Prof. Mwandosya kugombea Urais 2015

Prof. Mwandosya kugombea Urais 2015

Ni vema wajitokeze wengi ili tuweze kuwachuja vizuri hatimaye kupata rais bora mmoja anayetakiwa na watanzania.

Acha kujipa uhalali wewe hii nchi sio ya chama kimoja...

Andika kumpata mgombea mmoja anayetakiwa na wanaCCM...
 
Ameongeza kwa kusema kwamba yeye hana fedha za kuwahonga wajumbe,
NAJIULIZA:KUMBE CCM HUWA WANAHONGANA KWENYE CHAGUZ ZAO?
 
Acha kujipa uhalali wewe hii nchi sio ya chama kimoja...

Andika kumpata mgombea mmoja anayetakiwa na wanaCCM...

ha ha ha haaaa,mgombea urais ambaye anasema yeye ni maskini,sidhan kama nchi hii ishawahi kuongozwa na tajiri
 
Huyo jamaa yenu fisadi amejaribu kuwaua wenzie ili apunguze ushindani lakini Mungu kamuumbua sasa watashindana naye wakati yeye mwenyewe afya mgogoro mkubwa. Muweke akiba maana hatapata urais aidha kwa afya au ufisadi

Mbona hamsemi Mungu kawachapa kiboko kwa unafiki wao? Ugonjwa kila mtu anaweza kuugua. Hata wewe hii leo unaweza kuugua pasi kusababishwa na mtu yeyote. Haya kuzushiana tache.
 
Ni vema wajitokeze wengi ili tuweze kuwachuja vizuri hatimaye kupata rais bora mmoja anayetakiwa na watanzania.

umekosea anayetakiwa na wana CCM na si watanzania

mbona mnaishi kwa mazoea hivyo ndugu zangu
 
Ni mgonjwa, ajiuguze aongeze siku zake duniani! Uraisi unahitaji mtu mwenye afya bora! TTCL amesahau?
 
Lowasa ndio moango mzima wapende wasipende,ilikendelea hivi viongozi wote wa ccm watagombea uraisi,halafu wanakuja kukaa na kusema lowasa ni mgonjwa ,Mungu atawaona na sisi tuliowengi tunamtaka Lowasa sasa na hapo ndipo patamu
 
Mbona hamsemi Mungu kawachapa kiboko kwa unafiki wao? Ugonjwa kila mtu anaweza kuugua. Hata wewe hii leo unaweza kuugua pasi kusababishwa na mtu yeyote. Haya kuzushiana tache.

Only time will tell. We can only pray that Tanzania does not go to the "dogs"
A good leader does not seek leadership at any cost. Kuna watu wamefika mahali wanaona kupta Urais ni haki yao na wengine hawana haki. Why not stay aside to enjoy the loot!
 
Mwigulu Nchemba amvaa tena Spika wa Bunge.

