Prof. Mwandosya kugombea Urais 2015

Prof. Mwandosya kugombea Urais 2015

Si mwingine ni Prof. Mark Mwandosya akiwa na mtangulizi wake Prof.Jakaya Mrisho Kikwete
 
Thread za kipuuzi kama hizi sijui kama Mods wataiacha! Labda waihamishie jukwaa la Photos!
 
Mtasubiri sana... Lowassa asipokuwa Rais kwa Ticket ya CCM basi UKAWA wataikomboa nchi hii kutoka kwenye Utumwa wa CCM ...
 
Mtasubiri sana... Lowassa asipokuwa Rais kwa Ticket ya CCM basi UKAWA wataikomboa nchi hii kutoka kwenye Utumwa wa CCM ...

Kama kuna utumwa wa CCM nchini, hata EL hawezi kutoboa!
 
Za Asubuhi, Jamani.

Leo nataka tumdiscuss kwa kina Mzee wetu, Prof Mwandosya, hasa Pale jina lake linapotajwa tajwa kuwepo kati ya wale wanataka kugombea Uraisi.

Kwa upande wangu....

Mzee wetu Sawa hana kashifa nzito yoyote wakati wake wote wa Utumishi, pia alikuwa alikuwa ameweza kuingia kwenye Tatu Bora,mwaka 2005. kwenye kinyang'anyiro cha kuteuliwa kuwa mgombea Uraisi kwa Tiketi ya CCM.

Kwa sasa imepita zaizi ya Miaka 50. Tangu tupate Uhuru, na changmoto za nchi hii ni nyingi sana, na Upepo wa sasa hivi wa kimaendeleo Tunamuhitaji Raisi ambaye,anaweza kukisimamia kile anachokiongea,awe holistic kwa kukemia Strongly Ufisadi pamoja Na Rushwa, na Awe Mfano ,aweze kuwachukulia hatua watu wote watakaojihusisha na mambo ya ufisadi pamoja na Rushwa Asiwe mtu wa kufunika Kombe mwanaharamu Apite. JE MZEE WETU MWANDOSYA ANAWEZA? Ataweza kuwakoromea viongozi wenzie na wanaccm wenzake wanaoafanya ufisadi na kuchukua Rushwa bila kuwafumbia Macho.

Pamoja na kwamba Tunataka Raisi Mwadilifu, Uadilifu uwe pamoja na kuwa Mkali na Mfano wa kuigwa na Mataifa mengine linapotokea Suala la Rushwa na Ufisadi.
 
Za Asubuhi m,Jamani...

Tuendelee kuchangia Uzi huu(tuache matusi)..........

Bajeti ya mwaka 2013/14 Mapato yote ya ongezeko la kodi yameyeyuka:

Mwaka 2013/14 yalifanyika maboresho ya sheria mbalimbali za kodi wakati wa Bunge la bajeti kodi ambazo kimsingi zilimwongezea mwananchi mzigo mzito wa kulipia kodi hizo kwa ajili ya kuongeza mapato ya Serikali na ili kuiwezesha serikali kuwahudumia wananchi wake .

Pamoja na ongezeko hilo la kodi ,ukweli mchungu ni kuwa fedha yote iliyokusanywa kutokana na ongezeko la kodi mbalimbali katika mwaka wa fedha 2013/14 imepotea yote katika wizara tatu tu za serikali kutokana na vitendo vya kifisadi, na hii ni kwa mujibu wa taarifa CAG .

