyingi tu za kiafrica zenye uchumi na population kama Tanzania, why wao serikali zao zimeweza kusomesha (by loan) wananchi bila migogoro? Lakini education sector ya Tanzania ni kama gari bovu!
Mimi binafsi, naamini mambo yafuatayo (by serikali) ndiyo yanakwamisha Taifa hili:
-Bad governance (embezzlement, poor prioritization)
-Siasa za maji taka (To politicize everything even crucial development issues)
-Rushwa
-Intellectual laziness
-Kaveli-
Wizara hizi zinahitaji ubunifu wa hali ya juu kuwaokoa watanzania÷
*Mama Ndalichako (elimu)
*Mama Umi mwalim (afya)
*Mama Angela Kairuki (utumishi)
Viongozi hawa waige kazi nzuri na kasi ya mama Jenister Mhagama, mama Tulia na mama Samia Suluhu.
Hebu Thibitisheni kwamba wanawake wanaweza na tupo 50/50. Wanawake wenzenu wanawaangalia nyinyi kama kioo chao, ongezeni juhudi na kupiga kazi pamoja na kutetea maslahi ya wananchi kikweli kweli. Sio kila siku kupewa lawama na kuwapa huzuni wananchi wenu.