Naibu waziri wa Fedha anayeshughulikia Sera ndg Mwigulu Nchemba ambaye anajulikana kama Sokoine wa Pili amemvaa Spika wa bunge na kupinga vikali njama za bunge za kuupinga tena mswaada wa kufuta misamaha ya kodi. Itakumbukwa wakati wa bajeti wakati spika wa bunge akiahirisha mswaada wa sheria ya kodi ya ongezeko la thamani Mwigulu alisimama bungeni na kumpinga Spika waziwazi na kusema anaweka kumbukumbu sawa kuwa hakubaliani na uamuzi huo kwakuwa hauna nia njema na watanzania masikini. Mwigulu alisema bungeni kuwa utaratibu kuwatoza kodi masikini na kuwasamehe matajiri ni utaratibu wa kinyonyaji wenye lengo la kukuza pengo kati ya walionacho na wasio nacho.
"Nimekuwa nikichukizwa na utaratibu wa kusamehe matajiri na kutoza kodi masikini tangu siku nyingi, nilifurahi nilipopata fursa ya kuwa wizara ya fedha ili niwe sauti ya masikini, tumeleta mswaada wa kufuta misamaha isiyo na tija, imepita ngazi zote, leo mhe Spika kusema mswaada huu haujajadiliwa na wadau sio sahihi, mimi napingana vikali na maneno yako, huko ni kuwatumikia matajiri. Hivi kama tunawafutia matajiri misamaha ambayo imekuwa ikiwanufaisha kwa gharama za wanyonge kuendelea kuwa masikini leo unataka ukawaulize , kwanza utawauliza swali gani kuwa tunataka kuwafutia misamaha ya kodi? Unategemea watajibuje? Huku ni kutokuchukua majukumu, ni kutokuchukua uongozi na nikutokutimiza wajibu alisema mwigulu kwa ujasiri na kwa sauti ya uongozi.
Hata hivyo pamoja na Mwigulu kuongea kwa ujasiri na kuungwa mkono na watanzania wengi hasa masikikini, rai yake ilipuuzwa na mswaada huo haukujadiliwa. Kitendo hicho kilionekana wazi kuwa matajiri walitoa rushwa kwa wenyeviti wa kamati, kwa wabunge na hata kwa baadhi ya mawaziri.

Alikaririwa mfanyabiashara mmoja akisema Mwigulu haeleweki, yaani jamaa hana tamaa ya fedha, yuko kama Nyerere vile, hana gari, hana nyumba, hana biashara lakini hataki kuengea na wafanyabiasha kitu chochote yeye anasema tulipe kodi basi. Jamaa hanunuliki kabisa, sijui JK amemtoa wapi. Wewe angalia anavyokamata wakwepa kodi unafikiri mawaziri wengine hawawajui wakwepakodi? No, wanachukua chao wanaondoka, wanatuliza boli, tazama alivyovalia njuga kufuta misamaha kwa matajiru, hana urafiki, wenzake wote wanasema misamaha iachwe tu mpk spika, lakini jamaa akasimama kumpinga hata spika waziwazi. Kwa mjibu wa sheria spika akiongea anatakuwa kuongea waziri mkuu lakini jamaa mzalendo sana jambo la watanzania hata haogopi popote wakati wowote kuwatetea watanzania.

Tulipomuuliza Mwigulu kwanini anakazania sana misamaha ya kodi kwa matajiri ifutwe na kwanini wenzake hawakuyaona hayo miaka yote? Mwigulu anasema

Kwanza, wafanyakazi wanatozwa kodi kubwa na wanaishi maisha magumu kwasababu mzigo mzito wameachiwa wao kwakuwa matajiri wanasamehewa kodi. Angalia nchi ya watu milion 45 wanaolipakodi milioni 1.8. Sio sahihi, tunawasamehe wafanyabiashara matajiri, makampuni makubwa halafu tunawanyonya walimu na wafanyakazi masikini,

Pili, wafanyakazi wakilipa kodi ndizo zibatoa huduma kwa matajiri hivyo tunawalipa wafanyakazi mishahara midogo kwakuwa kodi ndogo toka kwao inahudumia na matajiri waliosamehewa kodi. Hili sio sahihi hata kidigo. Hii nikuongeza pengo la aliyenacho na wasionacho, hatuwezi kuwa na nchi moja wengine wakiishi kama ulaya huku wengine wakiwa na maisha magumu kwa kukamuliwa.

Tatu, mimi nimetokana na masikini kabisa wa Tanzania, nawajua masikini na naujua umasikini, kuna watu wanakosa huduma kwa ajili ya ufinyu wa makusanyo. Haiingii akilini kwamba tuna watoto wa masikini zaidi ya elfu 40 wakose mikopo ya kuibgia chuo kikuu huku tukiwa tumesamehe kodi migodi, makampuni, matajiri na wafanyabiasha, tunataka tufute misamaha tukusanye kodi tuwasomeshe watoto wa masikini.
Haiwezekani tukasamehe kodi migodi, makampuni tajiri na matajiri halafu tukahangaishane na wajane, yatima, wazee na masikini kuhusu ada elfu 20 ya sekondani.
Nataka nikusanye kodi halafu ada hizi elfu 20 zifutwe. "Tutoze kodi kwa matajiri tuwasomeshe watoto wa masikini" huu ndio mchango wa uwepo wangu mtoto wa masikini kwenye nafasi nyeti kwa masikini wa Tanzania.