Kodi zilizorekebishwa na mapato yake ni kama ifuatavyo;

a. Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148; kilipatikana kiasi cha sh.
48.977bilioni

b. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332;kilipatikana kiasi shilingi
131.686 bilioni

c. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147; kilipatikana kiasi cha shilingi
510.017 bilioni

d. Sheria ya Ushuru wa Mafuta, SURA, 220; kilipatikana kiasi cha shilingi
155.893bilioni

e. Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82 ;kilipatikana kiasi cha shilingi
28.213 bilioni

f. Sheria ya Usalama Barabarani, SURA, 168; kilipatikana kiasi cha shilingi
19.710 bilioni

g. Sheria ya Petroli (Petroleum Act) SURA, 392;kilipatikana kiasi cha shilingi 123.725 bilioni

Hali hiyo ilifanya marekebisho yote ya sheria za Kodi zilizofanywa katika mwaka huo wa fedha kuiwezesha serikali kukusanya jumla ya shilingi 1.018 Trilioni katika mwaka wa Fedha 2013/2014 na hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Hansard ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Hali hii haikubaliki na haivumiliki hata kidogo. Hapa tumezungumzia Wizara tatu tu za serikali kuu bado wizara 30 na idara mbalimbali za Serikali ikiwa ni pamoja na Halmashauri na Taasisi na Mashirika ya Umma.
Ripoti hizi zimezidi kudhihirisha kwa mara nyingine kuwa matatizo yanayowakabili Watanzania ikiwa ni pamoja na umaskini, maradhi, ujinga yanaendelea kudumu kwa sababu watawala wa Serikali ya CCM wameamua yaendelee kuwepo kwa kukumbatia adui wa nne ambaye ni ufisadi.

Ripoti hizo za CAG ambazo zimeanika ufisadi katika maeneo yaliyokaguliwa ikiwemo Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, mashirika ya umma na miradi ya maendeleo, kwa mara nyingine zimedhihirisha wazi kile ambacho CHADEMA kimekuwa kikisema kwa muda mrefu kwamba ufisadi huu unaoendelea kulitafuna taifa na kuwafanya Watanzania wazidi kuwa maskini ni matokeo ya kushindwa kwa sera, mikakati na mipango ya CCM.

Wakati kasi ya ufisadi inaongezeka kutoka mwaka hadi mwaka kwenye Serikali ya Rais Jakaya Kikwete chini ya usimamizi wa CCM, ndivyo serikali hiyo hiyo inaongeza kasi ya kushindwa kusimamia UWAJIBIKAJI ambayo ndiyo moja ya nguzo muhimu katika kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanaonekana katika kuboresha maisha ya wananchi hususan kuweka fursa za kujitafutia maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hatimaye ustawi wa jamii nzima.

Ufisadi huu hauvumiliki tena. Watanzania wasikubali kuendelea kubeba mizigo ya watawala walioshindwa kutekeleza wajibu wao. Hali ya siasa inazingirwa na sintofahamu kubwa. Uchumi unazidi kuyumba. Kijamii, maisha yazidi kuwa magumu na walioko madarakani wamelewa madaraka. Msamiati wa UWAJIBIKAJI haumo vichwani mwao tena.

Ni mwaka wa Watanzania kuamua kuachana na ufisadi huu.

JE ATAWEZA KUKEMEA HUU UFISADI?

ccm hakuna msafi binti,subiri waje na uchafu wake humu utashangaa.Hii nchi inahitaji dikteta sasa ili ikwamuke kwenye huu mkwamo,nikimuangalia le profeseri namuona amelegea kama uji wa mgonjwa!!!!
 
Tanzania kwa sasa hahitaji kiongozi wa kaliba ya akina Mwandosya kabisaaaaaa,....jamaa apumzike kwa amani.
 
Huyu si ndiye alinunuliwa na Mohamed Dewji akaidhinisha kusafirishwa kwa zile boti kupitia barabara kwenda Mwanza, huku akijua wazi uzito wake ungaharibu barabara? Isingekuwa Magufuli kukomaa barabara zetu kwisha...
 
"Bungeni leo" Katika kipindi cha maswali kwa waziri mkuu leo bungeni, Kafulila amemuuliza Mh. Pinda juu ya Serikali kuendelea kumlipa Seti wa IPTL zaidi ya shilingi Bilioni 5 kila mwezi kama capacity Charges, wakati umiliki wake ni feki, pamoja na mahakama kudhibitisha hivyo!

