Prof. Ndalichako awatupia lawama Bodi ya Mikopo kufanya kazi kwa mazoea, arejesha posho ya 8,500

WANASIASA ACHEN KUJITUNGIA MASWAL MNAPOHOJIWA BADALA YAKE MJIBU EXACTLY MLCHOULIZWA

MTANGAZAJ: asilimia ndogo ya wanafunz kupewa mikopo, Je uwezo wa serikal ndo umeishia hapo au wanafunz hawajakidh vigezo?
WAZIRI: nmetumia mda mrefu kuisafisha bod and bra braa brah nying

Asante sana mtangazaj wa tbc ulyeulza lile swal jana
wanasiasa weng wana hyo tabia badala ya kujbu walchoulzwa, wanajitungia tuswal twao rahs na kujibu
mnakera badiliken, kama hujui ni bora ukaomba muda ili ulitolee ufafanuz baadae.
Asante
 
Ukiwa mtendaji Unahitaji akili kubwa sana ya siasa kufanya kazi na serikali hii ya magu.
Juzi juzi wizara ilitoa tangazo tena kutoka kwa katibu mkuu wa wizara akielezea utaratibu mpya wa mikopo. Tumeshuhudia bodi ya mikopo ikinyanganywa mamlaka yake na wizara husika kuwa ndiye muamuzi mkuu wa maswala ya bodi. Leo waziri katika wizara hiyohiyo anakuja mbele ya watz anaitupia bodi lawama! Jamani!
 
Mi nadhani ilikuwa ni namna ya kuwafanya wanafunzi wasiombe ongezeko la boom maana maisha yamepanda bei huku serikali haina fedha. Hata hivyo baada ya muda tutajitokeza tena kuomba boom liongezwe kulingana na mahali chup kilipo.
 
Vya bure ni sumu na haitatokea Tz, elimu chuo kupewa bure, Mataifa yaliyoendelea kama America na Europe , yashindwe kutoa bure , Tz mnaanzia wapi wakat kila mara mnapiga magoti kuomba misaada? Tafakari kabla baada ya kusikia neno kwa upeo wako wote! Hata kutoa mikopo serikali imejitahidi sana, nchi za wenzetu hamnaga hizo, wanapewa discount katika ada na wazazi wanalipia watoto wao, ndo maana wanapomaliza wenzetu wanakuwa ni wazalendo kwa kusotea elimu kwa gharama zao. Wanabweteka na kukosa ubunifu kwa kusubiri vya bure!
Una uwakika au unaongea tu
 
Najivunia sana Daruso japo nshagraduate, yaani udsm pamekua.sehem salama ya mapambano ya haki za wanavyuo wote Tz, hata.boom lilivyopanda kutoka 3000 ni udsm walipambana hongereni sana vijana mnatufanya tuloopita ud kujivuna
 
Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Prof. Ndalichako amewatupia lawama bodi ya mkopo elimu ya juu kuwa wanafanya kazi kwa mazoea. Amesema pamoja na kutumia jitiada za kusafisha watumishi bodi hiyo amesema wapo watumishi bado wanafanya kazi kwa mazoea.

Prof. Ndalichako amesema ameyasikia malalamiko kutoka kwa wananchi na anayafanyia kazi na amesema wanafunzi wapewe mikopo semista hii kwa mwaka wa kwanza na wote bila kufuata mean tested.

Amesema lengo la serikali ni kuwapa wote wahitaji. Ameiagiza bodi ya mikopo kuwapa kama mfumo wa zamani na amesema bodi ya mkopo imekosea kuwapa wanafunzi shilingi elfu tano kwa miezi, kama pesa za kujikimu amesema bora kutompa.


Chanzo: TBC

Tatizo la wizara ya Elimu na serikali kwa ujumla ni kuendelea kuwatumia watendaji waliosababisha tatizo ili kulitatua. Hawa Loan board wanataka kumuhakikishia waziri kuwa walichokuwa wanakifanya kilikuwa sahihi na kuwa ni vigumu kudhibiti wanafunzi hewa. Ndiyo maana kila agizo serikali inalolitoa, linafanyiwa kazi na kuleta matokeo ya hovyo.

Mtu hawezi kuwa aliharibu makusudi halafu umpe njia ambayo itaonyesha kuwa alikuwa anafanya uzembe akaifanya sawasawa.

Kazi kwako waziri, kuendelea kufanya kazi nao au kuwaondoa uanze upya.
 
we are all together kwa hili lazma haki itendeke na kila m 2 apate haki yak, huwez kumpa m2 pesa ya kujikim 8500 n mwingjne unampa 350/=hata kama anasoma arts bt pesa ya kujikim haijalishi ww unaxoma arts o science
 
Bila umoja wa wana DARUSO wanafunzi wengi wa vyuo mbalimbali hapa nchini Tanzania wangeli teseka Sana Hongereni sana wana daruso kwa umoja wenu
Ndo Chuo kikuu kikubwa kilichopo Dar karibu na wizara ya elimu na HESLB hawana budi kupambania masilahi ya vyuo vyote.
 
Ndalichako ni Mama jasiri. Anatosha sana. Tatizo serikali yote haina fedha, sasa mnataka afanyaje?. Inni la tatizo liko pale karibu na IFM, sio Ndalichako
Ndalichenu ni profesa kikaza, jamaa wa udsm hawautambui uprofesa wake, ametunukiwa uprof na vyuo vya kufoji vya Wahindi
 
Back
Top Bottom