Kadhalika, haiwezekani masikini wanakosa dawa, wanalala chini, wajawazito wanajifungua gizani huku matajiri wakisamehewa kodi, matajiri wakiugua wanatibiwa ulaya kwa kodi za masikini, tunataka kutoza kodi ili masikini wapate huduma za matibabu. Tunafuta misamaha ya kodi kwa matajiri ili tutoe huduma za matibabu kwa masikini.
Haiwezekani masini wanakosa maji, akina mama wanabakwa wakutafuta maji usiku huku tukisamehe kodi, tunataka tutoze kodi ilituwape masikini maji safi na salama.
Pia tunatoza kodi ili Nchi yetu iache utegemezi kwenye misaada yenye mashart na masimango.
Hata hivyo dawati letu limepata taarifa kuwa Mwigulu anapigwa vita na matajiri na hata viongozi wenzake waliowekwa mifukoni na matajiri. Zipo taarifa kuwa kamati ya bunge inapinga mswaada huo usiingie tena bungeni. Mwigulu alimuulixa Spika kwa ukali unataka mswaada huu usiingie bungeni watanzania masikini wamekukosea nini hata usiwahurumie? Tazama wafanyakazi wanatozwa kodi kubwa hivi, wanalipwa kidogo, hata hawawezi kuwahonga wabunge, mswaada huu kukwama, misamaha kutofutwa ni wito wa matajiri, kwanini unaitikia wito wa matajiri? Nimechukizwa sana na hili. Zipo taarifa kuwa matajiri wanaxungusha fedha kwenye kamati, kw wabunge na kamati ya uongozi ili wazuie mswaada huu kupitishwa.

Watanzania wote , wafanyakazi, wanafunzi tuliokosa mikopo, wanyonge, masikini, wazalendo tumuunge mkono ndg Mwigulu Nchemba, (Sokoine wa Pili) Mzalendo wetu wa Vitendo kupigania kodi ilipwe na matajiri ili masikini wapate huduma. Hata kwa maadamano tushinikize bunge lipitishe sheria ya kufuta misamaha ya kodi kwa matajiri. TUNAIMANI NA MWIGULU
 
Lowasa ndio moango mzima wapende wasipende,ilikendelea hivi viongozi wote wa ccm watagombea uraisi,halafu wanakuja kukaa na kusema lowasa ni mgonjwa ,Mungu atawaona na sisi tuliowengi tunamtaka Lowasa sasa na hapo ndipo patamu

mko weng wew na nan hebu toa takwimu acha kuengea kama unapuliza tarumbeta la kitchen part
 
Ndio hao hao wanaowatuma watu kusema Lowasa mgonjwa. Kweli vituko havitakaa viishe.
Baba Sekela nae! Anadhani watanzania ni wasahaulifu wa kiasi kikubwa kihivyo mpaka kusahau kashfa zake akiwa waziri wa mawasiliano!

We unaficha? mi nasema.
Namba moja: Mwandosya kwa uzinzi wake alilazimisha kimada wake apewe ticket ya safari za ulaya na aliponyimwa akalazimisha mkurugenzi mkuu wa TCRA aondolewe. Ngono tu! Brigedia mzima akaondolewa.

Namba mbili: inakuja baadaye
 
Naskiliza uchambuzi wa magazeti hapa kupitia Morning Magic, Prof Mwandosya nae amesema anataka kuwa raisi.Habari hii imeandikwa na Gazeti la MTANZANIA, NA UHURU.