Pinda hakujibu hilo baada ya Madame Spika, kumzuia kutoa majibu ya suala hilo kwa sababu 'eti' ni swali jipya.!

JE PROFESA ATAWEZA KUPAMBANA NA HAWA WATU?
 
Mwandosya ni mzuri lakini si rais anayetufaa kwa sasa....Sasahivi tunahitaji mtu radical ambaye atageuza mambo chini juu juu chini..misingi hiyo ikishawekwa, hapo tunaweza kumkaribisha le profeseri..
Mtu pekee anayeweza kugeuza mifumo ya kishenzi ni Magufuli...
 
Chamani kwa muono wangu hakuna....maana lazima atahitajika kulipa fadhila na matokeo yake munayajuwa.
 
Prof. Mark Mwandosya mbunge wa jimbo la Rungwe Mashariki na Waziri asiyekuwa na wizara maalum amesema kuwa hatogombea tena ubunge bali urais. Ni mwendelezo wa wimbi la watangaza nia linaloshika kasi.

Chanzo : Mtanzania gazeti la leo.

Politics! Wanataka kumtumia Mzee wa watu kujikosha maana Prof ni mmoja wa viongozi wasio na sifa mbaya kama wengine (Sijasema ni msafi 100%). Ni vema akalitambua hilo, la sivyo anaweza kuja beba mizigo ya wengine na akajikuta anakabiliwa na msongo utakaomgharimu pakubwa....Amuulize Levy Mwanawasa (RIP)
 
Za Asubuhi, Jamani.

Leo nataka tumdiscuss kwa kina Mzee wetu, Prof Mwandosya, hasa Pale jina lake linapotajwa tajwa kuwepo kati ya wale wanataka kugombea Uraisi.

Kwa upande wangu....

Mzee wetu Sawa hana kashifa nzito yoyote wakati wake wote wa Utumishi, pia alikuwa alikuwa ameweza kuingia kwenye Tatu Bora,mwaka 2005. kwenye kinyang'anyiro cha kuteuliwa kuwa mgombea Uraisi kwa Tiketi ya CCM.

Kwa sasa imepita zaizi ya Miaka 50. Tangu tupate Uhuru, na changmoto za nchi hii ni nyingi sana, na Upepo wa sasa hivi wa kimaendeleo Tunamuhitaji Raisi ambaye,anaweza kukisimamia kile anachokiongea,awe holistic kwa kukemia Strongly Ufisadi pamoja Na Rushwa, na Awe Mfano ,aweze kuwachukulia hatua watu wote watakaojihusisha na mambo ya ufisadi pamoja na Rushwa Asiwe mtu wa kufunika Kombe mwanaharamu Apite. JE MZEE WETU MWANDOSYA ANAWEZA? Ataweza kuwakoromea viongozi wenzie na wanaccm wenzake wanaoafanya ufisadi na kuchukua Rushwa bila kuwafumbia Macho.

Pamoja na kwamba Tunataka Raisi Mwadilifu, Uadilifu uwe pamoja na kuwa Mkali na Mfano wa kuigwa na Mataifa mengine linapotokea Suala la Rushwa na Ufisadi.

Issue ni kwamba mwandosya anabebwa na Kikwete,na unafahamu kabisa kwamba kikwete ameshindwa kuwa na impact katika uongozi wake,so mwandosya ni chali tayaru
 
Ni habari njema kwa watanzania Baada ya Prof mark mwandosya kutangaza kuchukua fomu ya kogombea nafasi ya Urais kupitia chama Tawala cha CCM. Hakika huyu ndio Rais wa Tanzania ajaye kwani ana utendaji wa Kazi uliotukuka na Hana Doa hata kidogo na haitawawia Vigumu CCM kumnadi kwa Wananchi, Watanzania huyu ndiye Rais anayestahili tumuunge mkono kwa nguvu zetu zote.
 
Back
Top Bottom