Naona mbio zinapata washiriki wa kutosha hasa

ajiandae kwenda india kutoa sumu ya poloniam majamba kaka menzake hayatakubali anabisha ajaribu aone au amuulize mwa.kyembe
 
Yanajitangaza tu,siku Lowassa akifungua kinywa hawatalala
 
huyu mnyakyusa ? si anaumwa huyu mzee urais ataweza huyu?
 
Naskiliza uchambuzi wa magazeti hapa kupitia Morning Magic, Prof Mwandosya nae amesema anataka kuwa raisi.Habari hii imeandikwa na Gazeti la MTANZANIA, NA UHURU.

Naona mbio zinapata washiriki wa kutosha hasa

Kwa mtu yeyote aliyewahi kufanya kazi na Professor Mwandosya, atakuambia wazi kwamba kama kuna kigezo chochote cha kutambua kama mtu ni mwendawazimu au la, basi mwendawazimu ni yule anayemshutumu Prof Mwandosya bila kujua utendaji wake ukoje, kama wengi wanavyofanya katika hii thread.

Msemeni Prof. Mwandosya kuwa na mapungufu katika mambo yote, lakini sio katika kuwa mtu makini, mwenye akili na kuona mbali, mchapaji kazi, mzalendo na mtu ambaye kweli kweli anaweza kuipeleka nchii mbali akiwa raisi wa Tanzania. Na kama unamjua Mwandosya, huyu jamaa sio mwanasiasa, ni mtendaji, hivyo huwa anachukia sana ubabaishaji wa kisiasa. Na pia anakubalika sana kimataifa, kwa wale waliowahi kushuhudia uwezo na utendaji wake.

Muulizeni mtu yeyeote, kuanzia JK, Mawaziri na watu waliokuwa Wizara za Mwandosya watawaambieani ukweli juu yake.
Kwa hiyo acheni ubabaishaji kama kweli mnaitakia nchii hii uongozi makini na kuiondoa kwenye uozo wote wa mikataba ya madini, mafuta, gesi, umeme, uonevu wa mataifa makubwa nk.

Siku zote nimetamani sana serikali ya nchi hii yenye mchanganyiko wa watu kama Mwandosya, Dr. Slaa, Magufuli, Lissu, Lema, Mwigulu Nchemba, Manyika, Mdee, Mwakyembe, Mwesigwa, Zitto, Kafulila, January Makamba, nk. Labda hii itabaki kuwa ndoto tu.

Kikubwa kwangu ni mtu ambae anaweza kuipeleka Tanzania kunakojulikana, badala ya hawa vipofu wengi wanaojitokeza bila kuwa na dira ya wapi nchi iende. Mwandosya ni tofauti sana na utitiri wa koroboi mwingi unajitokeza kutaka uraisi. Mwandosya kwa Tanzania ni sawa na Clinton alivyokuwa kwa USA.
 
Ameongeza kwa kusema kwamba yeye hana fedha za kuwahonga wajumbe,
NAJIULIZA:KUMBE CCM HUWA WANAHONGANA KWENYE CHAGUZ ZAO?
Kwani wewe ulikuwa hujui?

Au huwa hufuatilii speech za Mwalimu Nyerere, ambapo katika hotuba yake mojawapo, aliwapasha wanaccm wenzake kuwa, baada ya yeye kuondoka madarakani, wanaccm wenzake waliotwaa mikoba, wamehalalisha utoaji na upokeaji rushwa, ambapo alibainisha kuwa CCM ya miaka hii, ukiwa ni bingwa wa kutoa rushwa, ndiyo inakuwa qualification no 1 ya wewe kuteuliwa kuwa mgombea wao, ambapo wakati wa enzi za utawala wake, mtu akibainika kugawa rushwa inakuwa disqualification no 1 ya kupigwa STOP kutogombea nafasi yoyote ya uongozi kwenye chama chao!
 
Naona hata NEC imeshindwa kuwadhibiti. Kigezo cha muda wa kutangaza haujafika.....it doesn't hold water any more. It is outdated.
 
Back
Top Bottom